Skip to main content

Posts

Showing posts from February, 2019

Balozi Seif Ali Iddi kufungua Mashindano ya Michezo ya Majeshi Jumamosi

Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Ufunguzi wa Mashindano  ya Michezo ya Majeshi yatakayoanza kuanzia Februari 23 hadi Machi 8 mwaka huu katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam. Hayo yamesemwa jana jijini humo na Menyekiti wa Baraza la Michezo ya Majeshi Tanzania (BAMMATA) Brigedia Jenerali, Suleiman Mzee ambapo amesema michezo hiyo itashirikisha vikosi kutoka kanda saba za majeshi likiwemo Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Jeshi la Uhamiaji, Jeshi la Polisi nchini, Magereza, Jeshi la Kujenga Taifa(JKT) na Zimamoto na Uokoaji. “ Mashindano hufanyika kila mwaka tumewaalika wageni wa heshima tunatarajia Balozi Seif Ali Idd kutufungulia mashindano Uwanja wa Uhuru,” amesema Brigedia Jenerali Mzee. Amebainisha kuwa mashindano hayo yatashirikisha michezo mbalimbali ikiwemo ya mpira wa pete, mpira wa miguu, mpira mikono wanawake na wanaume, Ndondi, mpira wa wavu, kikapu, kulenga shabaha wanawak

Zantel yakabidhi zawadi za Smartphone ICE2 kwa washindi wa droo ya wiki ya Tumia Eazy Pesa Ushinde

Kampuni ya Mawasiliano ya Simu ya Zantel imewakabidhi zawadi za Simu za Smartphone ICE2 washindi wa Jumatano ya wiki iliyopita wa Droo ya Wiki ya Tumia Eazy Pesa Ushinde. Akikabidhi zawadi hizo kwa washindi wa droo hiyo jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Zantel, Rukia Mtingwa amesema washindi 30 wa wiki wamekabidhiwa zawadi hizo ambapo kati yao watano wamepewa jijini humo huku 25 waliobaki wanatoka Visiwa vya Unguja na Pemba. “ Tulifanya droo ya Tumia Eazypesa Ushinde Jumatano iliyopita washindi 30 wanakabidhiwa zawadi ya Simu ya Smartphone ICE2 watano wanakabidhiwa hapa mmoja wao anaishi Dar waliobaki Unguja na Pemba,” amesema Rukia. Amebainisha kuwa washindi wa droo ya mwezi ya Tumia Eazypesa na Ushinde watakabidhiwa fedha taslimu ambapo mshindi wa kwanza atapata Sh milioni moja, wa pili Sh 500,000, wa tatu Sh 300,00 huku mshindi wa nne hadi wa 10 kila mmoja atakabidhiwa Sh 200,000. Amewataja miongoni mwa washindi hao ni Mohamed Kapoma, Suleiman

Tampro yawajengea Mwembenjozi Kibaha madarasa ya thamani ya shilingi milioni 60

Taasi ya wanataaluma wa kiislamu Tanzania (TAMPRO) imewajengea wanakijiji wa mwembenjozi Kibaha madarasa ya kisasa mawili    yenye thamani ya shilingi milioni 26. Kijiji hicho cha Mwembenjozi kilichokosa shule kwa miaka kadhaa tokea kuanzishwa kwake, ambapo sasa kimeondokana na adha ya wanafunzi wa eneo hilo kwenda umbali mrefu kuisaka elimu. Pichani Mbunge wa Kibaha Vijijini Hamoud Jumaa aliyekuwa mgeni rasmi katika hafla yakukabidhi madarasa hayo akikata utepe. Akizungumza na Majira jana Jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa TAMPRO Mashauri Ngolola amesema wameguswa kuisaidia jamii ya kijiji hicho kutokana na kutokuwa na shule kwa mda mrefu. “TAMRO inaendeshwa kwa misingi ya dini ya kislam hivyo basi sanjari na utoaji huduma za kifedha kwa ajili yakuhudumia jamii, hususani ya kiislamu kifedha, tunachangia maendeleo ya kijamii pasipokujali anayenufaika ni muislamu au laa,”amesema Ngolola amesema kutokana na eneo hilo kutokuwa na shule kwa miaka mingi wanafunzi walik

