Yusuf Manji ameshinda nafasi ya uenyekiti wa Yanga kiulaini kutokana
na kutokuwa na mpinzani kwenye nafasi hiyo hivyo kupita bila kupingwa
kwenye nafasi ambayo alikuwa akiitetea.
Clemen Sanga nae amepenya katika nafasi ya Makamu Mwenyekiti kwa kumbwaga mpinzani wake Titus Osoro.
Shughuli pevu ilikuwa kwa wagombea nafasi ya ujumbe ambapo jumla ya wagombea 20 walikuwa wakiwania nafasi 8 za ujumbe.
Mwenyekiti
Yusuf Manji ameibuka mshindi wa nafasi ya uenyekiti akipenya bila
kupingwa na kupata idadi ya kura 1468 zilizopigwa na wanachama, huku
kura 2 pekee zikiwa zimeharibika.
Makamu Mwenyekiti
Clement Sanga amemgaragaza mpinzani wake baada ya kupata kura 1428 wakati mpinzani wake Titus Osoro akiambulia kura 80 pekee.
Wajumbe
Ayoub Nyenzi (889), Salim Mkemi (894), Bakar Malima (577), Godfrey
Mheluka (430), David Ruhago (582), Lameck Nyambaya (655), Sylvester
Haule (197), Pascal Laizer (178), Samwel Lukumay (818), Hashim Abdallah
(727), George Manyama (249), Hussein Nyika (770), Siza Lyimo (1027),
Beda Tindwa (452),Tobias Lingalangala (889), Athumani Kihamia (558),
Mchafu Chakoma (69), Edgar W Chibura (72), Ramadhani M. Kampira (182),
Omary S. Amei (1069)
Kwa Matokeo hayo, uongozi mpya wa Yanga uliochaguliwa na wanachama
unaundwa na Mwenyekiti Yusuf Manji, Makamu Mwenyekiti Clement Sanga huku
wajumbe wakiwa ni Omary S. Amei, Siza Lyimo, Salim Mkemi, Tobias
Lingalangala, Ayoub Nyenzi, Samwel Lukumay, Hussein Nyika na Hashim
Abdallah
Matukio katika namba:
23 ni idadi ya wagombea wote waliokuwa wakigombea
nafasi mbalimbali za uongozi kwenye klabu ya Yanga kuanzia nafasi ya
Mwenyeti, Makamu Mwenyekiti na Ujumbe.
20-hii ni idadadi ya wagombea wa nafasi ya ujumbe wa kamati ya utendaji ya Yanga
8-ni idadi ya nafasi za ujumbe ambazo zilikuwa zikiwaniwa na wagombea waliokuwa 20
2-ni idadi ya wagombea wa nafasi ya Makamu Mwenyekiti
1-nafasi ya Uenyekiti ilikuwa ikigombewa na mtu mmoja tu ambaye aligombea bila kupingwa
Comments