Skip to main content

Posts

Showing posts from December, 2013

BAADA YA KATIBU MKUU - MSEMAJI WA SIMBA NAE AACHIA NGAZI MSIMBAZI

BAADA YA KATIBU MKUU - MSEMAJI WA SIMBA NAE AACHIA NGAZI MSIMBAZI Inatoka http://www.shaffihdauda.com/

Jaji Ramadhani awa mchungaji Anglikana

Jaji Mkuu Mstaafu, Augustino Ramadhani ametawa zwa kuwa Mchungaji wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Zanzibar na kusema ameshangazwa na mashambulizi ya tindikali dhidi ya viongozi wa dini Visiwani humo. Akizungumza na waaandishi wa habari mara baada ya kutawazwa ndani ya Kanisa la Anglikana la Minara Miwili Mjini Unguja, Jaji Ramadhan amesema vitendo vya hujuma vinavyofanywa dhidi ya viongozi wa dini na Serikali ni kinyume na utamaduni wa Zanzibar. Alisema Wakristo na Waislamu Zanzibar kwa miaka mingi wamekuwa wakiishi kama ndugu bila ya kubaguana kwa sababu za itikadi ya dini licha ya Waislamu kuwa asilimia 95. Hata hivyo, alikumbusha kuwa wakristo wana mchango katika harakati za ukombozi wa Zanzibar, ambapo idadi kubwa ya waumini wake walianzisha Chama cha African Association mwaka 1935, ambapo rais wake wa kwanza alikuwa hayati,

Dk Ngasongwa: CCM inababaika

Ni kutokana na viongozi wake kusema hadharani bila ya kutumia vikao vya chama Dar es Salaam. Waziri wa zamani katika Serikali ya Awamu ya Tatu ya Rais Benjamin Mkapa na katika Awamu ya Nne ya Rais Jakaya Kikwete, Dk Juma Ngasongwa amesema kuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM), kinababaika katika kutekeleza majukumu yake. Soma zaidi...

President Kagame’s Christmas and New Year Message to the Rwanda Defence Forces and the Rwanda National Police

On behalf of the Government of Rwanda and on my own behalf and my family, I wish all of you officers, men and women of our Armed Forces and your families, a Happy Christmas and a prosperous New Year 2014. President Paul Kagame The ending year has been yet another time of distinguished service to the people of Rwanda and our Nation’s interests. Each of you servicemen and women effectively contributed, through your collective work, to delivering the peace and safety Rwandans, residents and foreign guests have continued to enjoy within our national borders. The people of Rwanda are grateful for your selfless service, sacrifices and continued commitment. The Government and leadership of Rwanda, at the various levels, commend you for successfully achieving your core mission; securing our homeland and deterring hostile activities against our nation. Your contribution to socio-economic activities through various initiatives such as ‘Army Week’ and Gender

WAIMBAJI WA MUZIKI WA INJILI TAMASHA LA KRISMAS WASUUZA MIOYO YA MASHABIKI UWANJA WA JAMHURI MOROGORO

Mwimbaji wa muziki wa injili Rose Muhando akiimba katika tamasha la Krismas lililofanyika leo kwenye uwanja wa Jamhuri Mjini Morogoro likishirikisha waimbaji mbalimbali wa muziki huo hapa nchini na mwimbaji wa kimataifa kutoka nchini Zambia Ephraim Sekereti wamesuuza mioyo ya mashabiki baada ya kushusha burudani ya nguvu katika tamasha hilo, Katika tamasha hilo, mashabiki wamejitokeza kwa wingi kwenye uwanja wa Jamhuri, Tamasha hilo linaandaliwa na Kampuni ya Msama Promotion ya jijini Dar es salaam na linatarajiwa kuendelea mkoani Tanga Desemba 28 mwaka huu.(PICHA NA KIKOSI KAZI CHA FULLSHANGWE-MOROGORO) Mwimbaji Edson Mwasabwite akifanya vitu vyake mbele ya mashabiki wake wakati akitumbuiza kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro leo jioni. Boniface Mwaiteje naye akawanyanyua kwenye viti mashabiki waliojitokeza kushuhudia tamasha hilo. Mwanamama mwenye sauti ya mirindimo Upendo Nkone akakonga nyoyo za m

Skylight Band yaporomosha burudani ya kukata na shoka X-MASS ndani ya kiota cha Escape One

Rapa wa Skylight Band Sony Masamba akimpagawisha shabiki wake. Mrs. Kisso akisebeneka na wifi yake Digna Mbepera.Inatoka kwa mdau.

