Skip to main content

Posts

Showing posts from November, 2017

MAWAZIRI WANNE WA UGANDA WAFANYA ZIARA NCHINI

2 3 4 f Waziri wa Madini, Angellah Kairuki amekutana na mawaziri wanne kutoka nchini Uganda ambao wamewasili nchini Tanzania kwa ajili ya ziara ya siku mbili ya kubadilishana uzoefu katika usimamizi wa Sekta ya Madini. Mawaziri hao ni Waziri wa Nchi- Madini, Lokeris Peter, Waziri wa Nchi- Mambo ya Ndani, Obiga Kania, Waziri wa Nchi- Mamlaka ya Mji Mkuu wa Kampala, Namugwanya Bugembe na Waziri wa Nchi- Masuala ya Uchumi, Dkt. Kasirivu Atwooki. Waziri Kairuki amekutana na ujumbe huo Novemba 28, 2017 katika Ofisi za Wizara ya Madini jijini Dar es Salaam na kujadiliana masuala mbalimbali ya uendeshaji wa shughuli za Madini nchini ikiwemo suala la Sera, Sheria na Kanuni za Madini pamoja na masuala yanayohusu Wachimbaji Wadogo wa madini. Majadiliano baina ya Wizara na Ujumbe huo vilevile yalihusisha uwasilishaji wa mada mbalimbali kutoka kwa Kamishna wa Madini, Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST) na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO). Ujumbe huo utatembelea migodi mba

Waziri Mkuu Majaliwa amuagiza IGP Sirro kuwakamata vigogo hawa

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemtaka Inspekta Jenerali wa Polisi, Simon Sirro kuwakamata, Bw. Bahman wa kampuni ya NAS na Wakala wa Kampuni ya Wallmark Bw. Samwel kwa kutaka kutoa bandarini magari makubwa aina ya semi tela 44 bila ya kulipa kodi kwa kutumia jina la Waziri Mkuu. Pia Waziri Mkuu ameitaka Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) kufanya kazi kwa mujibu wa sheria na kutowasikiliza wafanyabiashara wanaotaka kukwepa kodi kwa madai ya kupewa vibali vya msamaha wa kodi kutoka kwa viongozi wa juu Serikalini. “Mtu asije hapa aseme amepewa kibali na Rais Dkt. John Magufuli, Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan au Waziri Mkuu cha kutaka kutoa mzigo wake bila ya kufuata taratibu. Akija mtu na taarifa hizo akamatwe mara moja na achukuliwe hatua kwa mujibu wa sheria.” Ametoa agizo hilo leo (Jumatano, Novemba 29, 2017) alipofanya ziara ya ghafla bandarini baada ya kupata taarifa za mfanyabiashara huyo aliyetaka kuutapeli uongozi wa TPA kutaka kutoa magari hay
Viongozi wa (CUF) chini ya Katibu Mkuu na Lipumba wameanza  kutupiana lawama na kushikana uchawi, Naibu Mkurugenzi wa Habari na  Uenezi wa CUF Mbarala Maharagande amefunguka na kusema Maalim  Seif analindwa na haki na si ushirikina. Mbarala Maharagande amedai kuwa Lipumba na kundi lake ni  watu ambao wanaamini sana ushirikina na kutegemea ushirikina  kufanikisha mpango wao kuivuruga na kuisambaratisha Taasisi ya CUF. "Lipumba na wafuasi wake ni watu wanaoamini sana mambo ya  ushirikina katika kufanikiwa mipango yao michafu dhidi ya Taasisi  ya CUF.  Mara kadhaa wameonekana kutumwa wafuasi wake kwenda  kununua Mbuzi kwa ajili ya kazi hiyo katika mnada wa  Vingunguti. Kamati ya ushirikina inaongozwa na Abdul  Kambaya na Hamisi Hassan kwa upande wa Tanzania  Bara na Mohamed Thiney na Nassor Seif kwa upande  wa Zanzibar" aliandika Naibu Mkurugenzi wa Habari na  Uenezi wa CUF Mbarala Maharagande Mbali na hilo Mbarala amesema kuwa Pr

