Mwimbaji mahiri wa kundi la Jahazi Modern Taarab Mzee Yusufu usiku wa jana alizindua albamu mpya ya kundi hilo iitwayo Kaning’ang’ania katika ukumbi wa Dar Live Mbagala jijini hapa.
Baadhi ya nyimbo nyingine zilizo pagawisha mashabaki katika uzinduzi huo ni 'Limekuuma' ya Fatma Ally, 'Nia Safi Hairogwi' ya Mish Mohyamed, 'Nina Moyo Sina Jiwe' ya Leila Rashid pamoja na Mashallah ya Mzee Yusuf akiwa na Vanessa Mdee
Malkia wa mipasho Bi Khadija Kopa nae atakuwa na lake jipya liitwalo Ogopa Kopa ni mmoja wa wasindikizaji wa onyesho hilo waliofanya balaa kwa kuibua shangwe
Comments