Mbowe ameshinda nafasi hiyo katika uchaguzi mkuu wa chama hicho uliofanyika katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Nafasi ya Makamu Mwenyekiti Bara imechukuliwa na Prof. Abdallah
Safari aliyepata kura 775 za ndiyo huku kura za hapana zikiwa 34 baada
ya kuwa mgombea asiye na mpinzani.
Makamu Mwenyekiti Zanzibar ni Said Issa Mohamed aliyepata jumla ya
kura 645 huku mpinzani wake Hamad Mussa Yusuph akiambulia kura 163.
Comments