Skip to main content

Posts

Showing posts from September, 2014

Diamond :Ampa zawadi ya gari Wema

  Jumapili ya September 28 ilikuwa ni siku ya kuzaliwa mrembo aliyebeba taji la Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu. katika kusheherekea siku hiyo mpenzi wake Nasib Abdul a.k.a Diamond Platnumz alithibitisha kwa vitendo kuwa mapenzi yao bado yako imara, kwa kumnunulia zawadi ya gari jipya aina ya Nissan. Picha ya gari hilo la rangi nyeusi iliambaatana na ujumbe mzuri ambao Diamond alimwandikia wema kupitia akaunti yake ya Instagram yenye followers 236,841. “Nlitama nikupe vingi, wenda ingenisaidia kueleza ni kias gani napenda nikuone ukifurahi kwenye siku yako hii ya kuzaliwa…lakini tu sina uwezo huo mumy… tafadhari pokea kidogo hichi nlichojaaliwa leo….” Huku akionesha gari hilo pichani

Wandamanaji wakesha Hong Kong

Mamia ya waandamanaj wa Hong Kong wamezingirwa na Askari polisi wanaowataka kusitisha maandamano na mkusanyiko wao karibu na ofisi za Makao makuu ya serikali. Waratibu wa maandamano hayo wamekaidi amri hiyo na kuwataka watu wengine zaidi kujitokeza ili kuwaunga mkono katika madai yao ya kuitaka China iwaachie uhuru wa kumchagua kiongozi wao katika uchaguzi ujao wa mwaka 2017. Kiongozi wa Mamlaka ya Hong Kong C Y Leung amesema serikali yake imesikiliza na kuzingatia madai ya waandamani lakini inapingana na mpango wao wa kujitenga. ''Mimi na serikali yangu tutazingatia sheria za msingi na uamuzi unaostahili wa NPCSC,tutajaribu juhudi zote kutekeleza uchaguzi wa kiongozi mkuu kwa kila anayestahili kupiga kura atafanya hivyo mwaka 2017. Serikali itaanzisha hatua inayofuata ya majadiliano kuboresha katiba hivi hivi karibuni. Inasihi sekta mbalimbali za jamii kushiriki katika m

Tibaigana: Wapinzani wana haki kuandamana

Alfred Tibaigan Katika mahojiano maalumu na gazeti la Mwananchi nyumbani kwake Buganguzi wilayani Muleba, Kamishna Tibaigana alisema suala la maandamano halikumsumbua kwa kuwa alielewa kuwa sheria inayaruhusu, hivyo alichokuwa akifanya ni kuwaita viongozi wa vyama vinavyotaka kuandamana na kufanya nao makubaliano ya namna maandamano hayo yanavyopaswa yafanywe kabla ya kuyaruhusu. "Pengine hiyo ndiyo sababu sikuwahi kushambuliwa kwa maneno ya kejeli au matusi na wanasiasa kwa kuwa sikuwahi kuzuia maandamano yao bila sababu na hata kama kulikuwa na sababu niliwaita na kuwaeleza na tulikubaliana. "Kikubwa ni kujenga tabia ya kuwaita viongozi wa waandamanaji na kujadiliana nao, vinginevyo wanaweza pia hata kukufikisha mahakamani wakipinga kuzuiwa maandamano yao," alisema Tibaigana ambaye alikumbana na sakata la kudai maandamano wakati akiwa Kamanda kwenye mikoa ya Tanga, Arusha na Dar es Salaam.

Rooney awaomba msamaha wenzake

  Wazza aliwaomba radhi wachezaji wenzake kwa kitendo hicho. Wayne Rooney amesema aliomba radhi kwa wachezaji wenzake baada ya kutolewa nje dhidi ya West Ham siku ya Jumamosi. Nahodha wa Manchester United alitolewa nje kwa kumchezea rafu mbaya Stewart Downing na kusema hana mpango wa kukata rufaa kwa maamuzi ya mwamuzi Lee Mason. “Yalikuwa maamuzi sahihi,” alisema. “ Bila shaka niliomba radhi.” Wayne Rooney alimchezea rafu mbaya Steward Downing na hatimay kupewa kadi nyekundu. Man United walishikilia ushindi wao wa 2-1 pamoja na kucheza watu 10 kwenye dakika 30 za mwisho. Adhabu ya mechi tatu za Rooney zitamfanya akose ‘Manchester derby’ dhidi ya Manchester City Novemba 2. Naye kocha wa West Ham Sam Allardyce alielezea ukabaji wa Rooney kama “ukichaa na usio na lazima” wakati kocha wa Man U Louis van Gaal alikubali kuwa mshambuliaji alipaswa kutolewa. Louis van Gaal anajitahidi kutafuta suluhisho la safu ya ulinzi. “Nilimuona mchezaj