Halotel yazindua huduma mpya za kupiga simu ya Royal Bando na Tomato Bando

KAMPUNI ya mawasiliano ya simu halotel imekuja na huduma  2  ya Royal bundle na Tomato bundle ambazo zitawawezesha wateja kupata huduma zisizo na kikomo  kwa kupiga simu ndani na kimataifa pamoja na kutumia intanenti bila kikomo. Akizungumza kwenye hafla fupi ya uzinduzi leo jijini Dar es salaam,mkurugenzi mkuu wa  halotel Tanzania Nguyen  Van Trung alisema kuwa huduma hizo zitawapa ubora na  unafuu wateja wao kila kona ya nchi. "Ninayo furaha kubwa kuwatangazia ujio wa huduma hii kabambe itakayoleta mapinduzi  makubwa nchini Royal bundle imekuja kukata kiu ya wateja ambao walikuwa wanatani  kutumia huduma zetu bila kupata bugudha zikiwemo salio kuisha au intaneti kukata," alisema Nguyen pICHANI Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Simu za Mkononi Halotel Bw. Nguyen Van Trung akimmiminia mvinyo Diva mtangazaji wa Clouds kulia ni DJ Makay kutoka East Africa Radio pamoja na wasanii mbalimbali ambao ni mabalozi wa kampuni

Mechi ya watani wa jadi anga na Simba zaingiza Mil. 342

Mchezo namba 270 wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara uliozikutanisha Young Africans na Simba uliochezwa Jumamosi Februari 16,2019 kwenye Uwanja wa Taifa umeingiza jumla ya shilingi Milioni 342,825,000. Mchezo huo uliingiza jumla ya watazamaji 41,266. VIP A waliingia Watazamaji 546 kwa kiingilio cha Shilingi 30,000 na kupatikana jumla ya shilingi 16,380,000,VIP B na C waliingia Watazamaji 3,185 kwa kiingilio cha shilingi 20,000 ikapatikana jumla ya shilingi 63,700,000,Majukwaa ya rangi ya Machungwa,Bluu na Kijani waliingia Watazamaji 37,535 kwa kiingilio cha shilingi 7,000 imepatikana jumla ya shilingi 262,745,000 Mgawanyo wa mapato VAT 52,295,338.98 Selcom 15,170,006.25 TFF 13,767,982.74 Uwanja 41,303,948.22 Young Africans 165,215,792.86 Gharama za mchezo 19,275,175.83 TPLB 24,782,368.93 BMT 2,753,596.55 DRFA 8,260,789.64

Waziri wa KilimoJaphet Hasunga ipo sababu yakuanzishwa haraka sheria ya kilimo

WAZIRI wa Kilimo Japhet Hasunga amesema ipo haja ya kuanzishwa kwa sheria ya kilimo itakayotoa suluhisho la changamoto zinzazoikabili sekta hiyo. Hasunga aliyasema hayo hivi karibuni wakati wa kikao cha siku moja baina ya wizara na watafiti wa kilimo kutoka Taasisi mbalimbali za kilimo nchini. “Kuna kila sababu yakuanzishwa haraka sheria ya kilimo,kwasababu inayotumika sasa ni sera iliyotungwa 2013 ambayo pia inahitaji kupitiwa upya,” alisema Hasunga aliongeza kuwa sheria zinazotumika kwa sasa ni za bodi za mazao mbalimbali, ambazo pia zinachangamoto zake na kuna mazao ambayo hayana bodi kiasi kwamba kuwatetea wakulima wa mazao hayo inakua ngumu. Mazao yaliyo katika utaratibu wa bodi ni pamoja na zao la pamba, Kahawa, Chai, korosho, pareto na tumbaku kwa upande wa mazao ya Biashara, mazao ambayo hayana bodi ni yale ya chakula ambayo nayo yana mchango mkubwa katika uchumi wa Taifa. Hasunga aliwataka watafiti hao kutumia kikao hicho kwakutoa maelezo yenye tija, nin

