Skip to main content

Posts

Showing posts from June, 2016

RAIS DKT. MAGUFULI AWAAPISHA WAKUU WA MIKOA WATATU IKULU JIJINI DAR

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Dkt. Binilith Satano Mahenge kuwa mkuu wa mkoa wa Ruvuma Ikulu jijini Dar es Salaam. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Dkt. Charles Mlingwa kuwa mkuu wa mkoa wa Mara Ikulu jijini Dar es Salaam. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Zainab Telack kuwa mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ikulu jijini Dar es Salaam. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Wakuu wapya wa Wilaya mara baada ya kuwaapisha wakuu wapya watatu wa Mkoa Ikulu jijini Dar es Salaam. Wengine katika picha ni Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan watatu kutoka kushoto, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa watatu kutoka kulia na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi wakwanza kushoto. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wakuu wa mikoa

OBEY CHIRWA AJIUNGA NA WENZAKE NCHINI UTURUKI

 Obey Chirwa tayati yupo nchini Uturuki Mshambuliaji mpya wa klabu ya Yanga Obey Chirwa, tayari yuko nchini Uturuki ambapo ameungana na kikosi cha Yanga kilichoweka kambi nchini humo kwa ajili ya mchezo wao wa kombe la shirikisho dhidi ya klabu ya TP Mazembe. Mzambia Obey Chirwa akiwa  na Mzimbabwe Thaban Kamusoko Chirwa ambaye ni raia wa Zambia amejiunga na Yanga akitokea FC Platinums ya Zimbabwe na ameanza mara moja mazoezi. Chirwa Atachukua nafasi ya Tambwe katika mechi dhidi ya TP Mazembe kwa kuwa mshambuliaji huyo raia wa Burundi ana kadi mbili za njano zitazomzuia kucheza mechi hiyo.   

MOISE KATUMBI AHUKUMIWA KWENDA JERA MIAKA 3

  .   Mgombea urais wa upinzani nchini Jamhuri ya Demokrasi ya Congo Moise Katumbi, amehukumiwa kifungo cha miaka 3 jela kwa kununua nyumba kinyume cha sheria kwenye mji ulio mashariki mwa nchi wa Lubumbashi. Pia alipigwa faini ya dola milioni 6. Katumbi ambaye pia ni mmiliki wa klabu ya TP Mazembe hakuwa mahakamani wakati wa kutolewa kwa hukumu hiyo, baada ya kusafiri kwenda afrika kusini kupata matibabu siku moja baada ya serikali kutangaza waranti wa kukamatwa kwake kwa mashtaka tofauti.   Analaumiwa kwa kuwaajiri mamluki wa kigeni ili kipanga njama dhidi ya serikali. BBC  wameandika Katumbi amekosoa hukumu hiyo, akisema kuwa ni jaribio la kutaka kuchelewesha kampeni yake ya kutaka kumrithi Rais Joseph Kabila mwezi Novemba.

Ufaransa yaimarisha ulinzi na usalama

Ufaransa imesema mtu mwenye itikadi kali aliewahi kutiwa hatiani huko nyuma, na ambaye alimuua afisa wa polisi na mke wake katika shambulizi la kisu alikuwa akitekeleza wito wa kiongozi wa Dola la Kiislamu, IS. Maafisa nchini Ufaransa wanasema kwamba mtu mwenye itikadi kali aliewahi kutiwa hatiani huko nyuma, na ambaye alimuua afisa wa polisi na mke wake katika shambulizi la kisu lililohamasisha na kundi la Dola la Kiislamu, alikuwa amebeba orodha ya walengwa mashuhuri wa mashambulizi, na kuwahimiza wafuasi kuyageuza mashindano ya Euro 2016 kuwa "makaburi." Shambulio la siku ya Jumatatu katika mji mdogo kaskazini magharibi mwa Paris ni la kwanza tangu kutokea kwa mashambulizi yaliyotekelezwa na IS mwezi Novemba na kuua watu 130. Kufuatia mashambulizi hayo ya kitongoji cha Magnanville, polisi wanasema maafisa wake sasa wat