Msanii Roma Mkatoliki Kujiunga na Chadema Wiki ijayo

    Msanii Roma Mkatoliki ---- Akiongea na Mabest zake Wa Mtaani huko Tanga amesema ana mpango Kuingia Kwenye Uringo wa Kisiasa ili apate nafasi Nzuri ya Kuikosoa Serikali baada ya Muziki wake Kupuuzwa na Viongozi wa Taifa hili. "Naplan Kuzamia Kwenye Mambo ya Politics hivi sasa, By the Way Wiki Ijayo naweza Kuchukua Kadi ya Chadema Rasmi"... Pia amesema Atahakikisha Wasanii Wenzake wanaoimba Muziki wa HipHop akina Kala Jeremiah nao Wanaunda timu ya Maangamizi Kuing'oa CCM Madarakani, ila aliwasihi sana Viongozi wa Chadema Kuwa Karibu nao pale Wanapozushiwa Shutuma za ajabu ajabu Kisa Wamejiunga na Chadema. Mpaka sasa baadhi ya wanamuziki wa Bongo Fleva waliojiunga na ambao wanampango wa kujiunga na Chama Cha kuwakomboa wanyonge CHADEMA ni Afande Sele wa Morogoro, Joseph Haule ambaye anajulikana kama Prof J, Soggy Doggy na Wengineo wengi. Ufuatao ni mmoja ya wimbo wa Roma Mkatoliki ujulikanao kama 2030.Inatokahttp://haki-hakingowi.blogspot.

MWENYEKITI WA WILAYA YA BUMBULI , CHADEMA , ABDI SHEKIMWAGA , ASIMAMISHWA

TAARIFA KWA UMMA KUKOMA/KUSIMAMISHWA KUWA KIONGOZI KWA MWENYEKITI WA WILAYA YA BUMBULI ndugu ABDI SHEKIMWAGA CHADEMA Kanda ya Kaskazini, inawatangazia umma wote kuwa, Ndugu ABDI SHEKIMWAGA amesimamishwa kuwa mwenyekiti wa CHADEMA jimbo la Bumbuli kuanzia 21 Desemba 2013. Ofisi ya kanda, ilipokea nakala ya taarifa na miniti ya kikao kilichoketi tarehe 22 septemba 2013 kutoka kamati tendaji ya wilaya/jimbo pamoja na nakala ya barua ya tuhuma alizoandikiwa ndugu ABDI SHEKIMWAGA ili ajieleze na kujibu, ikiwemo na barua ya tarehe 12 Desemba 2013 aliyoandikiwa katibu wa mkoa kujulishwa mapendekezo na hatua za kunusuru chama dhidi ya hila mbaya zilizokuwa zinafanywa na ABDI SHEKIMWAGA. Kwa bahati mbaya sana ndugu SHEKIMWAGA alitoa maneno ya kashfa na dharau pamoja na kutumia lugha isiyofaa kwa viongozi na kuamua kugoma kujibu barua ya tuhama hizo. Uongozi wa Kanda baada ya kupitia taarifa hizi na baada ya kufanya kikao cha pamoja na viongozi wa wilaya tarehe

BODABODA DAY: ASILIMIA 90 WAJIUNGA NA MPANGO WA UCHANGIAJI HIARI WA PSPF

 Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akikabidhi Zawadi kwa Afisa Uendeshaji wa PSPF, January Bunetta kwa kutoa Mchango mkubwa kwa Waendesha Bodaboda Mkoa wa Dar es Salaam. Zaidi ya asilimia 90 ya waendesha bodaboda waliohudhuria tamasha la siku ya waendesha bodaboda lililopewa jina la siku ya waendesha bodaboda wamejiunga na mpango wa uchangiaji wa hiari (PSS) wa mfuko wa Pensheni wa PSPF. Meneja wa Mpango wa Uchangiaji wa Hiari, Mwanjaa Sembe amesema udhamini wao katika tamasha hilo ni moja ya mikakati yake ya kuwafikia watu mbalimbali walio kwenye sekta isiyorasmi ili wajiunge na mpango wa uchangiaji wa hiari (PSS). Wakati tamasha hilo lililofanyika jumapili ya desemba 22 mwaka 2013 likiendelea waendesha bodaboda wengi walifurika kwenye banda la mfuko wa pensheni wa PSPF kujisajili na kujiunga na mpango wa hiari wa uchan

