Diego Costa atakosa michezo mitatu baada ya chama cha soka cha England FA kuthibitisha kukutwa na makosa.
Costa alikana mashtaka yaliyokuwa yakimkabili kuhusiana na kumfanyia
fujo mlinzi wa Arsenal Laurent Koscielny katika ushindi wa goli 2-0
dhidi ya Arsenal.
Costa mwenye miaka 26 alionekana kuweka mikono yake juu ya uso wa
Koscielny kabla ya kuanza kuzozana na Gabriel Paulista ambaye baadaye
alitolewa nje kwa kadi nyekundu.
Mlinzi huyo wa Arsenal alitolewa nje na mwamuzi Mike Dean kwa kumfanyia vurugu mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Hispania.
Costa atakosa mchezo wa kombe la ligi dhidi ya Walsall siku ya
jumatano sambamba na ile ya ligi kuu kati ya Newcastle na Southampton.
Baada ya kuthibitisha kuwa mwamuzi wa mchezo hakuona tukio la Costa
na Koscielny, chama cha soka England kimesambaza kanda hizo za vidio kwa
waamuzi wakongwe watatu wa zamani.
Chanzo: BBC Swahili
Comments