MAZEMBE YATOLEWA KWA MABAO YA UGENINI, FAINALI NI AS VITA NA SETIF LIGI YA MABINGWA

NDOTO za TP Mazembe kwenda Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika, hii leo zimeota mbawa baada ya kutolewa na ES Setif ya Algeria kwa mabao ya ugenini kufuatia sare ya jumla ya 4-4. Setif walishinda 2-1 Algeria wiki iliyopita na leo, Mazembe wameshinda 3-2 mjini Lubumbashi- maaba yake timu ya Algeria inakwenda kuumana na AS Vita ra DRC pia mwezi ujao. Mabao ya Mazembe leo yamefungwa na Mghana, Daniel Adjei Nii dakika ya 21, Salif Coulibaly wa Mali dakika ya 38 na Jonathan Bolingi dakika ya 53, wakati ya Setif yamefungwa na Abdelmalek Ziaya dakika ya tisa Sofiane Younes dakika ya 75. Poleni vijana, haikuwa bahati yenu; Watanzania wanaochezea TP Mazembe, Mbwana Samatta kushoto na Thomas Ulimwengu kulia

KAVUMBANGU ADHIHIRISHA KWELI MKALI WA MABAO, AFUNGA SABA MECHI NANE AZAM FC

Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM MSHAMBULIAJI Didier Kavumbangu amedhihirisha kweli ni mkali wa mabao, baada ya kuifungia klabu yake mpya Azam FC mabao saba ndani ya mechi nane. Kati ya mabao hayo, mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Burundi, manne amefunga katika mechi mbili tu za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, kuashiria kwamba yuko tayari kutwaa kiatu cha dhahabu msimu huu. “Nimefurahi kufanya vizuri katika mechi hizi mbili, na nitaongeza bidii nifanye vizuri zaidi, kwa sababu hiki ndicho kimenileta hapa, kufanya kazi. Nitafanya kazi. Mimi kufunga ndiyo starehe yangu ya kwanza. Ninaposhangilia bao, huwa nasikia raha sana,”alisema Kavumbangu juzi. Didier Kavumbangu kushoto amedhihirisha kweli ni mkali wa mabao baada ya kuifungia Azam FC mabao saba katika mechi nane Kavumbangu juzi alifunga mabao yote mawili Azam FC ikishinda 2-0 dhidi ya Ruvu Shooting ya Pwani katika Ligi Kuu Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam wakati kabla ya hapo, katika mchez

Viongozi wa Chadema wazidi kuhamia CCM

  Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiutangazia umati wa watu waliofurika kwenye uwanja wa mikutano Sunga kurejea rasmi kwa Charles Kagonji (mwenye shati la kitenge) kwenye Chama Cha Mapinduzi akitokea Chadema,wengine katika picha hii ni Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana, na mwenyekiti wa CCM wilaya ya Lushoto Balozi Abdi Hassan Mshangama. Mzee Charles Kagonji akiwasalimia wananchi na kutamka rasmi kurejea CCM yeye pamoja na wafuasi wake aliokuwa nao Chadema. Katika mkutano huu wengine waliorudi CCM kutoka Chadema ni aliyekuwa Mwenyekiti wa Jimbo Ismail Semkunde, aliyekuwa Katibu wa Jimbo Mzee Julius Kavurai na aliyekuwa mgombea wa udiwani kwa tiketi ya Chadema Ndugu Ally Gaha. Wananchi wakinyoosha mikono juu kama ishara ya kumkaribisha CCM Mzee Charles Kagonji. Mzee Charles Kagonji akishukuru kurudi nyumbani CCM. Mzee Julius Kavurai aliyekuwa Katibu wa Jimbo la Mlalo Chadema akiwapungia mkono wananchi kwenye mkuta

Liverpool yatoka sare na Everton

Timu ya Liverpool imeendelea na kupata matokeo yasiyo mazuri katika ligi ya uingereza baada ya wiki iliyopita kupata kipigo cha mabao 3-1 dhidi ya West Ham United na leo imeweza kulazimishwa sare katika uwanja wake wa nyumbani Anfield na Everton. Bao la nahodha Steven Gerrad dakika ya 65 lilionekana kuwapa alama zote Liverpool katika mchezo wa leo .Mchezo uliendelea kwa kasi sana na mnamo dakika za majeruhi Jagielka wa Everton kutoka umbali wa yadi 30 aliachia bunduki kali sana na kuokoa timu yake na kufanya mchezo kuishia 1-1.