WADAU WA MIFUGO WAMEIOMBA SERIKALI WASIHAME HAME KUNASABABISHA UFUGAJI USIO NA TIJA

Wadau wa mifugo  imeshauriwa kuweka mazingira mazuri kwa sekta ya mifugo ili kuongeza uzalishaji wa bidhaa zinazotokana na mifugo. Wadau wa sekta hiyo wamesema hayo Dar es Salaam Jumanne Novemba 28,2017 wakati wa uzinduzi wa mkakati wa ushawishi wa sera ya mifugo ulioandaliwa na jukwaa lawadau wa kilimo (Ansaf)ambapo wametaka Serikali ihakikishe wafugaji wanafanya shughuli zao katikamaeneo yanayoeleweka na si kuhamahama kama ilivyo sasa. Hadi sasa sekta ya ufugaji inatajwa kama  sekta inayokuwa kwa kasi ya asilimia 5o hapa nchini hapa huku Tanzania ikitajwa kuwa ni nchi ya tatukwa kuwa na wanyama wanaofugwa baada ya nchi za Ethiopia na Sudani. Katibu mkuu wa chama cha wafugaji nchini, Magembe Makoye amesema kuhamahama wafugaji kunasababisha ufugaji usio na tija na manufaa kwa viwanda, hivyo sekta hiyo kuendelea kuendeshwa kwa mazoea. “Hatuwezi kuzungumzia ufugaji wa tija au uchumi wa viwanda kama wafugaji wataendelea kuzunguka na kuhamahama. Muhimu wahakikishiwe usalama na utuli

Gattuso ameteuliwa kuwa kocha mpya wa klabu AC Milan

Kiungo wa zamani wa AC Milan,  Gennaro Gattuso ameteuliwa kuwa kocha mpya wa klabu hiyo baada ya  Vincenzo Montella   kutimuliwa kufuatia mwenendo mbaya msimu huu katika Ligi Kuu ya Italia - Seria A. Licha ya usajili wa bei mbaya uliofanywa na wamiliki wapya matajiri wa Kichina, AC Milan iko nafasi ya saba kwenye msimamo wa Seria A, ikiwa imeachwa kwa pointi 18 na vinara Napoli.

Kupitia mtandao wake wa twitter Zitto Kabwe ameandika hivi

Mh.Rais John Pombe  Magufuli-na-Zitto

Mazungumzo mapya kuhusu mgogoro wa Burundi kuanza Jumatatu hii Arusha

Polisi ikipiga doria katika mitaa ya Ngagara, kaskazini mwa Bujumbura, Aprili 25, 2015. Mazungumzo mapya kuhusu mgogoro wa kisiasa wa Burundi yanaanza tena Novemba 27 hadi Desemba 8, kwa mujibu wa timu ya Mwezeshaji katika mgogoro huo, rais wa zamani wa Tanzania, Benjamin Mkapa. Mazungumzo hayo mapya yatakayo dumu wiki mbili yatakua ni yenye maamuzi, kwa mujibu wa chanzo kilio karibu na timu ya Mwezeshaji. Mazungumo haya yatadumu siku 13 ili kujaribu kutafuta suluhu ya mgogoro huo uliibuka baada ya rais Pierre Nkurunziza kutangaza nia yake ya kuwania muhula wa tatu wa urais mwaka 2015. Hii itakua mara ya kwanza serikali ya Burundi kushiri mazungumzo nje ya nchi. Serikali imemtuma Katibu wa kudumu kwenye wizara ya Mambo ya Ndani, Therence Ntahiraja kushiriki mazungumzo hayo. Pia kiongozi wa chama tawala Evariste Ndayishimiye, akiambatana na viongozi wa vyama vya upinzani vinavyounga mkono serikali na mashirika ya kiraia kutoka Bujumbura watakuepo mjini Arusha ili kujaribu

Azam , Mtibwa Sugar zatoshana nguvu kwa sare ya bao 1-1

Timu ya Azam FC jana usiku imetoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Mtibwa Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) uliofanyika Uwanja Azam Cmplex. Timu ya Azam FC imetoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Mtibwa Sugar katika mchezo wa Ligi  Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) uliofanyika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam, jana usiku. Sare hiyo inaifanya Azam FC kufikisha jumla ya pointi 23 kwenye msimamo wa ligi hiyo sawa na vinara Simba wanaoongoza kwa tofauti ya mabao ya kufunga na  kufungwa. Mchezo huo uliokuwa mkali na wa aina yake ilishuhudiwa timu zote zikionyeshana  upinzani lakini Azam FC ilionekana kuutawala kwa kiasi fulani, ambayo ilijipatia bao la uongozi dakika ya 56 likifungwa kwa kichwa na winga Enock Atta akiunganisha krosi iliyopigwa na Mbaraka Yusuph. Hilo ni bao la kwanza kwa Atta kwenye msimu huu wa ligi likiwa pia la kwanza kufunga  katika ligi hiyo tokea usajili wake ulipokamilika msimu huu. Mtibwa Sugar ilisubiri hadi

