Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akikabidhi Zawadi kwa Afisa Uendeshaji wa PSPF, January Bunetta kwa kutoa Mchango mkubwa kwa Waendesha Bodaboda Mkoa wa Dar es Salaam.
Zaidi ya asilimia 90 ya waendesha bodaboda waliohudhuria tamasha la siku ya waendesha bodaboda lililopewa jina la siku ya waendesha bodaboda wamejiunga na mpango wa uchangiaji wa hiari (PSS) wa mfuko wa Pensheni wa PSPF.
Meneja wa Mpango wa Uchangiaji wa Hiari, Mwanjaa Sembe amesema udhamini wao katika tamasha hilo ni moja ya mikakati yake ya kuwafikia watu mbalimbali walio kwenye sekta isiyorasmi ili wajiunge na mpango wa uchangiaji wa hiari (PSS).
Wakati tamasha hilo lililofanyika jumapili ya desemba 22 mwaka 2013 likiendelea waendesha bodaboda wengi walifurika kwenye banda la mfuko wa pensheni wa PSPF kujisajili na kujiunga na mpango wa hiari wa uchangiaji PSS.
Comments