Maandamano ya kumpinga kabila yafanyika

Joseph Kabila Maelfu ya watu wameandamana nchini Jamhuri ya kidemorasi ya Congo wakimpinga rais wa taifa hilo Joseph Kabila. Wafuasi wa upinzani wanataka rais Kabila kuondoka madarakani wakati muhula wake wa pili wa uongozi utakapomilika mnamo mwaka 2016. Kuna shaka kuwa huenda katiba ikabatilishwa ili kumruhusu kuwania muhula wa tatu. Maandamano kwenye mji mkuu Kinshasa yaliripotiwa kuwa ya amani lakini polisi walitumia vitoa machozi kuwatawanya waandamanaji kwenye mji wa Goma ulio mashariki mwa nchi hiyo. Rais Joseph Kabila alichukua mamlaka mwaka 2001 kufuatia kuuawa kwa babake Laurent Kabila. BBC

Kumbe inshu ya Cole,Kumpigania Mwanaume Ilikuwa Kiki Tu,Cover Na Nyimbo za album mpya

Siku chache baada ya kukamatwa na polisi kwa kumpiga mwanamke aliyekuwa na mpenzi wake ambaye ni Birdman, Keyshia Cole ametangaza nyimbo na cover la album yake mpya ya  “Point Of No Return” . Wasanii walioshirikishwa kwenye album hii ni pamoja na 2 Chainz,Future, Wale, August Alsina na Juicy J.   1. “Intro (Last Tango)” 2. “Heat of Passion” 3. “N. L. U” (feat. 2 Chainz) 4. “Next Time” (Won’t Give My Heart Away) 5. “Rick James” (feat. Juicy J) 6. “Do That For (B.A.B.)” 7. “New Nu” 8. “She” 9. “Believer” 10. “On Demand” (feat. Wale & August Alsina) 11. “Love Letter” (feat. Future) 12 “Party Ain’t a Party” (feat. Gavyn Rhone) 13. “Remember (Part 2)”

BENKI YA EXIM KUIDHAMINI STAND UTD

Timu ya Stand Utd imepata udhamini wa Benki ya Exim wenye thamani ya shilingi milioni 10 za Kitanzania. Sehemu ya makubaliano ya udhamini huo ni ‘ku-brand’ basi la timu hiyo  kama picha zinavyoonyesha hapo juu. Source :www.mjengwablog.com

Lifetime Reveals Haunting 'Aaliyah' Teaser Trailer

Courtesy of Lifetime Alexandra Shipp plays Aaliyah After a bumpy road , Lifetime is finally revealing the first glimpse at its upcoming Aaliyah biopic.  The film, Aaliyah: The Princess of R&B , stars Alexandra Shipp as the eponymous singing star. Zendaya Coleman had been attached to the role but dropped out just before production began amid reports that Aaliyah's family did not approve of the project.  The trailer highlights Aaliyah's signature fashion sense and dance moves. At the end of the trailer, the images turn black-and-white, providing a haunting reminder of Aaliyah's untimely death.  Aaliyah, known for her hits "Try Again" and "Rock the Boat," was killed in a plane crash in 2001 at the age of 21. She also appeared in several films, including Queen of the Damned .Source www.hollywoodreporter.com