200 waomba kujiunga CCM

Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM, Humphrey Polepole amesema kuna wanachama wa vyama vya upinzani 200 ambao wameomba kujiunga na CCM. Akizungumza leo Jumanne wakati wa kutangaza majina ya viongozi wa mikoa na kitaifa walioomba nafasi mbalimbali za uongozi CCM, Polepole amesema wapinzani walioomba kujiunga na chama hicho wamo wabunge na wenyeviti. Amesema sababu waliyotoa ya kutaka kuhamia CCM ni kutokana na chama hicho kushughulika na matatizo ya watu. Polepole amesema chama kimewapokea wanachama wapya kutoka vyama vya upinzani. Amewataja wanachama hao kuwa ni Samson Mwigamba, Albert Msando na Profesa Kitila Mkumbo kutoka ACT-Wazalendo. Wengine na Lawrence Masha  na Protobas Katambi wa Chadema. "Tutawajulisha siku tutakapowapokea wanachama hawa wapya," amesema. Source:Mwananchi

TAMWA na maadhimisho ya Siku 16 Kupinga Ukatili wa Kijinsia

Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA), Bi. Edda Sanga akizungumza leo na wanahabari akutoa kauli ya maadhimisho ya Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia kwa chama hicho. Kushoto ni Ofisa Habari wa TAMWA, Happines Bagambi. Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA), Bi. Edda Sanga akizungumza leo na wanahabari akutoa kauli ya maadhimisho ya Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia kwa chama hicho. Kulia ni Afisa Mipango wa TAMWA, Strategic Manager.   Baadhi ya wanahabari na wasaidizi wa sheria ngazi za jamii wakifuatilia hotuba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA), Bi. Edda Sanga katika mkutano huo.  aadhi ya wanahabari na wasaidizi wa sheria ngazi za jamii wakifuatilia hotuba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA), Bi. Edda Sanga katika mkutano huo.  Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA), Bi. Edda Sanga akizungum

Inaelezwa Watu 235 wauawa nchini Misri baada ya kushambuliwa msikitini

Msikiti Kaskazini mwa Misri Watu 235 wamepoteza maisha katika mkoa wa Sinai nchini Misri baada ya watu waliokuwa wamejihami kwa silaha kuvamia na kushambulia Msikiti mmoja Kaskazini mwa nchi hiyo. Hili ndilo shambulizi baya zaidi kuwahi kutokea na kushuhudiwa katika miaka ya hivi karibuni. Walioshuhudia shambulizi hili baya wanasema wavamizi hao wakiwa wamejihami kwa mabomu na silaha, walizingira msikiti huo na kuwashambulia waumini wa Kiislamu waliokuwa msikiti siku ya Ijumaa wakiwa ibadani. Watu 109 wamejeruhiwa katika shambulizi hilo ambalo serikali ya Misri imesema ni la kigaidi. Rais Abdel Fattah al-Sisi amelaani shambulizi hilo na kutangaza siku tatu za maombolezo kuwakumbuka waliopoteza maisha. Al Sisi amesema serikali yake itatumia nguvu kulipiza kisasi dhidi ya magaidi hao. Rais wa Marekani Donald Trump naye amelaani shambulizi hilo na kusema limetekelezwa na watu waoga. Waziri wa Mambo ya nje wa Ufaransa Jean-Yves Le Drian na mwenzake wa Uingereza Bor