Tamasha la Filamu la Kimataifa la SZIFF litafanyika Februari 23 mwaka kwenye Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam

Jumla ya Tuzo  30 za Filamu zinatarajiwa kutolewa katika Tamasha la Filamu la Kimataifa la SZIFF  litatalofanyika kwenye Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam Februari 23 mwaka huu. filamu zilizotajwa kuingia katika duru ya pili kwa upande wa filamu ndefu za kiswahili ambazo  zilikuwa 141 zilizoingia duru ya pili ni 28, filamu fupi ni 73 zilizoingia 11, tamthili  20 zilizopita ni 7, makala zilizopita 3 huku kila kipengele kikitofautiana idadi ya  Filamu kutokana na ushindani uliokuwepo ambapo vigezo na masharti yakizingatiwa. Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam wakati akitangazafilamu zilizopita  katika mchujo wa kwanza Mratibu wa Tamasha hilo Sophia amezitaja filamu zilizoingia   katika duru ya pili kwa upande wa filamu ndefu za kiswahiliambazo zilikuwa 141 zilizoingia  duru ya pili ni 28, filamu fupi ni 73 zilizoingia 11, tamthili 20 zilizopita  ni 7, makala zilizopita 3 huku kila kipengele kikitofautiana idadi ya Filamu  kutokana na ushindani ulio

Tamasha la Pasaka Limetangaza kufanyika mara kwa mara na kwa wakazi wa Sumbawanga,mkoani Rukwa.

Kampuni ya Msama Promotions,inayoratibu tamasha la Pasaka nchini imetangaza kulipekeka tamasha hilo kwa mara ya kwanza kwa wakazi wa Sumbawanga,mkoani Rukwa.  Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam , Msama amesema wakazi wa Sumbawanga wamekuwa wakihitaji huduma ya tamasha hilo kwa muda mrefu, hivyo ameahidi kuikata kiu ya wakazi wa mji huo kwa namna ya kipekee kabisa. “Sumbawanga wamekuwa wakilalamika muda mrefu kuhusu kutokupelekewa Tamasha hilo, Mwaka huu kwa Mara ya kwanza tutapeleka Tamasha kwa wakazi wa Sumbawanga, wakae tayari kupokea ujio wa Tamasha lililobeba utofauti” amesema Msama.  Amesema katika Tamasha la mwaka huu kutakuwa na utofauti mkubwa, ambapo ameeleza kuwa wapo waimbaji wapya ambao hawajawahi kuja nchini, na kuongeza kuwa kwa Mwaka huu waimbaji wote watakaopata nafasi watalazimika kuimba kwa kutumia Band (LIVE) na si CD (PlayBack) kama ilivyozoeleka.  “Tumeongeza Waimbaji wapya ambao hawajawahi kuja nchini, waimbaji ambao h

Mwanza na mikoa mingine 6 wapewa tahadhari ya mvua kubwa na mafuriko

Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA) imetoa tahadhari ya kuwapo kwa mvua kubwa (juu ya wastani) kwa baadhi ya mikoa ya Kanda ya Ziwa, Dar es Salaam na Kilimanjaro. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana Februari 14, 2019 kuhusu utabiri wa mvua za masika kwa mikoa inayopata mvua mara mbili kwa mwaka, Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dk. Agnes Kijazi, amesema kuwa, kutokana na mifumo ya hali ya hewa ilivyo kwa sasa na inavyotarajiwa kuwa kwa kipindi chote kuanzia Machi mpaka Mei mwaka huu, maeneo mengi yanayopata mvua mara mbili kwa mwaka yanatarajia kuwa na mvua za wastani. Hata hivyo, Dk. Kijazi amesema baadhi ya maeneo katika mikoa ya Dar es Salaam, Zanzibar, Arusha, Kilimanjaro, Kagera, Mara, Mwanza, Geita, Simiyu na Shinyanga kuna uwezekano mkubwa wa kupata mvua kubwa (juu ya wastani). “ Kwa mikoa ya Kanda ya Ziwa, tunategemea mvua hizi zitaanza wiki ya mwisho ya mwezi huu, ikianzia mikoa ya Kagera na baadaye kusambaa kwenye mikoa mingine ya ukanda huo, ” amesema Kijazi

