Kwenye ukurasa wake wa twiter Godbless Lema ameandika ujumbe
akisema Kafulila ni rafiki yake wa karibu, lakini kwa namna alivyoamua
hana shaka atamshauri mke wake ambaye ni mbunge kupitia chama
cha CHADEMA, kufanya kama yale aliyoyafanya.
"David Kafulila ni rafiki yangu, nafikiri kwa namna hii alivyoamua ataweza
bila shaka kumshauri Mbunge wa Chadema, Jesca Kishoa (mke wake)
kufikiri kama yeye, hii inaweza kusaidia maoni yake juu ya uamuzi
aliouchukua leo na kuthibitisha ukweli huu kama hupo", ameandika
Godbless Lema.
Jana David Kafulila ametangaza kukihama chama cha CHADEMA
akidai vyama vya upinzani havina nia ya kupambana dhidi ya ufisadi,
lakini mke wake Jesca Kishoa ambaye ni mbunge wa viti maalum
kupitia CHADEMA bado hajazungumza chochote.
Comments