Viongozi wa (CUF) chini ya Katibu Mkuu na Lipumba wameanza
kutupiana lawama na kushikana uchawi, Naibu Mkurugenzi wa Habari na
Uenezi wa CUF Mbarala Maharagande amefunguka na kusema Maalim
Seif analindwa na haki na si ushirikina.
Mbarala Maharagande amedai kuwa Lipumba na kundi lake ni
watu ambao wanaamini sana ushirikina na kutegemea ushirikina
kufanikisha mpango wao kuivuruga na kuisambaratisha Taasisi ya CUF.
"Lipumba na wafuasi wake ni watu wanaoamini sana mambo ya
ushirikina katika kufanikiwa mipango yao michafu dhidi ya Taasisi
ya CUF.
Mara kadhaa wameonekana kutumwa wafuasi wake kwenda
kununua Mbuzi kwa ajili ya kazi hiyo katika mnada wa
Vingunguti. Kamati ya ushirikina inaongozwa na Abdul
Kambaya na Hamisi Hassan kwa upande wa Tanzania
Bara na Mohamed Thiney na Nassor Seif kwa upande
wa Zanzibar" aliandika Naibu Mkurugenzi wa Habari na
Uenezi wa CUF Mbarala Maharagande
Mbali na hilo Mbarala amesema kuwa Profesa Lipumba na
kundi lake wameshindwa kuigawa CUF kama ambavyo walikuwa
wakitegemea na kudai uchaguzi mdogo wa udiwani umeweza kutoa
majibu kwani wagombea wote wa Lipumba wamepata kura
chache sana na kuonekana wazi kuwa watu hao hawakubaliki
katika jamii.
"Lipumba na wafuasi wake wameshindwa kuigawa CUF na
mbeleko ya CCM inakaribia kukatika kutokana na kutoona faida
yao hasa katika ushindani wakati wa uchaguzi. Watazania
washawafahamu kuwa ni vibaraka, wasaliti na wachumia
tumbo, hawapo kwa dhati ya kutaka Mabadiliko ya kweli
kisiasa kutokea hapa nchini.
Mgombea wa Lipumba katika Kata ya Reli, Mtwara Mikindani kushika
nafasi ya nne kwa kupata kura 21 baada ya CCM, CHADEMA, na
ACT katika Jimbo linaloongozwa na Mbunge kutoka ‘CUF MAKINIKIA’
ni salamu tosha kwa Maftaha Nachuma na Lipumba kuwa
hawakubaliki na hawana mchango wa maana kwa CCM"
alisisitiza Mbarala
Pia Naibu Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa CUF Mbarala
Maharagande amekanusha taarifa inayosema kuwa Maalim
Seif anashirikiana na waganga wa kienyeji na kuwa mambo
yamezidi kuwa magumu kwake.
"Eti Maalim Seif anashirikiana na Waganga na mambo
yanazidi kuwa magumu kwake! Mambo yepi magumu
na Spika anatakiwa atangaze rasmi lini Wabunge halali wa
CUF waanze utumishi wao Bungeni kutokana na maamuzi
ya Mahakama. Msemaji wa Lipumba, David Maphone
kahamia kuwapigia kampeni wagombea wa UVCCM sasa"
Comments