Skip to main content

Posts

Showing posts from January, 2016

Mzee Yusufu azindua 'Kaning’ang’ania' Dar Live Usiku wa jana

  Mwimbaji mahiri wa kundi  la Jahazi Modern Taarab  Mzee Yusufu  usiku wa jana alizindua albamu mpya ya kundi hilo iitwayo Kaning’ang’ania   katika ukumbi wa Dar Live Mbagala jijini hapa. Baadhi ya nyimbo nyingine zilizo pagawisha mashabaki  katika uzinduzi huo ni 'Limekuuma' ya Fatma Ally, 'Nia Safi Hairogwi' ya Mish Mohyamed, 'Nina Moyo Sina Jiwe' ya Leila Rashid pamoja na Mashallah ya Mzee Yusuf akiwa na Vanessa Mdee   Malkia wa mipasho Bi Khadija Kopa nae atakuwa na lake jipya liitwalo  Ogopa Kopa ni mmoja wa wasindikizaji wa onyesho hilo waliofanya balaa kwa kuibua shangwe  

Business Travel laitunuku ETIHAD Tuzo ya Shirika la Ndege la mwaka

Be the first to comment! Meneja wa Chakula na Vinywaji wa Shirika la Ndege la Etihad. Etihad Business Studio. Shirika la ndege la Etihad limetajwa kuwa Shirika la Ndege la Mwaka wakati wa tuzo za Business Travel 2016. Hafla hii ilifanyika jana usiku katika hoteli ya Grosvenor House iliyopo Jijini London. Tuzo hizi zinatambua makampuni na watu binafsi waliopata mafanikio katika sekta ya biashara ya usafiri na hivyo kuwafanya wastahili kuwania tuzo hizo. Tuzo hizi zinazoandaliwa na jarida la Uingereza la Buying Business Travel, huwa na jopo la wataalamu wanaojadiliana na kisha kupiga kura kubaini washindi. Hii ni mara ya kwanza kwa Etihad kushinda tuzo hiyo, hii ikija siku chache tu baada ya shirika la ndege la Etihad kupokea “Tuzo ya Uvumbuzi katika Usafiri” kutoka tuzo za jarida la Globe Travel katika hafla nyingine iliyofany

Kiungo wa Chelsea Ramires atimkia China

Ramires amekamilisha uhamisho wake kwenda klabu ya Jisungsu Suning ya China kwa ada ya pauni milioni 25 Kiungo wa Chelsea Ramires amejiunga na klabu ya China Jiungsu Suning kwa mkataba wa kudumu, klabu ya Ligi Kuu imetangaza. The Blues ililipa pauni milioni 18 kwa Ramires mwaka 2010, alisaini mkataba wa miaka mine mwezi Oktoba. Lakini Mbrazil, 28, hajaanza kikosi cha kwanza Ligi Kuu tangu kipigo cha 2-1 na kutoka kwa Leicester City Desemba 14 na hivyo kutimkia China kwa pauni milioni 25. Ramires aliichezea Chelsea tangu 2010 Historia ya soka ya Ramires Joinville (2006) – 14 mechi 3 magoli Cruzeiro (2007-09) – 85 mechi 16 magoli Benfica (2009-10) – 42 mechi 5 magoli Chelsea (2010-2016) 242 mechi 37 magoli Brazil (2009-) – 52 mechi 4 magoli