MTANI JEMBE YAINGIZA MIL 422/-

Mechi ya Nani Mtani Jembe kati ya Yanga na Simba iliyochezwa juzi (Desemba 21 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na Simba kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 imeingiza sh. 422,611,000. Mapato hayo ni kutokana na washabiki 52,589 waliokata tiketi kushuhudia mechi hiyo kwa viingilio vya sh. 5,000, sh. 7,000, sh. 10,000, sh. 15,000, sh. 20,000 na sh. 40,000. Kiingilio cha sh. 5,000 ndicho kilichovutia watazamaji wengi ambapo walikuwa 19,044. Asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa kutokana na mapato hayo ni sh. 64,466,084.75 wakati gharama za kuchapa tiketi ni sh. 7,488,000. Mgawo mwingine ilikuwa kama ifuatavyo; kila klabu imepata sh. 117,470,066.61, asilimia 15 ya uwanja ni sh. 52,598,537.29, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 35,065,691.53 wakati gharama za mchezo zilikuwa sh. 28,052,553.22. Soma zaidi...

SASA KUJARIBU TIKETI ZA ELEKTRONIKI

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeandaa mechi mbili za majaribio ya matumizi ya tiketi za elektroniki zitakazochezwa Uwanja wa Azam Chamazi, Dar es Salaam. Mechi ya kwanza itakuwa Desemba 26 mwaka huu saa 10 jioni ambapo itazikutanisha timu za Azam na Ruvu Shooting. Mechi nyingine itachezwa Januari Mosi mwakani kwa kuzikutanisha Ashanti United na JKT Ruvu. TFF tunatoa mwito kwa washabiki kujitokeza katika mechi hizo ambapo mbali ya kushuhudia burudani pia watajionea jinsi mfumo huo wa tiketi za elektroniki unavyofanya kazi. Kwa kushirikiana na benki ya CRDB ambayo ndiyo iliyoshinda tenda hiyo ya tiketi za elektroniki, TFF imepanga vilevile kuandaa mechi nyingine majaribio mikoani kabla ya mfumo huanza kutumika rasmi Januari 25 mwakani katika mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL). PINGAMIZI DIRISHA DOGO MWISHO DES 23 Desemba 23 mwaka huu ndiyo mwisho wa kipindi cha pingamizi kwa usajili wa dirisha dogo kwa klabu za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) na

MANJI AWAOMBA WANACHAMA WA YANGA WASIVUNJIKE MOYO

Mwenyekiti wa Yanga Bw.Yusuf Manji akiongea na waandishi wa habari makao makuu ya klabu, kushoto ni makamu mwenyekiti Clement Sanga Mwenyekiti wa klabu ya Young Africans Bw. Yusuf Manji amewaomba wanachama, wapenzi na washabiki wasivunjike moyo kwa matokeo ya jana ya mchezo wa kirafiki dhidi ya ya Simba SC, mechi iliyochezwa katika dimba la Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam. Akiongea na waandishi wa habari makao makuu ya klabu ya Yanga makutano ya mitaa wa Twiga/Jangwani Manji amesema anajua wanachama, na wapenzi wameumia sana hakuna aliyefurahishwa na matokeo ya kufungwa mabao 3-1 lakini isiwakatishe tamaa uongozi unafanyia kazi mapungufu yaliyojitokeza. Soma zaidi...

Uchambuzi Wa Habari: Ni Vidole Viwili Au Chadema Mbili?

