Skip to main content

Posts

Showing posts from June, 2018

Michuano ya Kombe la Dunia nchi URUSI

 Uwanja huu  ulichukua idadi ya washabiki kama inavyosomeka kwenye ule ubao.  Kwa sasa mashabiki wa soka duniani wanaendelea kupata furaha tele kwa kuangalia mitanange ya kombe hilo .

TAKUKURU Mkoa wa Kinondoni yazungumza

TAASISI ya kuzuia na kupambana na Rushwa Mkoa wa Kinondoni  (TAKUKURU) imesema  kwa kipindi cha miezi(12) cha kuanzia  Julai hadi Juni 2018 imeweza kutekeleza malengo yake ya  utendaji  kazi kama yalivyoainishwa kwenye Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Na 11 ya mwaka 2007. TAKUKURU Mkoa wa Kinondoni kuanzia mwezi Julai,2017 hadi Juni, 2018 iliweza kutekeleza majukumu yake kwa kupokea taarifa mpya kufungua kesi mpya kuendesha kesi zilizokuwa zimeshafunguliwa,  kufungua majalada mapya ya uchunguzi na kuendelea na uchunguzi  wa majalada ya zamani. Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam  juu ya  taarifa hiyo  Naibu Mkuu wa Takukuru(M)Eugenius Hazinamwisho alisema kuwa mafanikio hayo ya utekelezaji wa jukumu la  kuchunguza taarifa za vitendo vya rushwa yametokana na  mwitikio mzuri wa jamii katika kutoa taarifa na utayari wa  kuipa TAKUKURU ushirikiano. "Taarifa 376 zimepokelwa  kutoka  kwa wadau ambao ni vyombo vya habari,vyom

KIGWANGALLA AFUNGUA WARSHA YA KITAIFA YA WADAU WANAOPINGA VITENDO VYA UHALIFU DHIDI WANYAMAPORI NA MISITU NCHINI

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akifungua warsha ya siku moja ya wadau wa kitaifa wa kupinga vitendo vya uhalifu dhidi ya wanyamapori na misitu nchini jijini Dodoma leo Juni 26, 2018. Warsha hiyo imelenga kujadili na kuainisha mahitaji na vipaombele vya sekta ya mahakama na mashtaka ya kudhibiti uhalifu huo.  Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla, Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Dk. Iddi Mfunda (wa pili kushoto), Mkurugenzi wa Mashtaka, Biswalo Mganga (wa pili kulia) na Mkuu wa ofisi wa Shirika la Ufuatiliaji wa Wanyamapori (TRAFFIC), Julie Thomson (kulia) wakiimba wimbo wa Taifa wakati wa warsha ya siku moja ya wadau wanaopinga vitendo vya uhalifu dhidi ya wanyamapori na misitu nchini jijini Dodoma leo Juni 26, 2018.  Baadhi ya wadau wa kitaifa walioshiriki hafla hiyo wakiimba wimbo wa Taifa. Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akifungua warsha ya siku moja ya wadau wa kitaifa wa kupi

Kakunda:Zipoidara nyingi ambazo zinaweza kuwasaidia vijana

Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Joseph Kakunda imesema kuwa zipo idara nyingi ambazo zinaweza kuwasaidia vijana kujikwamua ili kuendeleza biashara kama kujiunga katika idara ya vijana kwenye Halmashauri. Kauli hiyo imetolewa na Kakunda leo, Bungeni wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum (CCM)Zainab Katimba, aliyehoji “Kwa kuwa jitihada za kutoa mitaji kwa vijana na wanawake inabidi ziende sambamba na kuwajengea uwezo wa kuanzisha na kuendeleza biashara, Je serikali ina mkakati gani wa kuwatumia hawa maafisa Biashara katika kuwajengea uwezo vijana wanaokuwa katika vikundi ambao wananufaika na asilimia 10 inayotengwa kutoka kwenye mapato ya ndani ya Halmashauri? “Nataka nikuhakikishie kwamba vijana katika nchi hii wana idara nyingi sana za kuweza kuwasaidia mawazo ya kujikwamua kutoka pale walipo kutoka kwenda mbele, kuna idara ya vijana katika Halmashauri kuna idara katika maendeleo ya jamii, kuna idara ya mipango sasa Maafisa B