Kenya wafunga madrasa ya Machakos

Polisi wanasema baadhi ya washukiwa wa ugaidi walisoma kwenye madrasa ya Machakos. Uongozi wa Kenya unasema umefunga madrasa iliyo karibu na mji mkuu kwa kufundisha fikra kali za mapinduzi ya Kiislamu. Shule hiyo ya dini iliyopo Machakos, karibu kilometa 65 mashariki mwa Nairobi, ilikuwa imelengwa baada ya baadhi ya vijana wa eneo hilo kuwekwa kizuizini kwa kushukiwa wanajiunga na wanamgambo wa Somalia. Mkuu wa Idara ya Upelelezi ya Polisi (CID) ameonya kwamba madrasa hiyo itafungwa. Kundi la al-Shabab la nchini Somalia limeshafanya mashambulizi kadhaa nchini Kenya. Washirika hao wa al-Qaida wanasema wanalipiza kisasi kwa kuwepo na vikosi vya wanajeshi wa Kenya na nchini Somalia na mauaji ya Waislamu. Mwaka uliopita, watu 67 waliuawa wakati wapiganaji wa kundi hilo walipoteza na kituo cha duka kubwa la Westgate jijini Nairobi. Mwandishi wa BBC Abdullahi Abi aliyeko Nairobi anasema ni madrasa ya kwanza Kenya kufungwa na polisi kutokana na

Gari ya kwanza ya Mario Baloteli baada ya kuhamia Liverpool inathamani ya Mil 650 kwa pesa ya Bongo

  Wanasema tumia pesa ikuzoee na hiki ndo alichokifanya mchezaji mpya wa Liverpool Mario Baloteli wakati akiwasili katika uwanja unaotumiwa kwa mazoezi na Timu ya Liverpool. Baloteli aliingia uwanjani hapo akiwa na gari aina Ferrari F12 Berlinetta ambayo inauzwa Pound 240,000 ambazo ni sawa na milioni 652 zakibongo. Baloteli pia anamiliki gari nyingine aina ya Bentley GT ambayo inauzwa zaidi ya milioni 450 za kibongo. Baloteli ameamia Liverpool akitokea timu ya Ac Milan ambako alikua akichezea.

Hawa Hapa wasanii wa Hip Hop walioingiza mkwanja mrefu zaidi kwa mwaka huu

  Hii ni list mpya ya wasanii wa Hip Hop waliotengeneza pesa nyingi tangu June mwaka jana hadi June 2014. Na hii ndo list ya wasanii 20 huku Dr Dre akiwa namba moja. 1. Dr. Dre - $620 million 2.  Jay Z (tie) - $60 million 2. Diddy (tie) - $60 million  4. Drake - $33million 5. Macklemore & Ryan Lewis - $32 million 6. Kanye West: $30 million 7. Birdman: $24 million 8. Lil Wayne: $23 million 9. Pharrell Williams: $22 million 10. Eminem: $18 million 11. Nicki Minaj: $14 million 12. Wiz Khalifa: $13 million 13. Pitbull: $12 million 14. Snoop Dogg: $10 million 15. Kendrick Lamar: $9 million 16. Ludacris: $8 million (tie) 16. Tech N9ne: $8 million (tie) 16. Swizz Beatz: $8 million (tie) 16. 50 Cent: $8 million (tie) 20. Rick Ross: $7 million (tie) 20. J. Cole: $7 million (tie) 20. DJ Khaled: $7 million (tie) 20. Lil Jon: $7 million (tie) 20. Mac Miller: $7 million (tie) Forbes ndio waliotoa list hii ya  wasanii wa Hip Hop walioingiza mkw

IVO MAPUNDA AVUNJIKA KIDOLE, KUIKOSA YANGA OKTOBA 12

Zikiwa zimebakia wiki mbili kabla ya kukutana na mahasimu wao wa jadi, Simba imepata pigo kubwa katika timu kwa sababu kipa namba moja wa timu hiyo Ivo Mapunda amevunjika kidole mazoezini Zanzibar jana asubuhi na anatakiwa kuwa nje ya uwanja kwa wiki nane. Hatoweza kusimama golini wakati tiu yake ikicheza na Yanga October 12 2014 ambapo daktari wa Simba SC Yassin Gembe amesema Ivo aliumia wakati anachupia mpira katika mazoezi ya asubuhi na kwa bahati mbaya mpira ukamgonga kwenye kidole kidogo cha mwisho mkono wa kulia. Gembe amesema Ivo alitoka mazoezini baada ya tukio hilo na baadaye akapelekwa hospitali ya Mnazi Mmoja kisiwani humo ambako baada ya vipimo ikagundulika amevunjika sana. “Si kuvunjika kwa mzaha, amevunjika sana na anatakiwa kupumzika kwa wiki nane, baada ya hapo aanze taratibu… ina maana makadirio ya kurudi tena uwanjani ni hadi baada ya miezi mitatu‘ – Gembe. Kuumia kwa Ivo kunatoa nafasi kwa makipa chipukizi Hussein Sharrif ‘Cassilas’ na P