Ufaransa yaimarisha ulinzi na usalama Thursday, 16 June 2016 Published in Jamii Read: 33 times Be the first to comment! Frankreich Attentat auf Polizist bei Paris / Polizisten sichern Tatort ab Ufaransa imesema mtu mwenye itikadi kali aliewahi kutiwa hatiani huko nyuma, na ambaye alimuua afisa wa polisi na mke wake katika shambulizi la kisu alikuwa akitekeleza wito wa kiongozi wa Dola la Kiislamu, IS. Maafisa nchini Ufaransa wanasema kwamba mtu mwenye itikadi kali aliewahi kutiwa hatiani huko nyuma, na ambaye alimuua afisa wa polisi na mke wake katika shambulizi la kisu lililohamasisha na kundi la Dola la Kiislamu, alikuwa amebeba orodha ya walengwa mashuhuri wa mashambulizi, na kuwahimiza wafuasi kuyageuza mashindano ya Euro 2016 kuwa "makaburi." Shambulio la siku ya Jumatatu katika mji mdogo kaskazini magharibi mwa Paris ni la kwanza tangu kutokea kwa mashambulizi yaliyotekelezwa na IS mwezi Novemba na kuua watu 130. Kufuatia mashambulizi hayo ya kitongoji cha Magnanville, polisi wanasema maafisa wake sasa watapaswa kubeba silaha wakati wakiwa nje ya majukumu ya kazi kwa ajili ya tahadhari inayoweza kujitokeza. Katika shambulio la usiku wa Jumatatu, mshambuliaji Larossi Abballa aliyekuwa akifuatiliwa baada ya kutumikia kwa muda na wanajihadi, aliwaua kwa kuwachoma kwa kisu kamanda wa polisi Jean-Baptiste na mke wake nje ya nyumba yao. Walengwa wa shambulio Mwendesha mashitaka wa Paris Francois Molins amesema kwamba Abballa anayetoka kitongoji cha jirani cha Monte-la-Jolie aliwaambia polisi kuwa "muuaji alisema kwamba yeye ni Muislamu na alikuwa akitimiza Ramadhan, alisema kuwa alikuwa amekula kiapo cha utii kwa kamanda wa IS Abu Bakr al-Baghdad wiki tatu zilizopita. Aliongeza kwa kusema alitekeleza wito wa kiongozi huyo na namnukuu,waue makafiri nyumbani kwao na familia zao." amesema Molins. Dola la Kiislamu IS limedai kuhusika na shambulio hilo la Jumatatu katika taarifa iliyorushwa na shirika la habari la Amaq ambalo hutoa matangazo ya kundi hilo mara kwa mara. Polisi wanasema kwamba waliokota orodha katika eneo la tukio yenye majina ya polisi na wageni mashuhuri wakiwemo waandishi na wasanii kama walengwa wa mashambulizi. Pia waligundua visu vitatu kimoja kikiwa katika lindi la damu. Tayari washirika watatu wa Abballa wamekamatwa wakihusishwa na shambulio hilo, mmoja wao aliwahi kutiwa hatiani mwaka 2013 kwa kujihusisha na mtandao wa kusajili wapiganaji wa jihadi nchini Pakistan. Ulinzi waimarishwa Wakati huo huo, polisi nchini Ufaransa wanazidi kuimarisha kikosi chao cha usalama kwa kupeleka askari zaidi kaskazini mwa nchi hiyo pamoja na kupanua marufuku ya pombe katika jitihada za kudhibiti vurugu zaidi kutokea katika mashindano ya soka barani Ulaya yanayoendelea nchini humo. Mamlaka bado zina wasiwasi na mashabiki wa Urusi na wale wa Uingereza, waakti ambapo Uingereza itacheza dhidi ya Wales siku ya alhamis wakati Urusi ikimenyana na Slovakia. Mjini Lille maduka yamelazimika kuacha kuuza pombe kwa saa zipatazo 60 kuanzia Jumanne hadi Ijumaa huku baa na migahawa ikitakiwa kufungwa usiku. Zaidi ya wafanyakazi 2500 wa usalama wakiwemo askari

 

YAMETIMIA… YANGA YAKINUKISHA SIMBA KINOMA NOMA *Unauliza au unasema? Wachanga fuba la hela, Manji kama kawa, Mama Fatma amaliza mapemaa, asiyependwa Wekundu wa Msimbazi karudi

Ratiba

Euro 2016 Kundi A P    W   D    L     GF GA GD Pts 1     Albania           0     0     0     0     0     0     0     0 2     Ufaransa          0     0     0     0     0     0     0     0 3     Romania          0     0     0     0     0     0     0     0 4     Uswisi             0     0     0     0     0     0     0     0 Kundi B P    W   D    L     GF GA GD Pts 1     England           0     0     0     0     0     0     0     0 2     Russia              0     0     0     0     0     0     0     0 3     Slovakia          0     0     0     0     0     0     0     0 4     Wales              0     0     0     0     0     0     0     0 Kundi C P    W   D    L     GF GA GD Pts 1     Ujerumani      0     0     0     0     0     0     0     0 2     Ireland Kaskaz 0     0     0     0     0     0     0     0 3     Poland            0     0     0     0     0     0     0     0 4     Ukraine           0     0     0     0     0     0