Skip to main content

Posts

Showing posts from September, 2015

Mganga wa Chelsea aamua kuondoka

Daktari Eva Carneiro akionekana kujibizana na Jose Mourinho Daktari wa Chelsea Eva Carneiro ameamua kuondoka klabuni hapo wiki sita baada kukosolewa na kocha Jose Mourinho. Carneiro alidharauliwa na Mourinho ambaye alisema kuwa daktari huyo ni mwoga kwani alimtibu Eden Hazard wakati wa 2-2 dhidi ya Swansea Agosti 8. Mourinho akimpigia kelele Eva Carneiro (hayupo pichani) Chelsea walimuomba Carneiro, 42, arudi kazini, lakini alikataa na sasa anafikiria kuwaburuza mahakamani. Chama cha soka cha Uingereza FA kinachungumza malalamiko kwamba Mourinho alitumia lugha chafu dhidi yake. Eva na Fearn wakijaribu kumtibu Eden Hazard Chelsea wamesema hawazungumzii masuala ya ndani ya timu.

Diego Costa kukosa mechi tatu

Costa akimkwaruza Koscielny usoni Diego Costa atakosa michezo mitatu baada ya chama cha soka cha England FA kuthibitisha kukutwa na makosa. Costa alikana mashtaka yaliyokuwa yakimkabili kuhusiana na kumfanyia fujo mlinzi wa Arsenal Laurent Koscielny katika ushindi wa goli 2-0 dhidi ya Arsenal. Na kisha kumsukuma chini Costa mwenye miaka 26 alionekana kuweka mikono yake juu ya uso wa Koscielny kabla ya kuanza kuzozana na Gabriel Paulista ambaye baadaye alitolewa nje kwa kadi nyekundu. Mlinzi huyo wa Arsenal alitolewa nje na mwamuzi Mike Dean kwa kumfanyia vurugu mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Hispania. Costa akikwaruzana na Gabriel ambaye alionyeshwa kadi nyekundu baadae Costa atakosa mchezo wa kombe la ligi dhidi ya Walsall siku ya jumatano sambamba na ile ya ligi kuu kati ya Newcastle na Southampton. Baada ya kuthibitisha kuwa mwamuzi wa mchezo hakuona tukio la Costa na Koscielny, chama cha soka England kimesambaza kanda hizo za

CCM: Hatushangai

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimeeleza kutoshangazwa na matokeo ya utafiti wa taasisi huru ya Twaweza yaliyotoa ushindi wa asilimia 65 kwa Mgombea Urais wao, Dk John Magufuli, huku kikiahidi kuongeza kasi, nguvu na mikakati zaidi katika nusu ya pili ya kampeni. Hata hivyo, kimeshangazwa na taharuki hasa kutoka miongoni mwa wasomi na wanaharakati, kuhusu matokeo ya utafiti huo na kusema kilitegemea wasomi na wanaharakati hao wangefurahia utamaduni wa tafiti za kisiasa ulioanza kujitokeza nchini kwa vile unajenga. Pia kimesisitiza kuwa kimethibitisha kushiriki mdahalo wa wagombea urais ulioandaliwa na Baraza la Habari Tanzania (MCT), lakini kikisitiza uwashirikishe wagombea wenyewe na si wawakilishi wao, na pia wagombea wote, hasa wa vyama vikuu wawepo na washiriki . Juzi, Taasisi ya Twaweza ilitoa matokeo ya utafiti wake kuhusu ‘Sauti za Wananchi’ kwenye siasa na kuonesha kuwa, kama uchaguzi huo ungefanyika juzi, Dk Magu

Kutoka faceboo

Sebastian Maganga "Tuufyeke uso wa haya, pindi ambapo tunatengeneza "listi" ya watu wa maana katika maisha yetu, kwani katika kila kundi kubwaaa tunalofahamu, kuna wale kadhaa tu ambao watakuwa makini kujenga faida naasi, wengine woote watakuwa mizigo inayotupunguzia kasi katika safari zetu za mafanikio" nukuu kutoka kwa afisa mhamasishaji mkuu bwana Steve harvey..je?? Umeandika listi lakini??

