Taasi ya wanataaluma wa kiislamu Tanzania (TAMPRO)
imewajengea wanakijiji wa mwembenjozi Kibaha madarasa ya kisasa mawili yenye thamani ya shilingi milioni 26.
Kijiji hicho cha Mwembenjozi kilichokosa shule
kwa miaka kadhaa tokea kuanzishwa kwake, ambapo sasa kimeondokana na adha ya
wanafunzi wa eneo hilo kwenda umbali mrefu kuisaka elimu.
Pichani Mbunge wa Kibaha Vijijini Hamoud Jumaa aliyekuwa mgeni rasmi katika hafla yakukabidhi madarasa hayo akikata utepe.
Akizungumza na Majira jana Jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa TAMPRO Mashauri Ngolola amesema wameguswa kuisaidia jamii ya kijiji hicho kutokana na kutokuwa na shule kwa mda mrefu.
Akizungumza na Majira jana Jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa TAMPRO Mashauri Ngolola amesema wameguswa kuisaidia jamii ya kijiji hicho kutokana na kutokuwa na shule kwa mda mrefu.
“TAMRO
inaendeshwa kwa misingi ya dini ya kislam hivyo basi sanjari na utoaji huduma
za kifedha kwa ajili yakuhudumia jamii, hususani ya kiislamu kifedha,
tunachangia maendeleo ya kijamii pasipokujali anayenufaika ni muislamu au laa,”amesema
Ngolola
amesema kutokana na eneo hilo kutokuwa na shule kwa miaka mingi wanafunzi
walikuwa wakienda makao makuu ya kata ya Dutumi kuitafuta elimu, waliona ni
vyema kuwaunga mkono katika jitihada za ujenzi wa shule hiyo.
Kwa
upande wake Mbunge wa Kibaha Vijijini Hamoud Jumaa aliyekuwa mgeni rasmi katika
hafla yakukabidhi jengo hilo aliishukuru TAMPRO kwakuchangia katika maendeleo
ya elimu hususani katika jamii ya wahitaji nakuzitaka Taasisi, Makampuni na
wafadhiri kuchangia katika maendeleo ya shule hiyo.
“Kipekee
sana niishukuru nakuipongeza TAMPRO kwa jitihada zake zakupambana na umaskini
nakuwaletea watu maendeleo lakini leo hii niwashukuru kwakuchangia ujenzi wa
madarasa kwa ajili ya watoto wetu, wengine waige mfano wa TAMRO,” amesema
Mwajuma Said
mkazi wa Mwembenjozi ameushukuru uongozi wa TAMRO kwakuwajengea majengo mawili
ya madarasa ya kisasa nakusema kuwa kuwepo kwa shule kijijini hapo jamii hiyo
itaelimika zaidi.
“Elimu
ndiyo kila kitu watatoto wetu wakipata elimu kijiji hiki kitaendelea na kuwa na
maendeleo makubwa kama vijiji ambavyo vinashule ambavyo maendeleo yake yamekuwa
makubwa na maradufu,” amesema.
TAMRO ni
Taasi ya wanataaluma wakiislamu inayojihusisha na masuala ya utoaji wa mikopo
kwa jamii ya waislama yenye makao yake makuu Magomeni Dar es Salaam kupitia
taasisi hiyo maisha ya wengi yameimarika kiuchumi.
Comments