Skip to main content

Rais Magufuli akiwa na Rais Museven Wazungumzia Uanzishwaji mahakama maalum kushughulikia ufisadi na udhibiti wa safari holela


Rais Magufuli akiwa na Rais Museven(picha na mtandao)
UANZISHWAJI wa mahakama maalum kushughulikia ufisadi na udhibiti wa safari holela kwenda nje ya nchi ni miongoni mwa maeneo yaliyotajwa na Rais John Magufuli kuwa ndiyo yanayoipa Tanzania mafanikio makubwa katika vita isiyokoma dhidi ya rushwa na ufisadi. 

Mambo mengine, ambayo hujengwa na dhamira ya dhati ya serikali katika kuondokana na tatizo hilo linalochukuliwa kwa uzito mkubwa kama ilivyo kwa mapambano dhidi ya ugonjwa wa kansa, ni pamoja na kuwaondoa watumishi hewa, kuwabaini na kuwaondoa watu wenye vyeti bandia ndani ya kada ya utumishi wa umma na pia kukomesha ‘dili’ za rushwa.
 

Rais Magufuli alitoa ufafanuzi huo nchini Uganda jana wakati alipoulizwa na waandishi wa habari mbele ya mwenyeji wake, Rais Yoweri Museveni, kuhusu siri ya mafanikio ya serikali yake katika vita dhidi ya rushwa na ufisadi.
 

Baada ya ufafanuzi huo ulioambatana na maelezo ya kina, Rais Museveni alionyesha kuvutiwa na yale yanayofanyika Tanzania na kuahidi kuiga mazuri hayo ili kuongeza kasi ya mapambano dhidi ya rushwa nchini kwake.
 

Rais Magufuli alitoa ‘darasa’ hilo kwa Waganda alipokuwa na mwenyeji wake katika Ikulu ndogo ya Masaka nchini Uganda ambako, Rais Magufuli alikuwa akiendelea na ziara yake ya kikazi ya siku tatu nchini humo.
 

Awali, mwandishi mmojawapo katika hafla hiyo alimuuliza Magufuli namna serikali yake ilivyofanikiwa katika vita dhidi ya rushwa na namna ambavyo anaweza kumshawishi mwenyeji wake, Rais Museveni, kuiga hatua alizochukua.
 

Katika ufafanuzi wake, Magufuli alisema rushwa bado ipo Tanzania licha ya kwamba hatua zimeanza kuchukuliwa na kuongeza kuwa serikali inayopiga vita rushwa ni lazima ionyeshe njia kwanza.
 

Akielezea zaidi, Rais Magufuli alisema alianzisha mahakama maalum kushughulikia mafisadi, pamoja na kufuta mianya ya rushwa ikiwamo mishahara hewa, kufuta safari holela za nje ya nchi ambazo zilikuwa nyingi kaisi kwamba baadhi ya vigogo walikuwa wakiishia uwanjani na wake zao kuwapelekea mabegi kabla hawajapanda ndege kusafiri tena, lakini sasa hilo halipo baada ya safari zote za lazima kuhitaji vibali maalumu kutoka kwake na kwa Katibu Mkuu Kiongozi.
 

Alisema hatua zote hizo, zikiwamo pia za udhibiti wa mianya ya rushwa katika maeneo mbalimbali, zimewezesha fedha kuokolewa na mwishowe kuelekezwa katika shughuli za maendeleo kwa ajili ya kuwanufaisha wananchi.
 

Akitoa mfano, Rais Magufuli alisema hata yeye amekuwa akikataa kusafiri nje ya nchi pasipokuwa na ulazima wa kufanya hivyo, pamoja pia na makamu wake wa rais na pia waziri mkuu na badala yake kuwatuma mawaziri, lengo likiwa ni kupunguza gharama kubwa za safari zinazotokana na ukubwa wa msafara wake, makamu na waziri mkuu.
 

“Kwenye mkutano wa Umoja wa Mataifa (UN) hivi karibuni, nilitakiwa mimi nihudhurie lakini nilimtuma Waziri wa Mambo ya Nje … na nilimsisitizia itakuwa safari ya watu watatu tu. 


