Na mwandishi wetu
RAIS Dk John Magufuli ameagiza jengo la makao makuu ya shirika la umeme(Tanesco) na lile la wizara ya maji lililopo Ubungo kuwekewa alama ya X ili kuvunjwa.
Makao Makuu ya Tanesco
Ametoa agizo hilo leo jijini Dar es Salaam alipokuwa katika ziara ya kukagua ujenzi wa daraja la ghorofa tatu makutano ya barabara eneo la Ubungo
"Ikiwezekana leo au kesho muweke x katika jengo la Tanesco na lile la wizara ya maji ambapo ukuta wake upo sehemu ya ndani ya barabara. Sheria ni msumeno hata serikali ikifanya kosa inasurubiwa na hata raia akijenga kwenye hifadhi ya barabara anasurubiwa," amesema rais na kuongeza
"Sheria ya hifadhi ya barabara ilianza tangu mwaka 1932 ikafanyiwa mabadiliko mwaka 1959,1963 na 1997 ukubwa wa barabara Morogoro kutoka mjini ni mita 22.5 kwa 22.5."
- Get link
- X
- Other Apps
- Get link
- X
- Other Apps
Comments