Ligi Daraja la Kwanza nchini kuwasha moto kesho

Ligi Daraja la Kwanza nchini (FDL) inatarajiwa kuanza kutimua vumbi kesho Jumamosi Septemba 19 kwa michezo 10 kuchezwa katika viwanja mbalimbali nchini, ambapo jumla ya timu 24 zinashirki ligi hiyo zitaanza kusaka nafasi tatu za juu ili kuweza kupanda Ligi Kuu msimu ujao. Kundi A, Polisi Dar watakuwa wenyeji wa Friends Rangers kwenye uwanja Mabatini mkoani Pwani, Mjii Mkuu ya Dodoma watapambana na Polisi Dodoma kwenye uwanja wa Jamhuri mjini humo. Kundi B, Polisi Morogoro watacheza na Burkina Faso uwanja wa Jamhuri Morogoro, Njombe Mji FC watacheza na Kurugenzi uwanja wa Amani mjini Njombe, Lipuli ya Iringa watawakaribisha Kimondo FC Uwanja wa Wambi- Iringa na JKT Mlale watakua wenyeji wa Ruvu Shooting katika uwanja wa Majimaji mkoani Ruvuma. Kundi C, Mbao FC watawakaribisha Geita Gold uwanja wa CCM Kirumba, Rhino Rangers watacheza dhidi ya Polisi Tabora uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora, Panone FC watawakaribisha JKT Oljoro katika uwanja wa Ushirk

The Cure - "Lovesong".

Beef Jay Z Vs Nas

 

Taarifa kuhusu ajali iliyotokea kwenye Msikiti Mkuu Saudi Arabia

Hii taarifa imegusa Vichwa vya Habari vya Vyombo vingi vya habari Duniani, inahusu ajali ambayo imetokea wakati watu wakiwa ndani ya Msikiti Mtakatifu wa Mecca, Saudi Arabia ambako waumini wengi wa Dini ya Kiislamu huwa wanakwenda kwa ajili ya Hijjah.Ajali hiyo inahusisha winch kubwa ambalo lilikuwa likitumiwa kwenye ujenzi eneo la jirani na Msikiti huo kuangukia Msikiti huo, ambapo kwa wakati huo kulikuwa na watu zaidi ya 800 wakiendelea na sala ndani ya Msikiti. Kumekuwa na wasiwasi mkubwa kuhusu usalama wa watu wanaoenda kwenye Msikiti huo kutokana na maeneo yanayozunguka Msikiti kuna majengo mengi yanayoendelea kujengwa na kukarabatiwa pamoja na Ms

MWANA FA FEAT G NAKO MFALME

Rais JK awapo pole majeruhi wa Uwanja wa Jamhuri, Morogoro

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro Dkt. Ritha Lyamuya alipokwenda kuwapa pole majeruhi walioumia katika msongamano mkubwa uliotokea katika mlango wa kutokea nje baada ya mkutano wa kampeni wa CCM katika Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro Septemba 6, 2015. Watu wawili walipoteza maisha, akiwemo mvulana wa miaka 12 aliyejulikana kwa jina la Ramadhani Abdallah na mwanamama Grace George (42), ambapo jumla ya watu 17 walijeruhiwa na kukimbizwa hospitalini hapo. Hadi jioni hii majeruhi saba walikuwa wameruhusiwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Kaimu Mganga Mku wa Hospitali ya Mkoa wa Morogoro Dkt. Samson Tarimo alipokwenda kuwapa pole majeruhi walioumia katika mlango wa kutokea nje baada ya mkutano wa kampeni katika Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro Septemba 6, 2015 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mweka Hazina wa CCM mkoa wa Morogoro Ndg. Hassan Bantu alipokwenda

Lowassa aiteka Kibamba

Wakazi wa Jimbo la Kibamba jijini Dar es Salaam wajitokeza kumlaki mgombea urais wa Ukawa Edward Lowassa Septemba 7, 2015 Ni ishara ya Lowassa Mabadiliko, Mabadiliko Lowassa Edward Lowassa akiongozana na Freeman Mbowe kwenda kufanya kampeni katika jimbo la Kibamba jijini Dar es Salaam Lowassa akimtambulisha mgombea ubunge Jimbo la Kibamba John Mnyika kwa wakazi wa eneo hilo Edward Lowassa akilakiwa na mamia ya wakazi wa Kibamba Lowassa akiwasalimia wakazi wa Kibamba Lowassa akionyesha ishara ya kuwasalimia kwa dhati wakazi wa Jimbo la Kibamba jijini Dar es Salaam Mamia ya wakazi wa Kibama wajitokeza kumlaki Edward Lowassa Mabadiliko Lowassa, Lowassa Mabadiliko Meza Kuu (kutoka kushoto) Frederick Sumaye, Edward Lowassa, Freeman Mbowe, Salim Mwalim Mwnedo wa Mabango tu Mbunge wa Kawe Halima Mdee akizungumza na wakazi wa jimbo la Kibamba Mgombea urais Edward Lowassa akizungumza na wakazi wa Jimbo la Kibamba Septemba 8, jijini Dar

Mwanafunzi mwerevu apata alama 0 !