Picha:Wanafunzi wa Chekechea Tunduru Wasomea Chini ya Mti

Wanafunzi wa darasa la awali katika Shule ya Msingi Nakayaya Wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma wakiwa wamekaa chini na mwalimu wao pembeni kuonesha sehemu ambayo hutumika kama darasa wawapo masomoni. ---   Tunduru WANAFUNZI wa darasa la awali katika Shule ya Msingi Nakayaya Wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma wanasomea chini ya mti kutokana na darasa hilo kuendeshwa bila ya kuwa na chumba maalum kwa ajili ya kusomea wanafunzi hao. Hali hiyo imebainika baada ya mwandishi wa habari hizi kuitembelea shule hiyo hivi karibuni na kuwakuta wanafunzi wakiwa wamekaa chini huku wakiendelea na masomo hayo nje chini ya mti ulio na kivuli cha kuwahifadhi wakati wa jua kali. Akizungumza shuleni hapo Kaimu Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Nakayaya, Christina Mhowera alisema watoto hao wamelazimika kusomea nje baada ya huduma ya elimu hiyo kuanzishwa shuleni hapo bila ya kuwa na jengo maalum kwa wanafunzi wa awali. Alisema awali wanafunzi hao walikuwa wakisome

TBL YATOA MSAADA WA VISIMA VYA MAJI ZANZIBAR NA MBAGALA

Mwakilishi wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Zanzibar Samir Manji ( wa tatu kushoto),  akikabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya sh. mil 51 wananchi wa majimbo ya Chumbuni na Mpendae ikiwa ni msaada wa kampuni hiyo kwa ajili ya mradi wa uchimbaji wa visima vya maji safi na salama katika majimbo hayo juzi. Wa pili kushoto ni Ofisa Uhusiano wa TBL, Dorris Malulu  Mwakilishi wa Mauzo ya Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Kanda ya Temeke, Bw. Alen Mwebuga (kushoto), akimkabidhi Mganga Mkuu wa Kituo cha Afya cha Mbagala Round Table Maternity Home, Dkt. Baturi Luhanda, mfano wa Hundi ya sh. Milioni 20, kwa ajili ya kusaidia kuchimba kisima cha maji. Wengine katika picha ni Afisa Uhusiano wa TBL, Bi. Doris Malulu (wa pili kulia), Mhandisi wa mradi huo, Bw. Onesmo Zakaria na Rais wa Rotary Klab Agnes Batenga. (Na Mpigapicha Wetu)

Tambwe:Okwi atanipa ufungaji bora.

Amissi Tambwe mshambuliaji wa Simba SC amejipanga vyema kuhakikisha anaendelea na moto wake wa ufungaji wa mabao mengi katika ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara msimu huu. Tambwe aliibuka mfungaji bora wa kombe la Kagame mwaka jana na vilevile mfungaji bora katika ligi kuu Tanzania bara kwa kufunga mabao 19 katika michezo 23 aliyocheza katika timu yake ya Simba . Akifanya mazungumzo na vyombo vya habari jana,Tambwe anaamini usajili uliofanywa na Simba kwa kuweza kumrudisha Okwi katika timu yao ni mzuri sana kwa timu na hasa kwake yeye kwani atacheza sambamba na yeye  na kuweza kumtengenezea nafasi nyingi za kufunga mabao mengi msimu huu. Chanzo : kandanda.galacha.com

Boko Haram waamua kujisalimisha

Jeshi la Nigeria limesema kwamba zaidi ya wanamgambo 260 wa Boko Haram wamejisalimisha kaskazini-mashariki mwa Nigeria. Msemaji alisema jeshi hilo lilimuua mtu anayechukuliwa kama kiongozi wa kundi, Abubakar Shekau. Inasemekama Mohammed Bashir ametokea kwenye video ya kundi hilo ila anaonekana kama mtu mwenye sura ya uongo. Book Haram wameingia hasara kubwa ndani ya wiki za karibuni baada ya jeshi la Nigeria kupambana na kundi hilo karibu na mji wao wa Maiduguri kaskazini-mashariki. Jeshi lilisema kwamba wanachama 135 wa Boko Haram wamejisalimisha pamoja na silaha zao mjini Biu, kwenye jimbo la Borno – na kwamba wengine 135 wamejisalimisha maeneo mengine ya kaskazini-mashariki mwa Nigeria na wanahojiwa kwa sasa. Mwandishi wa BBC Will Ross aliyekuwepo mjini Lagos anasema kwamba hii haijawahi kutokea katika vita dhidi ya Boko Haram.

