baadhi ya magari Arusha|(picha na mtandao)
Jeshi la Polisi kikosi cha usalama barabarani mkoani Arusha limewataka waendesha vyombo vya moto kuhakikisha wanafata sheria na taratibu za usalama barabarani ikiwa ni pamoja na kuepuka kuendesha gari pasipokuwa na leseni ama vyeti vya udereva.
Jeshi la Polisi kikosi cha usalama barabarani mkoani Arusha limewataka waendesha vyombo vya moto kuhakikisha wanafata sheria na taratibu za usalama barabarani ikiwa ni pamoja na kuepuka kuendesha gari pasipokuwa na leseni ama vyeti vya udereva.
Hayo yamesemwa leo na Mrakibu wa polisi na mkuu wa kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Arusha RTO,Joseph Charles Bukombe wakati akizungumza na Mussatz Blog ambapo amesema wamejipanga kufanya msako wa kuwakamata madereva ambao wamekuwa wakikiuka sheria na taratibu za usalama barabarani.
RTO Bukombe amesema ni vyema madereva wanaoendesha vyombo vya moto hususani wanaowapakia abiria kuhakikisha wanavyeti vinavyowaruhusu kuwapakia abiria kwani hatima ya watu wanaowabeba ipo mikononi mwao.
Amesema wanakumbana na changamoto mbalimbali ikiwemo baadhi ya madereva kutofuata alama za barabarani lakini pia kuvunja sheria za usalama barabarani kwa makusudi pasipokuchukua tahadhari kwa watembea kwa miguu.
Halikadhalika RTO Bukombe amewataka wamiliki wa magari pale wanapotaka kuwaajiri madereva wajiridhishe kama wanavyeti na leseni husika ya kuendesha magari yao.
Hata hivyo amesema watawachukulia hatua kali za kisheria madereva wote ambao hawatii sheria bila shuruti za usalama barabarani ili kuendana na kaulimbiu ya mwaka huu ya usalama barabarani isemayo endesha salama okoa maisha tii sheria.
Comments