Kiungo wa Chelsea Ramires yuko mbioni kujiunga na klabu ya China inayofamika kwa jina la Jiangsu Suning.
Ramires, 28, alisajiliwa na Chelsea akitokea Benfica mwaka 2010 kwa kitita kinachokaribia pauni milioni 17.
Anatarajiwa kujiunga kwenye ligi ya China Super League kwa dau linalotarajiwa kufikia kiasi cha pauni milioni 25.
Ramires alisaini mkataba mpya na Chelsea October 2015 lakini hadi
sasa amekuwepo kwenye kikosi cha kwanza kwenye mechi saba za Premier
League ambapo Chelsea imekuwa ikipambana kupata matokeo.
Jiangsu ilimaliza kwenye nafasi ya tisa kwenye ligi ya China msimu wa
2015 na kwasasa kikosi hicho kinanolewa na beki wa zamani wa The Blues
Dan Petrescu.
Akiwa Chelsea Ramires amefanikiwa kushinda the Premier League, FA Cup, League Cup, Champions League pamoja na Europa League.
Comments