Watafiti wanasema Faru mweupe wa mwisho wa kiume duniani anayejulikana kwa jina la Sudan amefariki kufuatia matatizo aliyokuwa nayo yaliyochangiwa na umri wake. Taarifa kutoka hifadhi ya wanyama ya Ol Pejeta nchini Kenya imesema faru huyo aliyekuwa na umri wa miaka 45 alidungwa sindano ili afe, baada ya hali yake kiafya kuwa mbaya zaidi hadi kufikia hatua ya kushindwa hata kusimama.
Faru huyo alikuwa ni moja ya matumaini na juhudi za kuendelea kulinda Faru hao wasitoweke kwa msaada wa Faru wengine wawili wa kike. Faru Sudan alikuwa ni balozi mzuri na atakumbukwa kwa kazi aliyofanya ya kuhamasisha juu ya madhira siyo tu yanayowakabili Faru pekee bali pia jamii ya wanyama wengine walio katika hatari ya kutoweka kutokana na shughuli zinazofanywa na binaadamu.
Chanzo: DW Ujerumani
Comments