Na Daniel Mjema na Sharon Sauwa Mwananchi
Dar es Salaam / Dodoma. Ripoti ya Kamati ya Maliasili, Ardhi na
Mazingira iliyowasilishwa jana asubuhi bungeni mjini Dodoma, imewang’oa
madarakani mawaziri wanne ambao wizara zao zilishindwa kusimamia vizuri
utekelezaji wa Operesheni Tokomeza Ujangili.
Dk Emmanuel Nchimbi
Kung’oka kwa mawaziri hao kulitangazwa bungeni jana usiku na Waziri Mkuu Mizengo Pinda aliyeeleza kuwa Rais Jakaya Kikwete ametengua uteuzi wao baada ya kuwasiliana naye kwa mashauriano akiwa nchini Marekani kwa matibabu.
Kung’oka kwa mawaziri hao kulitangazwa bungeni jana usiku na Waziri Mkuu Mizengo Pinda aliyeeleza kuwa Rais Jakaya Kikwete ametengua uteuzi wao baada ya kuwasiliana naye kwa mashauriano akiwa nchini Marekani kwa matibabu.
Mawaziri waliong’olewa kutokana na ripoti ya kamati hiyo iliyoongezewa
shinikizo na michango ya wabunge wengi ni Waziri wa Maliasili na Utalii,
Khamisi Kagasheki, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel
Nchimbi, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Shamsi Vuai Nahodha
na Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Dk Mathayo David Mathayo.
Waziri wa kwanza kutangaza kujiuzulu alikuwa ni Kagasheki huku uamuzi
wa mawaziri watatu kujiuzulu ukitangazwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.
Kagasheki alitangaza kujivua wadhifa huo sa 2:09 usiku alipokuwa
akichangia majumuisho ya ripoti ya kamati hiyo iliyowasilishwa na
mwenyekiti wa kamati hiyo James Lembeli ambaye ni Mbunge wa Kahama
(CCM).
Katika maelezo yake Kagasheki alisema: “…Mimi ni mtu mzima nimesikia
hisia nzito sana kwa waliyoyasema wabunge. Rais Kikwete aliponiteua
ilikuwa ni kwa furaha yake na operesheni hii, yaliyotokea yametokea hali
ya wanyama huko si nzuri;
Mimi mwenyewe nimewasikia na nachukua fursa hii kuteremka ngazi hii ya
uwaziri na nitachukua taratibu za kawaida kuijulisha sehemu
inayohusika(Rais).
Baada ya Kagasheki kutangaza hatua hiyo, Spika aliwaita mawaziri Dk
Nchimbi na Nahodha kuchangia hoja hiyo, hata hivyo hawakuwepo ndipo
alipoitwa Dk Mathayo na kutoa maelezo yake.
Comments