Kocha wa Manchester United Louis van Gaal angependa kumsajili Cristiano Ronaldo ila hatarajii Real Madrid kumuuza.
Nyota huyo, 29, amekuwa akihusishwa na kurudi Old Trafford, aliondoka
mwaka 2009 kwa uhamishi wa rekodi ya dunia wa ada pauni milioni 80.
Alipoulizwa kuhusu kumsaini mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Ureno, Van Gaal alisema; “Inawezekana.
“Wachezaji kama Ronaldo huzipa timu zao vitu vingi vya ziada, ila sidhani Real Madrid watamuuza.”
Ronaldo, mchezaji bora wa dunia wa mwaka, aliisadia Real Madrid kuwa mabingwa wa Ulaya kwa mara ya 10 mwezi Mei.
Comments