Usafiri Mgumu Dar kubaki historia

Changamoto za usafiri nchini Tanzania hususani katika majiji  makubwa zipombioni kupunguzwa ama kumalizika.  Hayo yamebainishwa jana  na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Poul Makonda kwa niaba ya Makamu wa Rais Samia Suluhu Hasssani katika mkutano na wadau wa usafiri kutoka nchini zaidi ya 36 duniani ambao wako hapa nchini kujadili namna sahihi ya kumaliza changamoto za usafiri nchini Tanzania utakao fanyika kwa siku tatu kuanzia leo jijini humo.   Alisema hawa ni wataalam walioboba katika masuala ya usafiri ambao wameichagua Tanzania kuwa mwenyeji wao baada ya Tanzania kupata tuzo ya kwanza katika utoaji wa huduma bora ya usafiri barani Afrika baada ya kuanzisha usafiri wa mabasi yaendayo kasi (UDART)ambayo kwa kiasi kikubwa yamepunguza msongamano wa magari katikati ya jiji la Dar es Salaam na kero ambazo miaka mitano iliyopita zilikuwa tishio.   "Moja ya changamoto za usafiri sio tu kumiliki gari au chombo cha usafiri tatizo lipo pale ambapo

Kesi ya Mbowe yasogezwa mbele

  Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo imeahirisha kesi inayowakabili Viongozi wa Chama cha Demokarsia na Maendeleo (Chadema) akiwemo Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe  hadi June 27 mwaka huu kwa sababu Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Vincent Mashinji kutofika mahakamani hapo. Hatua hiyo imefikiwa mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu,  Wilbard Mashauri  baada  wakili wa serikali,  Faraja Nchimbi  kueleza kuwa kesi hiyo imeitishwa ili washtakiwa wasomewe maelezo ya awali lakini mshtakiwa wa sita,  Dkt. Mashinji  hayupo mahakamani. Kwa upande wa Wakili wa utetezi,  Peter Kibatala  amedai kuwa  Dk. Mashinji  ana udhuru yupo katika mahakama ya Songea ana kesi nyingine, hivyo wanaomba ahirisho. Maombi hayo ya ahirisho yaliibua mvutano wa kisheria baada ya wakili wa serikali Paul Kadushi kutaka kesi iahirishwe hadi kesho, huku wakili Kibatala akitaka iahirishwe hadi tarehe nyingine. Kutokana na mvutano huo, Hakimu Mashauri ameahirisha kesi hiyo hadi June 27, mwaka huu. Mbal

Wasafiri wanne kutoka Kenya walishukiwa kuwa na maambukizi ya vimelea vya ugonjwa wa homa ya Chikungunya

  WIZARA ya Afya Maendeleo ya Jamii jinsia wazee na watoto imesema kuwa Jumla ya wagonjwa 226 wa homa ya Dengue pamoja na wagonjwa nne wa homa ya Chikungunya wameripotiwa kuugua magonjwa hayo kwenye mikoa ya Dar es Salaam na Tanga. Hayo yamesemwa Dar es Salaam leo na Waziri mwenye dhamana hiyo Ummy Mwalimu wakati akitolea taarifa kuhusiana na magonjwa hayo yanayoshabihia na homa ya Chikungunya pamoja na Gengu. Alisema mnamo Juni 26 mwaka huu wasafiri wanne kutokea Mombasa nchini Kenya walishukiwa kuwa na maambukizi ya vimelea vya ugonjwa wa homa ya Chikungunya Waziri Ummy ameongeza kuwa mpaka kufika july mosi mwaka huu watakuwa na vituo maalum vya kufuatilia magonjwa hayo ikiwemo kudhibiti mazalia ya mmbu. "Niwajibu wa kila mtoa huduma za afya kutoa taarifa hasa hospitali binafsi ambako changa kubwa imekuwa ni kushindwa kupata taarifakuhusu ugonjwa huo,"amesema . Amesema ugonjwa wa Ebora pia bado haujaingia rasmi katika nchini hila tumejipanga kukabiliana nao hiwapo utain

Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji Profesa Kitila amezitaka Asasi zisizo za Kiserikali kuchangia katika uwekezaji

KATIBU MKUU Wizara ya Maji na Umwagiliaji Profesa Kitila Mkumbo ,ameyataka Mashirika ya maendeleo ya kimataifa,Taasis binafsi na Asasi zisizo za Kiserikali kuchangia katika uwekezaji wa miradi ya maji nchini. Prof Mkumbo aliyasema hayo jana katika hoteli ya New Africa wakati wa majadiliano baina ya wadau wa sekta binafsi na Wizara ya Maji ,nakusema kuwa Serikali peke yake haiwezi kutatua kero ya maji nchini nakuyataka mashirika hayo kuunga mkono jitihada za serikali. “Serikali inatekeleza maendeleo ya sekta ya maji kwakushirikisha halmashauri zote nchini, katika vipaumbele vya miaka mitano ambapo sekta ya maji ni miongoni mwao na ni sekta ambayo hupata pesa nyingi. Alisema  zipo jitihada    nyingi zinazofanywa na serikali katika kuhakikisha tatizo la maji linakwisha nakufikia malengo   ya Dunia namba sita lakini pia serikali ina malengo ya miaka mitano ambapo hadi sasa 58%-60 ya watu wa vijijini wanapata maji safi na salama. Aidha Prof Mkumbo alisema kuwa sekta ya m

Ndemla akubali kusaini mkataba mpya Simba

BAADA ya mvutano na majadiliano ya hapa na pale, hatimaye kiungo wa Simba, Said Ndemla amekubali kusaini mkataba mpya wa kuendelea kuwatumikia mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba ya jijini Dar es Salaam. Wiki iliyopita, Ndemla aliwagomea Simba kusaini mkataba baada ya kuwekewa mezani kiasi cha Sh. milioni 50. Kiungo huyo ambaye alipandishwa kutoka timu ya vijana ya umri chini ya miaka 20 (Simba B), alihusishwa na mipango ya kujiunga na Yanga na alikiri kufanya mazungumzo na mabingwa hao wa zamani wa Ligi Kuu Bara. Taarifa kutoka ndani ya klabu  zimesema kuwa Ndemla alikutana na mwekezaji na mfanyabiashara maarufu nchini, Mohammed Dewji 'Mo' na kupewa kiasi ambacho alikihitaji na aliona ndio kinafanana na thamani yake. "Tayari Ndemla ameshamalizana na Mo, sasa roho yangu imetulia, maana nilikuwa kila wakati namshauri awe na subira na asifanye uamuzi wa haraka, yeye ni mtoto wa Simba na anastahili kuendelea kubakia hapo," alisema

