David Moyes amekaribishwa kwa kipigo West Ham baada ya kuishuhudia timu yake hiyo mpya ikilambwa 2-0 na Watford katika mchezo wa Ligi Kuu ya England.
Moyes aliyevurunda Manchester United na Valencia, anaingia kwenye hatari ya kuishusha daraja timu nyingine baada ya msimu uliopita kuishusha Sunderland.
Magoli ya Will Hughes na Richarlison yakaifanya West Ham ipate kipigo cha saba msimu huu ndani ya mechi zake 12 za Premier League na kuendelea kubaki nafasi ya tatu kutoka chini.
Comments