Maelfu ya wazazi na wanafunzi wamejitokeza kumuunga mkono mwanafunzi mmoja shupavu aliyepata sufuri katika mtihani wake wote wa mwisho. Amini usiamini,Mariam Malaka ambaye amekuwa mwanafunzi wa kupigiwa mfano nchini Misri kutokana na alama za juu alizopata katika mitihani ya awali, alikuwa na matarajio ya kuzoa alama ya juu zaidi yaani A itakayomwezesha kujiunga na chuo cha mafunzo ya daktari lakini wapi ? Katika mtihani wake wa mwisho Mariam Malak alipewa alama za chini zaidi . Hii ikimaanisha kuwa, bi Malak hakuandika hata herufi moja aliyojibu kikamilifu. Bi Mariam Malak anashuku kuwa kulitokea kosa kubwa kwani yeye alivyofanya mtihani huo hadhani kama angeufeli. ''Kwa kweli sikuamini macho yangu eti nimefeli mtihani wa mwisho'' bi Mariam Malak aliiambia BBC.

Heart of a City (Ain't No Love) - Jay Z

MUSSA: WATU WALIKUWA WANAIPA NIGERIA NAFASI YA KUSHINDA LAKINI MAMBO YAMEKUA TOFAUTI

Ahmed Mussa, nahodha wa timu ya Taifa ya Nigeria ‘Super Eagles’ Nahodha wa Nigeria Ahmed Mussa amesema, soka la sasa halina timu kubwa wala ndogo. Huku akisema kwamba watu walikuwa wakiipa nafasi kubwa Nigeria ya kushinda kwenye mchezo wao dhdi ya Stars lakini mambo yamekuwa tofauti “Mchezo wetu umemalizika vizuri na sasa uaweza kuona kwamba hakuna timu ndogo wala kubwa kwenye mchezo wa soka. Watu walikuwa wanasema Nigeria ni taifa kubwa kimpira ukilinganisha na Tanzania huku wakitupa sisi nafasi ya kushinda mchezo wa leo  lakini mambo yamekua tofauti”. “Kocha bado anatengeneza timu yake naamini baada ya mechi kadhaa tutakuwa vizuri japo nimefurahi kwa jinsi tulivyocheza leo. Kipindi cha kwanza tulishikwa lakini kipindi cha pili tukacheza vizuri”.Inatoka http://shaffihdauda.co

STARS NA SUPER EAGLES KATIKA PICHA JANA UWANJA WA TAIFA

Mshambuliaji wa Tanzania, Mbwana Samatta akimtoka beki wa Nigeria, Solomon Kwambe katika mchezo wa Kundi D kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika jana Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Timu hizo zilitoka 0-0.   Mshambuliaji wa Taifa Stars, John Bocco akipambana na beki wa Nigeria, Kenneth Omeruo Mshambuliaji wa Tanzania akijiandaa kupiga mpira mbele ya beki wa Super Eagles, Kenneth Emeruo Winga wa Tanzania, Simon Msuva akimtoka beki wa Super Eagles, Kenneth Emeruo Beki wa Tanzania, Mwinyi Hajji Mngwali akimtoka winga wa Nigeria, Ahmed Musa huku Nwankwo Obiora (kulia) akiwa tayari kutoa msaada Winga Farid Mussa wa Tanzania akimtoka beki wa Nigeria, Kingsley Madu Kiungo wa Tanzania, Mrisho Ngassa akitafuta maarifa ya kuwatoka wachezaji wa Nigeria Kipa wa Nigeria, Carl Ikeme Onora akidaka mpira wa juu jana

MAMA SAMIA AMALIZA ZIARA YA KAMPENI MKOA WADAR ES SALAAM

 Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan, akihutubia maelfu ya wananchi katika mkutano wa kampeni uliofanyika leo eneo la Majohe kwa Warioba, jimbo la Ukonga, Dar esSalaam, leo.  Wananchi wakimshangilia Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia, alipohutubia mkutano wa kampeni leo katika jimbo la Ukonga, Dar es Salaam  Mgombea Ubunge jimbo la Ukonga, Jerry Silaa, akiwahutubia wananchi katika mkutano wa kampeni wa Mgobea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia,uliofanyika katika jimbo hilo leo.  Maelfu ya waanchi wakimsikiliza Mgombea Ubuge jimbo la Ukonga, Jerry Silaa alipowahutubia mkutano wa kampeni katika jimbo hilo leo. (P.T)  Wema Sepetu (kushoto) akiwa na wasanii wenzake ambao wamo katika kampeni ya MAMA ONGEA YA MWANAO AMPE KURA DK. MAGUFULI, kumsaidia Mgomb