Cole akimbilia LA Galaxy

Ashley Cole amesajiliwa na klabu ya LA Galaxy ya nchini Marekani Nyota wa zamani wa Uingereza Ashley Cole amethibitisha kujiunga na LA Galaxy ya Major League Soccer nchini Marekani. Baada ya kushindwa kufanya vizuri na Roma ya Italia, Cole ataungana na akina Robbie Keane na Steven Gerrard kwenye klabu ya Los Angeles. Cole, ambaye alizichezea Arsenal na Chelsea kabla ya kutimkia Rome, alicheza mechi 11 katika miezi 18 klabuni hapo, na hakuwahi kucheza hata dakika moja msimu huu. Cole akikabidhiwa kofia ya dhahabu baada ya kufikisha mechi 100 alizocheza Uingereza mwaka 2013 HISTORIA YA SOKA YA ASHLEY COLE Arsenal  228 games (9 magoli) Crystal Palace (mkopo) 14 (1) Chelsea  339 (7) Roma 16 (0) England 107 (0) Heshima kubwa: Premier League: 2002, 2004, 2010 FA Cup: 2002, 2003, 2005, 2007, 2009, 2010, 2012 Champions League 2012 Europa League: 2013

RAMIRES KUTIMKA CHELSEA

Kiungo wa Chelsea Ramires yuko mbioni kujiunga na klabu ya China inayofamika kwa jina la Jiangsu Suning. Ramires, 28, alisajiliwa na Chelsea akitokea Benfica mwaka 2010 kwa kitita kinachokaribia pauni milioni 17. Anatarajiwa kujiunga kwenye ligi ya China Super League kwa dau linalotarajiwa kufikia kiasi cha pauni milioni 25. Ramires alisaini mkataba mpya na Chelsea October 2015 lakini hadi sasa amekuwepo kwenye kikosi cha kwanza kwenye mechi saba za Premier League ambapo Chelsea imekuwa ikipambana kupata matokeo. Jiangsu ilimaliza kwenye nafasi ya tisa kwenye ligi ya China msimu wa 2015 na kwasasa kikosi hicho kinanolewa na beki wa zamani wa The Blues Dan Petrescu. Akiwa Chelsea Ramires amefanikiwa kushinda the Premier League, FA Cup, League Cup, Champions League pamoja na Europa League.

Nyota wa filamu ya “Straight Outta Compton” Marekani awajapata mwaliko wa tuzo za Oscar mwaka huu

Waigizaji walioigiza kwenye filamu ya “Straight Outta Compton” hawajakaribishwa kwenye tuzo za Oscar na hata mtayarishaji wa filamu hio Ice Cube hajapata mualiko. Inasemekana hata Ice Cube angealikwa asinge hudhuria tuzo hizi ambazo zimepondwa mwaka huu baada ya waigizaji wengi weupe kuwania tuzo hizi kuliko weusi. Ice Cube atahudhuria tuzo za SAG na NAACP ambazo zote zimeweka filamu ya “Straight Outta Compton” kwenye tuzo zao.

Soma Mpango wa Yanga

YANGA imevunja ratiba yao ya kucheza na Coasta Union katika mchezo wa Ligi baada ya kutangaza kikosi chao kwenda Afrika Kusini katika mashindano mafupi. Mkuu wa Idara na Mawasiliano ya Yanga Jerry Muro amesema kikosi chao kinatarajiwa kuondoka nchini Ijumaa ya wiki hii tayari kwa mashindano hayo ambayo hata hivyo hawakuyaweka wazi. Muro amesema safari hiyo inataka kutumiwa na kikosi chao katika kujiweka sawa kabla ya kuanza mechi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika ambayo timu hiyo itafungua dhidi ya Cercle de Joachim ya Mauritius kati ya Februari 12-14. “Barua rasmi itapelekwa TFF na Katibu wetu Baraka Deusdedit kesho kuweza kuwajulisha kwamba tunalazimika kwenda huko baada ya uongozi wetu kukubali mualiko huo ambao ulifika muda tu lakini kuna mambo tulitaka yawekwe sawa,” amesema Muro. “Kwasasa timu tutakazocheza nazo tutaziweka wazi baada ya kupata ratiba lakini pia ikumbukwe kwamba tunashiriki Ligi ya Mabingwa sasa tutatumia nafasi hiyo