Baa ya miongo kadhaa Wanawake Saudi Arabia rasmi sasa kukaa kwenye usukani

Wanawake nchni Saudi Arabia rasmi sasa wameruhusiwa kukaa kwenye usukani, baa ya miongo kadhaa kutopata ruhusa hiyo Mabadiliko haya yalitangazwa mwezi Septemba mwaka jana na Saudi Arabia ikatoa leseni za kwanza kwa wanawake mwanzoni mwa mwezi huu. Ilikuwa nchi pekee iliyobaki duniani ambapo wanawake walikuwa hawaendeshi magari na familia zao zilikuwa zinakodisha dereva kwa ajili ya wanawake. Hata hivyo, hatua hii imefikiwa wakati kukiwa na Kampeni ya kuwakamata wanaharakati ambao wamekuwa wakipaza sauti wapatiwe haki ya kuendesha magari. Takriban wanaharakati wa haki za wanawake wanane wanashikiliwa na huenda wakafikishwa mahakamani na kupatiwa kifungo kwa uanaharakati wao, Shirika la kutetea haki za binaadamu, Amnesty International limeeleza. Miongoni mwa wanaoshikiliwa ni pamoja na Loujain al-Hathloul, mwanaharakati kinara katika kampeni hiyo. Amnesty pia imetaka kufanyiwa mabadiliko makubwa nchini Saudi Arabia, ambapo wanawake bado wameendelea kukandamizwa

Rais Mnangagwa anusurika kifo

Jana Juni 23, 2018  jioni Rais wa Zimbabwe, Emmerson Mnangagwa amenusurika kifo baada ya mlipuko mkubwa kutokea kwenye jukwaa mjini Bulawayo alikokuwa akijinadi kwenye kampeni za uchaguzi mkuu nchini humo. Mnangagwa ambaye aliongozana na mke wake pamoja na makamu wake wa Rais, Kembo Mohadi  wote wameumia miguuni na tayari wamepelekwa hospitalini kwa matibabu zaidi. Kwa mujibu wa gazeti la serikali la The Herald limeeleza kuwa mlipuko huo ni jaribio la kutaka kumuua Rais Mnangagwa ambaye toka aingie madarakani mwaka jana baada ya kumpindua aliyekuwa Rais wa taifa hilo, Robert Mugabe  amekuwa akipokea vitisho. Shirika la Taifa la Utangazaji nchini Zimbabwe (ZBC) pia limeripoti kuwa mwenyekiti wa kitaifa wa Zanu PF Oppah Muchinguri-Kashiri, na Afisa mkuu wa kisiasa Engelbert Rugeje pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa ZBC walijeruhiwa Kufuatia tukio hilo Mnangagwa amesema kuwa jaribio hilo lilipangwa na watu wenye nia mbaya juu yake ila siku zake hazikutimia. “Nawapa

Asilimia 65 ya watanzania wote hawana uelewa juu ya huduma za bima na wengine hawajui bima ni nini

WANAFUNZI wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha nchini kilichopo jijini Dar es Salaam (IFM) kimefanya maandamano ya hamasa juu ya kada mbalimbali kuelewa zaidi umuhimu wa wananchi kuwa na bima. Maandamano hayo yenyelengo la kuongeza uelewa wa wananchi juu ya utumiaji wa huduma za bima yaliyopewa kaulimbiu ya "BILA BIMA HAUNA SALAMA YA KUTOSHA" yalianzia katikati ya mitaa ya Jiji na kuhitimishwa katika ukumbi wa Karimjee jijini hapa. Katika maandamano hayo hamasa kwa wananchi ilitolewa na chama cha madalali wa BIMA tanzania TIBA juu ya huduma za bima nchini  imeelezwa kuwa mwitikio bado ni mdogo .    Hali hiyo imethibitishwa na wadau wa bima katika maandamano yaliyoratibiwa na chuo hicho cha IFM  kwa hisana  ya TIBA yaliyojumuisha wadau wa bima na wanafunzi wote wa masomo ya bima kutoka chuoni hapo na wakuu wao wa idara ya bima. Wadau mbali mbali walioshiriki katika maandamano hayo kwa lengo la kuongeza mwamko wa kutumia bima za aina mbali mbali kat

