Katibu
Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Mwesigwa Selestine leo Jumatano anatarajiwa kuongozana na mshambuliaji wa timu ya Taifa
ya Tanzania na klabu ya TP Mazembe ya Congo DR, Mbwana Samatta kuelekea
nchini Nigeria kwenye sherehe za utoaji wa tuzo kwa wachezaji bora
barania Afrika.
Mwesigwa
anatarajiwa kuondoka na Samatta kuelekea Nigeria katika mji wa Abuja
ambapo sherehe za utoaji tuzo hizo zitafayika Alhamisi Januari 7, ambapo
siku ya sherehe hizo Katibu Mkuu ataambatana na Ofisa ubalozi wa
Tanzania nchini Nigeria
Mbwana
Samatta anawania tuzo ya mchezaji bora wa Afrika kwa wachezaji wa ndani,
huku pia akiwa mfungaji bora wa michuano ya Ligi ya Mabingwa (CAF CL)
baada ya kuifungia klabu yake ya TP Mazembe mabao 8 na kuibuka mabingwa
wapya wa michuano hiyo.
Rais wa
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amemtakia
kila la kheri Mbwana Samatta katika kinyanganyiro hicho cha uchezaji
bora na kusema kwa niaba ya watanzania wote wanamuombea dua njema aweze
kuibuka mchezaji bora wa Afrika kwa wachezaji wa ndani.
Samatta
anawania tuzo ya mchezaji bora wa Afrika pamoja na mlinda mlango wa TP
Mazembe, Robert Kidiaba (Congo DR) na mshambuliaji wa Etoile du Sahel
Baghdad Boundjah (Algeria).(P.T)
Comments