MANYIKA JR ALIVYOSHUHUDIA GAME YA YANGA VS RANGERS AKIWA NA MTOTO MZURI

Manyika Jr akiwa na mpenzi wake uwanja wa taifa akishuhudia game kati ya Yanga dhidi ya Friends  Rangers Golikipa wa Simba SC Peter Manyika jana alikuwa kivutio uwanjani akiwa na mpenzi wake wakati wakishuhudia mchezo wa Azam Sports Federation Cup kati ya Yanga dhidi ya Friends Rangers kwenye uwanja wa taifa mchezo uliomalizika kwa Yanga kusonga mbele kwa mabao 3-0. Hizi hapa ni picha ambacho zilinaswa na camera ya shafihdauda.co.tz ‘Timu ya Ushindi’ iliyokuwepo uwanja wa taifa kunasa matukio kadhaa.  inatoka www.shaffihdauda.co.tz

Rooney apata mtoto mwingine

Wayne Rooney alikuwa na furaha kama baba alipotuma picha nzuri Instagram ya mwanae mwingine, Kit, akiwa na umri wa dakika kadhaa Alikaribisha mtoto wa tatu wa kiume duniani wikiendi hii. Siku ya Jumatatu, Wayne Rooney alikuwa na furaha kama baba alipotuma picha nzuri Instagram ya mwanae mwingine, Kit, akiwa na umri wa dakika kadhaa. “Nakutana na Kit kwa mara ya kwanza. Muda wa kwenda nyumbani sasa,” mchezaji huyo aliandika katika picha hiyo. Rooney na mkewe Coleen wana watoto wengine Kai (kushoto) na Klay (kulia) Rooney, 30, na mkewe Coleen walitangaza kuzaliwa kwa mtoto wao wa kiume – waliompa jina la Kit Joseph Roone – siku ya Jumapili. Awali Coleen, 29, aliwahi kuzungumza kuwa anatamani kupata mtoto wa kike.

MC Galaxy wa Nigeria kufanya Kushiriki na mtoto wa Michael Jackson ‘Brandon

Msanii kutoka Nigeria Mc Galaxy anategemea kuwepo kwenye wimbo wa mtoto wa Michael Jackson ‘Brandon Howard’. Galaxy alionekana na kundi la marafiki wa Brandon Howard na yeye mwenyewe. Mc Galaxy ametajwa kuwepo kwenye wimbo mpya wa Brandon Howard uliorikediwa hivi karibuni nchini Marekani. Mpaka sasa MC Galaxy ameshafanya collabo na Busta Rhymes.

Wauzaji bidhaa holela soko la Buguruni wapigwa marufuku

Na Jacquiline Mrisho MAELEZO Halmashauri ya Manispaa ya Ilala yapiga marufuku uuzwaji holela wa bidhaa katika soko la Buguruni unaochafua mazingira ya soko na kuhatarisha afya za walaji. Hayo yamesemwa leo na Afisa Habari wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala David Langa wakati akifafanua kuhusu kero ya wauzaji holela wanaopanga bidhaa chini katika soko la Buguruni. “Bidhaa zinazopangwa chini katika soko la Buguruni sio rasmi na hakuna utaratibu unaoruhusu wauzaji kufanya biashara hiyo, hivyo

Mh .Rais Magufuli akiwa mkoani Arusha

JamiiForums Wananchi mkoani Arusha wamejitokeza kumlaki Rais Magufuli Jijini Arusha leo. Rais alikuwa amevalia magwanda ya kijeshi. Yupo Mkoani Arusha katika ziara yake ya kwanza ll iiii                                

LIVERPOOL KUMNASA MSHAMBULIAJI WA BRAZIL!!