HOSPITALI MLOGANZILA WAJIANDAA KUTIBU SELIMUNDU KWA KUPANDIKIZA UTE WA MIFUPA

MKUU wa Idara ya Hematolojia, Uwekaji wa Damu na Mtafiti Mkuu wa Program ya Selimundu katika Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili(MUHAS) Profesa Jullie Makani amesema wapo katika mchakato wa kutoa huduma ya kutibu Selimundu kwa Kupandikiza ute wa Mifupa Prof.Makani amesema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Selimundu Duniani yaliyofanyika katika Hospitali ya Mlaganzila ambapo amesema kwa sasa wapo katika mchakato wa mazungumzo na yakikamilika wanatarajia kuanza kutibu Selimundu kwa kutumia tiba ya Kupandikiza Ute wa mifupa kwa mgonjwa. "Zipo njia mbili zinazotumika kutibu Selimundu.Njia ya kwanza ni kwa kutumia Hydroxyurea na ndio ambayo tunaitumia hapa nchini.Njia ya pili ni ya kutibu kwa kupandikiza ute wa mifupa ambayo kitalaam inafahamika Bone Marrow Transplant,"amefafanua. Alipoulizwa ni lini wataanza kupandikiza ute wa mifupa kwa mgonjwa wa Selimundu katika hospitali hiyo amejibu wanatarajia kuanza mwakani

Tanesco Manyara limewatahadharisha wakazi wanaoendelea kufanya shughuli za kibinadamu karibu na miundombinu ya shirika hilo

Maneja wa Tanesco mkoa wa Manyara Gerson Manase akiongea na waandishi wa habari hawapo kwenye picha hivi karibuni katika kampeni ya kuhamasisha wananchi kuacha kufanya shughuli za kibinadamu karibu na miundombinu ya shirika hilo.   Na Mwandishi Wetu, Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) Mkoa wa Manyara limewatahadharisha wakazi wanaoendelea kufanya shughuli za kibinadamu karibu na miundombinu ya shirika hilo na kusema kuwa hatua kali zitachukuliwa dhidi yao. Tahadhari hiyo imetolewa na meneja wa Tanesco mkoa huo hivi karibuni, Gerson Manase kupitia kampeni maalumu inayofanywa na Tanesco makao makuu ikiwa na lengo la kuhamasisha juu ya athari za kuhujumu miundombinu ya shirika na kufanya shughuli karibu. “Kuanzia sasa mkazi yoyote atakaye kiuka sheria na kufanya shughuli za kibinadamu karibu na miundombinu ya umeme, tutafyeka mazao yake yote na hatua nyingine za kisheria zitafuata,” alisema meneja huyo Kwa sasa Tanesco Manyara inahudumia wilaya tatu ikiwemo Babati, Mb

WANACHAMA YANGA WAMREJESHA MANJI, TARIMBA,KIKWETE WAPEWA JUKUMU LA KUSAJILI WACHEZAJI WAPYA YANGA

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM WANACHAMA wa klabu ya Yanga kwa kauli moja wamekubaliana kumrejesha madarakani, Mwenyekiti wao Yussuf Mehboob Manji katika mkutano Mkuu wa mwaka uliofanyika Bwalo la Maafisa wa Jeshi la Polisi, Oysterbay, Dar es Salaam leo. Pamoja na kumrejesha Maji aliyejiuzulu Mei mwaka jana, wanachama hao wameunda Kamati ya watu tisa chini ya Rais wa zamani wa klabu, Tarimba Abbas kusimamia usajili na mambo mengine muhimu ya klabu kwa sasa. Akizungumza na Waandishi wa Habari baada ya mkutano huo, Kaimu Katibu Mkuu, Charles Boniface Mkwasa amesema kwamba agizo la Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harison Mwakyembe kufanyika kwa uchaguzi wa kuziba nafasi za viongozi waliojiuzulu ndani ya miezi miwili pia linafanyiwa kazi. Mkwasa pia amesema kwamba wameridhia mwongozo wa mabadiliko ya uendeshwaji wa klabu kwa kuingia kwenye soko la hisa na kwamba mchakato wa zoezi hilo unashughulikiwa na Wakili maarufu, Alex Mgongolwa.  Mapema a