RTO ARUSHA:TUTAFANYA MSAKO WA KUWAKAMATA MADEREVA WASIOKUWA NA LESENI ZA UDEREVA

baadhi ya magari Arusha|(picha na mtandao) Jeshi la Polisi kikosi cha usalama barabarani mkoani Arusha limewataka waendesha vyombo vya moto kuhakikisha wanafata sheria na taratibu za usalama barabarani ikiwa ni pamoja na kuepuka kuendesha gari pasipokuwa na leseni ama vyeti vya udereva. Hayo yamesemwa leo na Mrakibu wa polisi na mkuu wa kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Arusha RTO,Joseph Charles Bukombe wakati akizungumza na Mussatz Blog ambapo amesema wamejipanga kufanya msako wa kuwakamata madereva ambao wamekuwa wakikiuka sheria na taratibu za usalama barabarani. RTO Bukombe amesema ni vyema madereva wanaoendesha vyombo vya moto hususani wanaowapakia abiria kuhakikisha wanavyeti vinavyowaruhusu kuwapakia abiria kwani hatima ya watu wanaowabeba ipo mikononi mwao. Amesema wanakumbana na changamoto mbalimbali ikiwemo baadhi ya madereva kutofuata alama za barabarani lakini pia kuvunja sheria za usalama barabarani kwa makusudi pasipokuchukua tahadhari kwa watembe
Msanii na mwanamitindo wa muda mrefu, DJ Waiz mbali na  kuachia kazi zake kama ‘Shobo Robo’ huku akichapamwendo wa kasi katika kutafuta manufaa ya muziki wake amsema kuwa yupo katika hatua za mwisho kuamishia maskani ya shughuli zake Dar es Salaam akitokea Zanzibar. Moja ya nyimbo zake ni pamoja na video ya wimbo wake ‘Shobo Robo’ ambayo alioshirikiana na Baby Jay na Kijukuu. DJ Waiz  amesema mbali na kuwa alijikita visiwani humo kwa muda mrefu  kutokana na majukumu ya anayojipangia sasa imebadilisha taswira na anataka kutia  jijini hapa. “Mmuziki umekuwa katika hatua zake nyingi za maendeleo nchini hadi sasa kumekuwa kukuongezeka badiliko la aina yake katika muziki wa Bongofalava” Amesema DJ Waiz. Video ya wimbo huo imetayarishwa na Director Pablo na katika video hiyo wanamitindo mbali mbali walishirikishwa akiwemo Chidy Adore na wengine wengi.

Sikia maneno haya kutoka kwa Lema:Kafulila Usiende CCM peke yako, Nenda na Mkeo

  Kwenye ukurasa wake wa twiter Godbless Lema ameandika ujumbe  akisema Kafulila ni rafiki yake wa karibu, lakini kwa namna alivyoamua  hana shaka atamshauri mke wake ambaye ni mbunge kupitia chama  cha CHADEMA, kufanya kama yale aliyoyafanya. "David Kafulila ni rafiki yangu, nafikiri kwa namna hii alivyoamua ataweza  bila shaka kumshauri Mbunge wa Chadema, Jesca Kishoa (mke wake)  kufikiri kama yeye, hii inaweza kusaidia maoni yake juu ya uamuzi  aliouchukua leo na kuthibitisha ukweli huu kama hupo", ameandika  Godbless Lema. Jana David Kafulila ametangaza kukihama chama cha CHADEMA  akidai vyama vya upinzani havina nia ya kupambana dhidi ya ufisadi,  lakini mke wake Jesca Kishoa ambaye ni mbunge wa viti maalum  kupitia CHADEMA bado hajazungumza chochote.

Soma hapa Dkt Slaa Baada ya Kuteuliwa Kuwa Balozi

Dk Slaa enzi akiwa Katibu Mkuu wa Chadema (Picha na Maktaba)     Aliyekuwa Katibu Kuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dkt.   Wilbroad Slaa amezungumzia hatua aliyoichukua Rais John Magufuli kumteua kuwa  Balozi. Dkt. Slaa amesema ubalozi ni nafasi ambazo zipo katika himaya ya Mkuu wa Nchi  hivyo bila shaka hadi Rais kufikia hatua ya kumteua atakuwa na sababu za uteuzi huo. “Hatimaye kama ni mapenzi wa Mungu namshukuru kwa uteuzi huo ninachoweza  kusema katika hatua hii ni kwamba ni wajibu mkubwa katika kipindi hiki cha  kujenga taifa letu. Kama ni kutoa mchango wangu nitakuwa tayari kutoa,  Mwenyenzi Mungu akinisaidia” Dkt. Slaa amekiambia kituo cha runinga  cha Azam. Hapo jana November 23, 2017 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  Rais Dkt. John Magufuli alimteua Dkt. Wilbroad Slaa kuwa Balozi na inatarajiwa  ataapishwa pindi taratibu zikikamilika.