Liverpool wanataka kumsajili mshambuliaji wa Shakhtar Donetsk Alex Teixeira mwenye asili ya kibrazil na kama dili hilo litafanikiwa huo utakuwa ni usajili mkubwa wa kwanza kufanywa na kocha Jurgen Klopp tangu awe manager wa kikosi cha Liverpool. Wekundu hao wako tayari kulipa kiasi cha pauni milioni 24.5 kwa ajili ya kuinasa saini ya nyota huyo mwenye miaka 26. Klabu ya nyota huyo ambaye pia anahusishwa na Chelsea imeweka dau la pauni milioni 39 kwa klabu inayotaka kumsajili mshambuliaji wao. Klopp anataka kuimarisha safu yake ya ushambuliaji kwa kuwa washambuliaji wake wengi ni majeruhi kwa sasa, Danny Ings, Divock Origi pamoja na Daniel Sturridge wote wanauguza majeraha. Usajili wa pauni milioni 32.5 kumnasa Christian Benteke umeshindwa kuzaa matunda yaliyotarajiwa baada ya timu hiyo kujikuta ikufunga mabao 25 katika mechi 22 za ligi kuu England hadi sasa. Teixeira ameshatupia kambani jumla ya magoli 22 kwenye mechi 15 za ligi na magoli me

Ukali wa Bendi ya Akudo Impact

SOMA MAPYA KUHUSU SAMATTA NA TP MAZEMBE

Baada ya dili la uhamisho wa mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania Mbwana Samatta kusuasua kutoka klabu yake ya TP Mazembe kwenda klabu ya Genk ya Ubeligiji, star huyo ameamua kurejea kwenye klabu yake hiyo ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kwa ajili ya mazungumzo na tajiri wa Mazembe Moise Katumbi kuhakikisha dili hilo linakamilika. Manager wa Samatta Jamal Kisongo amesema, mbali na mazungumzo, Samatta amerejea kwenye klabu yake ili aendelee kujifua hata kama ikitokea boss huyo akamfungulia mlango wa kutokea basi awe yuko fiti kuingia moja kwa moja kwenye timu kuliko kuendelea kukaa nyumbani. “Tumeona ni vyema Samatta akarejea Mazembe katika kumpa presha na kumsukuma Katumbi, amerejea kwenye kituo chake cha kazi na kumpa taarifa Katumbi kuwa kama hato muuza kwenye klabu ya Genk basi yeye atamalizia mkataba wake TP Mazembe na ataondoka mwezi April. Jambo ambalo kwa hakika Katumbi hawezi kukubaliana nalo kwakuwa anajua Samatta akiondoka mwezi Ap

MWANASAIKOLOJIA ANTI SADAKA AWAFUNDA WANAWAKE WA JIJI LA MWANZA

Mwanasaikolojia Anti Sadaka akitoa Mada kwenye Mafunzo ya ujasiriamali kwa wanawake wa Mkoa wa Mwanza yanayoendesha na  Taasisi ya Manjano foundation yanaoendelea kwenye ukumbi wa Rocky city Jijini Mwanza. Mwanasaikolojia Anti Sadaka amewafunda wanawake wa Mkoa wa Mwanza wanaoshiriki mafunzo ya ujasiriamali ya kujikita katika biashara ya Vipodozi vya LuvTouch Manjano. Mafunzo hayo yanaendeshwa  na wataalamu kutoka taasisi ya Manjano  Foundation  yanayoendelea Jijini Mwanza kwa wiki nzima. Anti Sadaka amewataka wanawake hao kujitambua kwa lengo la kufikia malengo yao waliojiwekea. Akieleza zaidi katika semina hiyo amewataka wanawake hao kujitambua wao ni nani  wana nafasi gani kwenye jamii inayowazunguka, kufanya kazi kwa bidii na kudumisha nidhamu yao kwa kila wakifanyacho kwa lengo la kufikia malengo yao. Wanawake wa Mkoa wa Mwanza wakifuatilia kwa amkini Mada zilizokuwa zinaendeshwa   kwenye Mafunzo hayo. Pia amewaasa wanawake wa

