Katibu mkuu wa wizara ya Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano amewataka wakandarasi kufanya kazi kwa uadilifu
Katibu mkuu wa wizara ya Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano,Mhandisi Joseph Nyamhanga akizungumza kwenye mkutano wa siku ya makandarasi uliofanyika Diamond Jubilee jijini Dar es salaam
Katibu mkuu wa wizara ya Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano,Mhandisi Joseph Nyamhanga kwenye picha ya pamoja na makandarasi walihudhuria kwenye mkutano huo
makandarasi mbalimbali walihudhuria kwenye mkutano wa siku ya makandarasi(picha zote na blog hii)
Na Mussa.N.Khalid
Wakandarasi kutoka maeneo mbalimbali nchini wametakiwa kufanya kazi kwa uadilifu ikiwa ni pamoja na kuepuka kupokea rushwa ili kutekeleza kwa wakati miradi mbalimbali ya kimaendeleo.
Katibu mkuu wa wizara ya Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano,Mhandisi Joseph Nyamhanga ameyasema hayo leo alipokuwa mgeni rasmi kwenye mkutano wa siku ya makandarasi ambao umefanyika jijini Dar es salaam.
Mhandisi Nyamhanga amesema serikali imepanga kufanya miradi mbalimbali ya kimaendeleo ikiwemo bomba la mafuta kutoka nchini Uganda kuja Tanzania hivyo amewataka kutumia fursa mbalimbali zilizopo ikiwemo kushiriki katika ufanyaji wa kazi za ukandarasi.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Makandarasi Tanzania CATA, Mhandisi Lawrence Esili Mwakyambiki amesema wanakumbana na changamoto mbalimbali ikiwemo kutokuwepo kwa miradi ya kutosha nchini lakini pia serikali kupenda kuwatumia makandarasi kutoka nje ya nchi.
Mkutano huo wa siku ya makandarasi umewajumuisha wakandarasi kutoka mikoa mbalimbali nchini ambao umeambatana na kauli mbiu imesayo wajibu wa makandarasi katika kuchangia uchumi wa viwanda.Chanzo kimoja kimeripoti.
Comments