meneja masoko wa Kampuni ya Yara Tanzania Ltd Linda Byaba akizungmza na waandishi wa habari katika Ofisi za YARA Tanzania zilizopo Kurasini jijini Dar es Salaam
Meneja Masoko wa Kampuni ya uzalishaji Mbolea ya Yara , Linda Byaba akionyesha ubora wa mbolea aina ya YaraMila Otesha leo jijini Dar es Salaam.
Meneja Masoko wa Kampuni ya uzalishaji Mbolea ya Yara , Linda Byaba akionyesha ubora wa
mbolea aina ya YaraMila Otesha leo jijini Dar es Salaam.
Meneja Masoko wa Kampuni ya Uzalishaji Mbolea ya Yara , Linda Byaba akizungumza na
waandishi habari kuhusiana na punguzo bei ya mbolea ya YaraMila Otesha leo jijini Dar
es Salaam.
Kampuni ya usambaaji mbolea ya Yara Tanzania imepunguza
ghara ya maMbolea YaraMila Otesha kwa asilimia 50 ili kuwezesha wakulima wazalishe mazao
bora yatayongia katika viwanda vya bidhaa mbalimbali.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Meneja Masoko wa
Kampuni hiyo, Linda Byaba amesema kupunguza bei ya mbolea kwa asilimia 50
ni kuwawezesha wakulima waweze kumudu gharama hizo.
Amesema Yara ni kampuni inayoongoza duniani kwa uzalishaji wa mbolea
zenye virutubisho linganifu kama YaraMila. Kila punje moja ya YaraMila
ina virutubisho vyote kama Nitrojeni, Fosiforasi, Kalisiam, Boroni,
Magniziam kwa ajili ya kuupa mmea lishe linganifu.
Byaba amesema wakulima wanaozalisha mazao ya nafaka, kahawa, chai,
sukari, tumbaku, alizeti, viazi na mbogamboga wanafaidika na mbolea
zenye virutubisho kupitia matawi yake yaliyopo Tanzania
na Rwanda.
Amesema faida za mbolea hii ya Kupandia ya YaraMila Otesha ,
lishe linganifu ya mmea ,ni mbolea ya NPK yenye kiwango cha juu
cha kirutubisho cha Fosforasi na ina jumla ya virutubisho
7 kulinganisha na mbolea zingine za kupandia, haichachushi
wala udongo,huchochea uotaji wa mizizi mingi hivyo kuufanya mmea
kuwa imara muda wote,huchochea machipukizi mengi yanayoleta mavuno mengi
katika zao la mpunga.
Aidha amesema faida zingine ni kuyeyuka kwa haraka zaidi kwenye udogo
na kufanya mmea upate vizurubishovyake stahiki kwa muda unaohitajika Pamoja
asilimia 50% ya ongezeko la uzalishaji kwa wakulima waliotumia.
Comments