Tottenham v Sunderland katika dimba la White Hart Lane

Mshambuliaje wa Tottenham Harry Kane Tottenham inapambana na Sunderland katika mchezo wa mapema Ligi Kuu leo. Vikosi ni kama ifuatavyo; Tottenham XI: Lloris; Trippier, Alderweireld, Vertonghen, Rose; Dier, Dembele; Lamela, Eriksen, Alli; Kane Akiba: Vorm, Davies, Wimmer, Carroll, Chadli, Onomah, Son Msimamo wa Ligi Kuu Sunderland XI: Pickford; Jones, O’Shea, Brown, Van Aanholt; Johnson, Lens, Cattermole, M’Vila, Defoe, Graham Akiba: Rodwell, Borini, Coates, Fletcher, Kirchhoff, Watmore, Mannone Mshaambuliaji wa Sunderland Jermaine Defoe print

Soma Sani.Jarida Sasa ni kila Jumatano na si Jumatatu.

  Tumesikiliza maombi yenu wasomaji na wapenzi wa Sani.Jarida lenu Sani Katuni sasa ni kila Jumatano na si  Jumatatu. Usikose nakala yako iliyoboreshwa na kuongezwa kurasa kwa bei ileile ya Tsh, 1,000/= tu upate burudani isiyopatikana kwingineko duniani!

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Apewa Masaa 48 Ya Kujieleza

  NAIBU Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais ( Mazingira na Muungano) Luhaga Mpina amempatia saa 48 Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Magesa Mulongo kujieleza sababu za Jiji la Mwanza kuwa chafu. Mpina alisema hayo jana jijini hapa wakati akieleza mambo aliyoyabaini wakati wa ziara yake ya siku mbili jijini Mwanza. Alisema licha ya serikali kutangaza suala la usafi kuwa ni hoja ya kitaifa, Jiji la Mwanza linatisha kwa uchafu wa mazingira. Mpina ambaye alianza ziara jana kukagua maeneo mbalimbali ya jiji, alisema uchafu wa jiji kwa kiwango kikubwa unachangiwa na baadhi ya watendaji wa Serikali na wataalamu, kutowajibika vyema. “ Ni sehemu ndogo tu ya uchafu wa jiji la Mwanza unaochangiwa na wananchi, kutokana na hali hii nilivyoiona ninampatia Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Magesa Mulongo masaa 48 ajieleze ni kwanini jiji la Mwanza ni chafu ilihali lina watendaji wa kutosha na wataalamu”, alisema. Alisema Januari 30 mwaka huu atarudi jijini Mwanza, kushiriki usafi n

Angalia Mpendwa huyu anavyo tililika kwa shukrani za Mora

Lucy Andrew feeling blessed with Judith Raphael and 6 others . 13 mins · Am saving a living God who z always by my side......my Lord z awesome always God z good all da time....am favoured and blessed....... sintoacha kuimba fadhili zake ni nyingi maishani mwangu.....Your grace z enough for me

Jaribu kumsoma Mtanzania huyu

Flaviana Matata 14 mins · Leo tarehe 11.01.2016 Taasisi ya Flaviana Matata imezindua rasmi msimu wa "BACK TO SCHOOL" kwa kutoa vifaa vya shule kwa jumla ya watoto 270 wa Shule ya Msingi Msinune. Tunawashukuru wale wote walio wezesha zoezi hili INSPIRE | EMPOWER | SUPPORT 111 Likes 13 Comments 2 Shares

Klabu ya Etoile yatakiwa kuilipa Simba haraka

Emmanuel Okwi Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA) iliyokutana Disemba 15 mwaka jana, imeiagiza klabu ya Etoile du Sahel ya Tunisia kuilipa Simba SC ya Tanzania pesa za uhamisho wa mchezaji Emmanuel Okwi ndani ya siku sitini (60) kuanzia Januari 7, 2016. Katika taarifa hiyo ya FIFA na nakala yake kutumwa kwa TFF, Etoile du Sahel na Simba SC, Kamati ya Nidhamu imefikia uamuzi huo baada ya klabu ya Etoile du Sahel kupuuza kuilipa klabu ya Simba SC kiasi cha dola za kimarekani 300,000 za uhamisho wa mchezaji wa Emmanuel Okwi uliofayika Januari 2014. Katika barua hiyo ya maamuzi ya kikao hicho, Kamati ya Nidhamu imesema baada ya siku sitini (60) zilizotolewa kwa klabu ya Etoile kuwa imeilipa Simba SC kumalizika bila malipo hayo kuwa yamaefanyika, wataagiza Etoile du Sahel kuk