Alikwenda na alituwakilisha vizuri sana,” alisema na kuongeza: 
Aidha, alisema watumishi hewa 20,000 walilipwa mshahara wa Sh. bilioni 238.7 kwa mwaka na kwamba fedha hizo zimeokolewa baada ya kuondolewa kwao.
 

Kuhusu vyeti feki, Rais Magufuli alisema zaidi ya watumishi 12,000 walilipwa bilioni 142 kwa mwaka, licha ya kutokuwa na sifa za elimu na kitaaluma na baadhi yao waliwekwa kwenye nyadhifa na nafasi mbalimbali za uongozi.
 

Kwa upande wake, Rais Museveni, alisema ameona matokeo mazuri ya serikali ya Tanzania baada ya kuanza kuchukua hatua za kupiga vita rushwa na kwamba tatizo kubwa Uganda ni kuwapo kwa urasimu ambao unasababisha rushwa.
chanzo:muungwana

Comments

Popular posts from this blog

MBINU ZA KUMFIKISHA MWANAMKE MWENYE MAKALIO MAKUBWA KILELENI KWA HARAKA

Kwa kawaida wanawake wanafikia kilele (mwisho wa utamu wa ngono) kati ya dakika ishirini na saa moja, yaani kwa kifupi inawachukua muda mrefu sana hali inayopelekea mpenzi mvivu kuchoka na ufanyaji wake utakuwa wa “ovyo” hali itakayo kufanya wewe kuishiwa na hamu ya kuendelea. Pamoja na kuchelewa huko ambako kunatokana na utofauti wetu kati ya mwanaume na mwanamke lakini nakumbuka hapo nyuma nilikutana na wanawake 2 waliokuwa ndani ya ndoa na wamezaa lakini hawajawahi kabisa kujua utamu wa tendo hilo alimaharufu kama “kufanya mapenzi”. Natambua kuwa ni ngumu au niseme si wanawake wote ambao wamejaaliwa kimaumbile kwamba wanafanikiwa kufika kileleni zaidi ya mara mbili kila wanapofanya mapenzi/ngono (kumbuka ni kati ya dakika 15 na saa moja hivyo Jibaba hapa awe na uwezo wa kujizuia kwa zaidi ya dk 45) na ikiwa jamaa ni “mzamiaji” basi unaweza ukaondoka na goli 3 ktk mzunguuko mmoja. Lakini kwa nini basi baadhi yao tu ndio wafike kileleni na wengine was...

Uganda Police issue fresh terror alert

  By Chris Kiwawulo, The Police have issued a fresh terror alert against a possible attack on Uganda by four terrorists from Kazakhstan. Police spokesperson Judith Nabakooba “We have received a security notification in form of an orange notice of four terrorists originating from Kazakhstan who are planning to travel to foreign countries in order to commit attacks and participate in hostile acts,” Police spokesperson Judith Nabakooba said in a statement on Monday. Nabakooba named the four active members of radical organizations as; Nassiruauly Kairat, Umurzakov Marat Eskendirovich, Kovtun Denis Valerevich and Mazhibayen Alimzhan Akhlazhanovich. By press time, a search on the international web has not yielded anything on the named persons.Last evening, police said that in collaboration with other security agencies vigilance has been stepped up to avert the terrorists’ evil plans. Police have in the past issu...

Poland’s GROM special services mastermind found dead

Brigadier General Slawomir Petelicki, responsible for the formation of the GROM special services unit in the 1990s, was found dead at his apartment, Saturday, with bullet wounds to the head. Sławomir Petelicki, 1946-2012. Photo: Archive/PAP/Radek Pietruszka Police spokesman Maciej Karczynski informed that Petelicki’s body was found by his wife in the garage of his Warsaw apartment on Saturday. He was 65. Primary investigations point to suicide as the cause of death. It is expected that prosecutors will decide on an investigation into Petelicki’s death on Monday. After examining the scene of the incident, “the body of General [Petelicki] has been taken to a forensic laboratory, although a post-mortem will probably take place on Monday,” prosecutor Katarzyna Calow-Jaszewska from the Warsaw District Prosecution told the PAP news agency. “He was a tough man, a brilliant soldier and commander,” Colonel Krzysztof Przepiorka, head of the ...