Licha ya Jokate Mwegelo aka Kidoti kuachana na Hasheem Thabeet kwenye mahusiano yao ambayo yalidumu kwa takribani miaka mitatu, bado wawili hao wameonyesha kutokuwa maadui na wameendelea kuwa watu wa karibu.
Jokate ameonyesha kupokea zawadi ya maua kutoka kwa mchezaji huyo wa kikapu kwa ajili ya kusherehekea siku yake ya kuzaliwa ambayo ilikuwa Jumanne ya March 20 ya mwaka huu.
Kidoti ameweka picha ya zawadi hiyo ya maua kwenye mtandao wa Instagram na kuandika ujumbe ambao unasomeka, “Still receiving birthday roses. Thank you Sheemy @hasheemthedream @bloom_eventfully for the delivery .”
Hata hivyo kwa sasa kubwa linalosubiriwa kwa mrembo huyo ni ndoa yake ambapo katika siku yake hiyo ya kuzaliwa alithibitisha kuwa yupo mbioni kuolewa japo hakumtaja mwanaume ambaye atafunga naye ndoa
Comments