Msanii Nigeria Atajwa kutorudi kwenye ubora wake baada ya kujifungua

Blog za Nigeria zimetoa mitazamo tofauti kuhusu ubora wa msanii Tiwa Savage kwenye stage baada ya kujifungua na kusema bado hawajaona ubora wake wa awali. Tiwa Savage kwa sasa yuko barabarani akifanya show kwaajili ya kutangaza album yak mpya ya “RED” . Tiwa Savage aka Mavin Queen, African titan, urban tastemaker, pop darling ametumia nguvu nyingi kutangaza album yake mpya ya “RED” na kufanya mazoezi ya kufanya show kali tena. Wakati wa ukimya Tiwa alitumia muda wake kurekodi album yake na kujianda kulea mtoto wake, pia wakati huu muziki wa wasanii kama Yemi Alade na Seyi Shay ulipata nafasi kubwa kwneye maisha ya Wanigeria.

UDA-RT yasalimu amri viwango vya nauli

Moja ya basi liendalo kasi la Kampuni ya DART Kampuni ya Mabasi yaendayo Kasi jijini Dar es Salaam (UDA-RT) imesema haina ugomvi na serikali na kwamba itakubaliana na kiwango chochote itakachoona kinafaa. Akizungumza kwa njia ya simu jana, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, David Mgwassa, alisema kiwango walichopendekeza na kujadiliwa katika Baraza la walaji la Mamlaka ya Usafirishaji wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra) kisitafsiriwe kuwa ni nauli halali, badala yake inaweza kukubalia au kukataliwa na serikali. Juzi, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, alikataa ongezeko la nauli mpya kwa mabasi yaendayo kasi, alisema nauli hiyo itasababisha mzigo kwa wanbanchi na watumishi wa umma. Alizitaka mamlaka husika zikiwemo TAMISEMI, Wizara ya Ujenzi, Sumatra na UDA-RT kukaa haraka kurekebisha viwango hivyo. Kiwango kilichopendekezwa na UDA ni Sh. 1,200 kwa safari ya njia kuu na Sh. 1,400 kwa njia ya pembeni, wanafunzi watalipa nusu ya kiasi hicho kwa

UEFA’s 2015 Team of the Year 'Bab Achaa Kabisa ' Barca ni tishio

Mshambuliaji wa Barcelona Lionel Messi Nyota wa Barcelona wameonekana kutawala katika kikosi cha Timu ya Mwaka ya UEFA huku kukiwa hakuna hata mchezaji mmoja wa Ligi Kuu kushiriki katika kikosi hiko. UEFA ilitangaza kikosi hiko siku ya Ijumaa asubuhi baada kupigiwa kura na watumiaji wa mtandao wao. Mlinda mlango wa Bayern Munich Manuel Neuer Washambuliaji wawili wa Barcelona Lionel Messi na Neymar ndio wanaounda safu ya mbele ya 4-3-3 wakishirikiana na mfungaji magoli wa Real Madrid Cristiano Ronaldo. Kiungo wa Juventus Paul Pogba Lionel Messi alijizolea kura 448,445 kutoka kwa watumiaji wa mtandao wa UEFA. Mlinzi wa Bayern Munich David Alaba (kushoto) Katika kikosi hiko wamo nyota wengine wa Barca kama Dani Alves, Gerard Pique na Andres Iniesta. UEFA’s 2015 Team of the Year Wengine kutoka ligi nyingine ni Manuel Neuer, David Alaba na Paul Pogba.