Bunge lazika suala la uraia pacha

Rasimu ya Katiba inayopendekezwa katika Bunge Maalum la Katiba imezika rasmi suala la uraia pacha. Rasimu ya Katiba inayopendekezwa imezika rasmi suala la uraia pacha. Kwa muda mrefu sasa kumekuwa na mjadala kuhusu uraia pacha, huku Watanzania wanaoishi nje wakishinikiza kiwepo kipengele kwenye Katiba kinachoruhusu suala hilo. Akiwasilisha rasimu hiyo jana, Mwenyekiti wa Kamati ya Uandishi wa Katiba, Andrew Chenge, alisema hakutakuwa na uraia pacha isipokuwa watu wenye asili ya Tanzania ambao hawana uraia watapewa hadhi maalumu. “Kamati ya Uandishi ilifanya utafiti katika Katiba za nchi nyingine kama za India na Ethiopia na imebaini wao huwapa watu wenye asili ya nchi zao hadhi maalumu na kuwawezesha kupata haki mbalimbali,” alisema Chenge. Hivyo alisema watu wenye asili ya Tanzania ambao waliacha kuwa raia wa Tanzania na kupata uraia wa nchi nyingine watatambuliwa na kupewa hadhi maalumu. Kwa mujibu wa Chenge, haki hizo ni pamoja na kutoh

Soma kuhusu Liverpool Kuchunguzwa chunguzwa na FFP

FFP inaichunguza Liverpool kwa kuvunja sheria ya matumizi ya fedha. Liverpool ni moja ya vilabu vinavyofanyiwa uchunguzi kwa kuvunja sheria za matumizi sahihi ya fedha michezoni (Financial Fair Play (FFP). Kwa mujibu wa sheria za Uefa, vilabu vyote vinavyoshindana barani Ulaya lazima vifikie kutumia pauni milioni 35.4 ndani ya misimu miwili. Kuna adhabu kwa wale ambao hawafikii huko, ikiwemo Manchester City iliyopigwa faini na kuwekewa kiwango cha kutumia fedha na kiasi cha timu mwezi Mei baada ya kuvunja sheria. Liverpool wanaamini kuwa watafutiwa mashtaka yao baada kupeleka taarifa zao za matumizi ya fedha. Ila pamoja na kupoteza pauni milioni 49.8 kwa msimu wa 2012-13 na pauni milioni 41 kwa msimu wa 2011-12, Liverpool wanaamini kuwa watafutiwa mashtaka. The Reds, pamoja na Monaco, Inter Milan na Roma – hakuna kati yao katika mashindano barani Ulaya msimu uliopita – wamepeleka akaunti zao kwenye bodi inayosimamia matumizi ya

Ebola bado tishio Nigeria

Shule zililazimika kufungwa kutokana na tishio la ebola Jitihada zimeendelea kufanywa katika nchi kadhaa za Afrika magharibi na jumuia ya kimataifa kupambana na ugonjwa wa ebola ambao umeathiri nchi za Sierra Leone,Liberia , Guinea hali kadhalika Nigeria kwa kiasi kikubwa huku Serikali za nchi hizo zikifanya jitihada za kujinusuru na ugonjwa huo. Baadhi ya shule Nchini Nigeria zimefunguliwa baada ya kuchelewa kwa zaidi ya wiki mbili kwa lengo la kujaribu kuzuia maambukizi ya ugonjwa ebola lakini shule zilizopo mjini lagos ambapo ndio kitovu cha ugonjwa huo zitaendelea kufungwa mpaka mwezi ujao . Shirikisho la walimu nchini humo linaitaka serikali kuchukua hatua ili kuzuia tishio la maambukizi ya ugonjwa wa ebola kwa wanafunzi, na kusema kuwa wamesitisha mgomo Wakati huo huo, Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema kuwa maambukizi ya virusi vya ebola

Ujauzito wa Witness umeharibika ulikuwa wa Watoto Mapacha

Akiongea na Times Fm, Witness ameeleza kuwa alikuwa anatarajia mapacha na alikuwa katika hatua za mwisho lakini ghafla ikatokea hali hiyo ambayo hadi sasa inafanyiwa uchunguzi na madaktari kubaini chanzo. “Kuna mambo ambayo niliambiwa kwamba endapo ningekuwa sina mazoezi au ningekuwa siko strong ina maanisha kwamba na mimi mwenyewe ningekuwa hatarini.” Amesema Witness. Ameeleza kuwa hali hiyo ilitokea Ijumaa iliyopita lakini yeye na mchumba wake Ochu waliamua kukaa kimya kwa muda hadi leo walipoamua kuiweka wazi. Akiongelea afya yake,Witness ameeleza kuwa hivi sasa anaendelea vizuri.