Africa: Launch of the first ever Africa Protected Areas Congress

PRESS RELEASE Launch of the first ever Africa Protected Areas Congress The launch steered awareness and visibility of the upcoming conference to be held on 18th to 23rd November this year NAIROBI, Kenya, February 14, 2019/ -- This year’s Valentine day was marked on Thursday with special African flavour that saw the launch of the first-ever Africa Protected Areas Congress (APAC) ( www.APA-Congress.org ) at Nairobi National Park’s historic Ivory Burning Site. Kenya’s Principal Secretary - State Department of Tourism and Wildlife, Dr. Margaret Mwakima accompanied by Dr.John Waithaka the Congress Director and Mr. Luther Anukur Regional Director, International Union for Conservation of Nature (IUCN), East and Southern Africa presided over the launch. Dubbed for the love of nature, the APAC 2019 launch sought to position Africa’s protected areas within the goals of economic and community well being as well as seek commitment from African governments

Kampuni ya Botch kutoka Ujerumani kujakuwekeza nchini

KAMPUNI ya Uwekezaji kutoka Ujerumani Botch  kutoka Ujerumani inatazamiwa kuinua  pato la Taifa inchini na hivyo taasisi mbalimbali hapa nchini zimetakiwa kuchangamkia fursa kupata manufaa. Kuja kwa uwekezaji kumetajwa utawezesha kujengwa kwa karakana ya kurepea magari hivyo kutoa fursa na kipaombele kwa vijana wa kitanzani waliosomea fani mbalimbali ikiwemo vyuo vya ufundi stadi VETA kupata ajira na utaalamu wa kiwango cha juu zaidi. Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji Angela Kairuki amezitaka taasisi  hapa nchini kutumia fursa ya ujio wa kampuni  hiyo ya Botch. Hayo yalisemwa na Waziri huyo mwenye dhamana juzi jijini Dar es Salaam katika kikao cha pamoja na wawekezaji alisema kuwa  wawekezaji hao wako tayari kuwekeza kwenye maeneo mengi ikiwemo vifaa  vya majumbani, Friji na hita pamoja na vifaa vya magari, ujenzi na mashine za mawasiliano na usalama vitakavyouzwa soko landani na nje ya nchini. Alisema kuwa ujio huo tayari imewekeza katika nchi nyingi Afrika na endapo wa

Uongozi soko la Mabibo umesema unajitaidi kuboresha mazingira ikilinganishwa na hapo awali

UONGOZI wa soko la Mabibo maarufu mahakama ya ndizi umesema kuwa kwa sasa unajitaidi kuboresha mazingira ikilinganishwa na hapo awali kabla ya utawala mpya wa soko. Akizungumza Jijini Dar es Salaam leo Meneja Masoko wa soko hilo James Msulwa alisema kuwa limejiimarisha katika suala la usafi na usalama wa raia ikilinganishwa na kipindi cha nyuma. Amesema Soko hilo lipo chini ya uendeshaji wa serikali kwa sasa ambapo makusanyo ya maduhuri ya ushuri hukusanywa moja kwa moja na serikali nakuwasilishwa manispaa ya Kinondoni ushuru ni sh 500 hutozwa kila siku. “Si vyema kujadili yaliyopita hususani uongozi uliopita isipokuwa ninachoweza kusema nidhamu ya ukusanyaji mapato kumechangia soko kuwa katika hali ya usafi na ubora,ukilinganisha na hapo awali,” amesema Msulwa. Msulwa amesema soko la mabibo linajumla ya masoko 8 yaliyo gawanyika kwa mujibu wa vitengo vya mazao ya kilimo yanayouzwa sokoni hapo. Fatuma Shabani ambaye ni mfanyabiashara wa nyanya soko namba moja(ge