Shekhe mkuu wa dhehebu la shia ithna sheria Ahmed Jalala akizungumza na wanahabari(picha na Ashura Dunda)
Na Ashura Dunda Dar es salaam
Zaidi ya waumini milioni thelasini wa dhehebu la shia ithna sheria kutoka mataifa mbalimbali wamewasili karbal nchini Iraaq katika kumbukumbu ya arubaini ya Imam Hussein kwa lengo la kumbukumbuka ya kifo cha imam huyo.
Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es salaam Shekhe mkuu wa dhehebu la shia ithna sheria Ahmed Jalala amesema tukio hilo la arubaini ya Imamu Hussein ambaye ni mjukuu wa Mtume Muhammad (S.A.W) ni tukio la kawaida kwa waumini wa dini ya kiislam.
Aidha Jalala amebainisha mafunzo yatokanayo na tukio hilo ni pamoja na kuuenzi utukufu na heshma ya mwanadamu Duniani pamoja na kujenga umoja, upendo, amani na mshikamano Nchini.
Aidha amewataka waumini wa dini ya kiislam na wasiokuwa waislam kuhakikisha wanapokea mafunzo wanayoyapata katika kujikita kusimamia amani na upendo.
Katika tukio la Arbaini ya Imamu Hussein mwaka huu kauli mbiu yake ni Tusimame Kutetea haki za binaadam na kupinga ugaidi.
Comments