Na Heri Shaaban
JUMUIYA ya Wazazi Wilaya ya Ilala yakerwa na watendaji wasiojua majukumu yao..
Hayo yalisemwa Dar es salaam Jana, na Katibu wa Wazazi Wilaya ya Ilala
Sophia Hamadi katika ziara ya kamati ya utekelezaji wilaya va Ilala
walipokuwa jimboni SEGEREA kuangalia uhai wa jumuiya.
" Sirizishwi na nafasi zilizo wazi katika jumuiya hii ya wazazi has a kata ya SEGEREA " alisema Sophia
Alisema kila kazi INA misingi yake ukichaguliwa lazima utekeleze
majukumu sitaji kuona nafasi zinapwaya bila kuzibwa huyo atakakuwa sio
kiongozi ambaye yupo nyuma kimaendeleo .
Aidha Sophia alisema Mara. Baada ya ziara hiyo atashuka chini ngazi ya matawi kuangalia kama vikao vinafanyika.
Alisema dhumuni lingine la ziara hiyo kujua idadi ya wazee waliopo kila kata, kujua idadi ya Shule na zahanati.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Wazazi Wilaya ya Ilala Lucas Lutainurwa
alizitaka kila jumuiya kuanzisha vikundi vya uzalishaji
vitakavyowakomboa kiuchumi.
Lucas alisema jumuiya hiyo ikiwa na vikundi itasaidia wanachama wake kuendesha jumuiya hiyo bila kuwa ombaomba.
Wakati huo huo aliagiza
Makundi yalio katika Jumuiya hiyo Kuvunjwa badala yake washirikiane katika kuongeza wanachama na kufatilia hada kwa wakati.
Alisema chaguzi zilishakwisha tushirikiane tuwe wamoja na kuakikisha idadi ya wanachama inaongezeka.
Comments