“Viongozi Wakuu wa Chadema akiwepo Mwenyekiti wa Chama hicho Taifa, Freeman Mbowe waliokuwa wameripoti Kituo Kikuu cha Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam wakitimiza masharti ya dhamana yao wamewekwa mahabusu.
Taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Idara ya Mawasiliano na Habari CHADEMA, Tumaini Makene imeeleza kuwa Polisi hawajaeleza sababu ya kufanya hivyo ila Mawakili wanashughulikia.
“Viongozi Wakuu wa Chama pamoja na wabunge waliokuwa wameripoti Kituo Kikuu cha Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam wakitimiza masharti ya dhamana yao, wamewekwa mahabusu. Polisi hawajaeleza sababu ya kufanya hivyo. Mawakili wetu wanashughulikia. Tutaendelea kuwapatia taarifa zaidi,” amesema Makene.
Viongozi walioripoti Polisi ni Mwenyekiti wa Chadema Taifa,Freeman Mbowe,Katibu Mkuu wa chama hicho Dkt. Vicent Mashinji ,Naibu Katibu Mkuu Bara, John Mnyika,salum Mwalimu na Mweka Hazina wa Baraza la Wanawake (Bawacha)Esther Matiko.
Comments