Maandamano ya Chadema Mara, mabomu yarindima, viongozi wakamatwa

Moja ya maandamano yaliyowahi kufanywa na wafuasi wa Chadema mkoani Mara mwaka 2011. Leo kuanzia saa mbili asubuhi makamanda na wanachama wa CHADEMA na wananchi wasio na vyama vya siasa walikusanyika katika mtaa wa Nyasura iliyopo katika wilaya ya Bunda mkoa wa Mara kwa ajili ya kuanza maandamano ya kupinga Bunge la Katiba kuendelea na vikao vyake. Wananchi waliojitokeza walikuwa karibu 1,200 na ilipofika saa tano kamili maandano yalianza kuelekea stendi ya zamani ambapo ilitalakiwa ufanyike mkutano mkubwa, polisi walikuja na kuanza kurusha mabomu ya machozi na kwa kuwa wananchi walikuwa wamejizatiti, mabomu ya machozi ni kama hayakufua dafu ndipo risasi za moto zilianza kutumika. Mpaka sasa wameshakamatwa viongozi sita wa Chadema. Wananchi bado wanaendelea kujikusanya na kutiana hamasa! Shuhuda mmoja alisema ameona makundi makubwa ya watu sasa yanatoka kwenye nyumba zao na wameanza kujikusanya wakiwa na lengo la kuendelea na maandamano! Habari

MAMA SALMA KIKWETE AFUNGUA MKUTANO WA ELIMU

Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA, Mama Salma Kikwete akipokewa na Dkt. Peter Feiler, Mkuu wa Idara ya Ushirikiano wa Kiuchumi katika Wizara ya Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo ya Ujerumani wakati alipowasili kwenye Ofisi ya Ubalozi wa Ujerumani kwenye Umoja wa Mataifa huko New York alipokwenda kuhudhuria mkutano uliozungumzia masuala ya elimu: kuwawezesha vijana kufanya maamuzi sahihi ya kiafya tarehe 22.9.2014. Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Ushirikiano wa Uchumi na Maendeleo wa Ujerumani Mheshimiwa Gerd Mueller (kulia) na Mke wa Rais wa Malawi Mheshimiwa Getrude Mutharika wakati wa ufunguzi wa mkutano ulioandaliwa na serikali ya Ujerumani kuzungumzia masuala ya elimu ili kuwawezesha vijana barani Afrika kufanya maamuzi sahihi ya kiafya. Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akisa

Tupia Macho kuhusu inshu hii huko majuu

Mashabiki wa Apple Ijumaa hii wamezishika simu zao mpya za iPhone 6 baada ya kungojea kwa siku kadhaa nje ya maduka yanayouza simu. Hata hivyo, zaidi ya iPhones milioni 5 zinaweza kuishia kwenye soko haramu la Kichina ambapo zinaweza kuuzwa kwa bei mara tatu zaidi. Jijini London Ijumaa hii mamia ya watu walikuwa wamejipanga kwenye mistari mirefu huko Covent Garden na Regent Street walionekana wakisherehekea kila baada ya kupata simu zao.  Sam Sheikh, 27, anayeishi London, amedai kuwa amesubiria kwa siku tatu kungoja siku yake na amekuwa mteja wa kwanza wa Uingereza kupata simu  Wakati huo huo huko Marekani kwenye duka la Birmingham kulikuwa na msululu mrefu wa zaidi ya mita 100 ambapo simu zote ziliisha ndani ya dakika 10 tu. Simu hizo zinauzwa kwa kuanzia £539 kwa zile zenye GB16, £619 kwa zile zenye GB 64 na £699 kwa simu zenye GB 128. iPhone 6 Plus zinauzwa kwa kuanzia £619 kwa ile yenye 16GB, £699 kwa yenye 64GB na £789 yenye 12