Ndugu zangu, Nimemaliza kusoma hotuba ya Zitto Kabwe, Kigoma, jana. Na hata baada ya kumaliza, nimebaki na kitu ninachokiona; kuwa sasa kuna Chadema mbili mpaka pale wenye kuvutana ndani ya Chadema watakapotuhakikishia kwa vitendo kuwa kuna Chadema moja. Maana kwa kuyasoma haya ya Zito; "Mabadiliko ni kiu kikubwa cha Tanzania kwa sababu mabadiliko huleta matumaini. Na kiu hii ni kubwa zaidi kwetu sisi vijana wa kizazi hiki kipya. Siasa za kizazi kipya cha viongozi ni siasa za majawabu ya kero za wananchi. Siasa za mabadiliko ni siasa za kujenga na kuimarisha; ni siasa za kuaminiana na kuheshimiana hata pale mnapopingana kimawazo. Ninataka tujenge siasa mpya Tanzania;siasa za mabadiliko; siasa zinazojenga matumaini ya kweli;siasa zinazowajali na kuwajengea uwezo wananchi wa Tanzania." - Zitto Kabwe. Naam, Kwa kuyasoma hayo, sasa naziona ' C

Jokate Mwegelo azindua Kidoti Club

Baada ya kutamba na mitindo ya nywele na nguo aina ya Kidoti brand, msichana mwenye vipaji vingi hapa nchini, Jokate Mwegelo aimeanzisha klabu yake ijulikanayo kwa jina la Kidoti Club. Akizungumza katika uzinduzi wa klabu hiyo jana, Jokate alisema kuwa Kidoti Club ni tofauti na vilabu vingine kwani katika ujio wake huo mpya, atakuwa anajihusisha na mambo mbali mbali katika jamii husani masuala ya urembo na mitindo. Jokate pia alizindua aina mpya ya nywele zake za kisasa katika mtindo wa kidoti Brand. Jokate alisema kuwa kupitia klabu yake atakuwa anatoa ushauri mbali mbali katika jamii na ikiwa pamoja na taarifa za muziki, filamu, wasanii mbalimbali na nyinginezo kwa ajili ya rika tofauti. Alisema kuwa lengo lake kubwa ni kupanua mtandao wake kwa jamii na anaamini watu wengi watajiunga naye. Kwa mujibu wa Jokate ambaye ni Miss Tanzania namba mbili mwaka 2006, ili uwe mwanachama wa klabu hiyo, unatakiwa kutuma neno kidoti kwenda namba 15678 na kuanza kupata taarif

Mawaziri wanne wang’oka

Na Daniel Mjema na Sharon Sauwa Mwananchi Dar es Salaam / Dodoma. Ripoti ya Kamati ya Maliasili, Ardhi na Mazingira iliyowasilishwa jana asubuhi bungeni mjini Dodoma, imewang’oa madarakani mawaziri wanne ambao wizara zao zilishindwa kusimamia vizuri utekelezaji wa Operesheni Tokomeza Ujangili. Dk Emmanuel Nchimbi Kung’oka kwa mawaziri hao kulitangazwa bungeni jana usiku na Waziri Mkuu Mizengo Pinda aliyeeleza kuwa Rais Jakaya Kikwete ametengua uteuzi wao baada ya kuwasiliana naye kwa mashauriano akiwa nchini Marekani kwa matibabu. Mawaziri waliong’olewa kutokana na ripoti ya kamati hiyo iliyoongezewa shinikizo na michango ya wabunge wengi ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Khamisi Kagasheki, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Shamsi Vuai Nahodha na Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Dk Mathayo David Mathayo. Waziri wa kwanza kutangaza kujiuzulu alikuwa ni Kagasheki huku uamuzi wa

AZAM, SHOOTING TIKETI ZA ELEKTRONIKI

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeandaa mechi mbili za majaribio ya matumizi ya tiketi za elektroniki zitakazochezwa Uwanja wa Azam Chamazi, Dar es Salaam. Mechi ya kwanza itakuwa Desemba 26 mwaka huu saa 10 jioni ambapo itazikutanisha timu za Azam na Ruvu Shooting. Mechi nyingine itachezwa Januari Mosi mwakani kwa kuzikutanisha Ashanti United na JKT Ruvu. TFF tunatoa mwito kwa washabiki kujitokeza katika mechi hizo ambapo mbali ya kushuhudia burudani pia watajionea jinsi mfumo huo wa tiketi za elektroniki unavyofanya kazi. Kwa kushirikiana na benki ya CRDB ambayo ndiyo iliyoshinda tenda hiyo ya tiketi za elektroniki, TFF imepanga vilevile kuandaa mechi nyingine majaribio mikoani kabla ya mfumo huanza kutumika rasmi Januari 25 mwakani katika mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL). Soma zaidi...