Mkurugenzi wa shughuli za kitakwimu kwa niaba ya mkurugenzi mkuu,ofisi ya Taifa ya Takwimu,Irenius Ruyobya akizungumza na wanahabari
Magrethy Katengu Dar es salaam |
Ofisi ya Taifa ya Takwimu ya Taifa leo imetoa taarifa imesema mfumo wa bei wa Taifa kwa mwezi Octoba,2017 umepungua hadi kufikia asilimia 5.1 ikilinganishwa na asilimia 5.3 ilivyokuwa mwezi septembaer 2017.
Mkurugenzi wa shughuli za kitakwimu kwa niaba ya mkurugenzi mkuu,ofisi ya Taifa ya Takwimu,Irenius Ruyobya ametoa taarifa hiyo leo wakati akizungumza na wanahabari jijini Dar es salaam ambapo amesema kupungua kwa mfumuko wa bei kumechangiwa hasa na kupungua bei za baadhi za vyakula kwa kipindi kilichoishia mwezi octoba,2017 zikilinganishwa na mwezi octoba 2016.
“baadhi ya bidhaa za chakula zilizochangia kupungua kwa mfumuko wa bei ni pamoja na Unga wa mtama kwa 2.6%,samaki kwa 7.1%,matunda kwa 2.7%,mbogamboga kwa 7.4%,maharage kwa asilimia 2.9,viazi kwa 14.4% na karaka kwa 7.8%”amesema Mkurugenzi Ruyobya
Kwa upande mwingine amesema mfumuko wa bei nchini una mwelekeo unaofanana na baadhi ya nchi nyingine za Afrika Mashariki ambapo Kenya mfumuko wa bei mwezi octoba 2017 umepungua 5.72% kutoka 7.06 mwezi septemba 2017,na Uganda umepungua kwa asilimia 4.8% mwezi octoba kutoka asilimia 5.3 mwezi septemba 2017.
Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) ni taasisi ya umma iliyoanzishwa kwa sheria ya Takwimu ya Mwaka 2015.Kwa mujibu wa sheria hiyo,NBS imepewa mamlaka ya kutoa,kusimamia na kuratibu upatikanaji wa Takwimu Rasmi nchini kwa ajili ya matumizi ya serikali na wadau wa takwimu.
Comments