Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji Profesa Kitila amezitaka Asasi zisizo za Kiserikali kuchangia katika uwekezaji
KATIBU MKUU Wizara ya Maji na Umwagiliaji Profesa Kitila
Mkumbo ,ameyataka Mashirika ya maendeleo ya kimataifa,Taasis binafsi na Asasi
zisizo za Kiserikali kuchangia katika uwekezaji wa miradi ya maji nchini.
Prof Mkumbo aliyasema hayo jana katika hoteli ya New Africa
wakati wa majadiliano baina ya wadau wa sekta binafsi na Wizara ya Maji ,nakusema
kuwa Serikali peke yake haiwezi kutatua kero ya maji nchini nakuyataka
mashirika hayo kuunga mkono jitihada za serikali.
“Serikali inatekeleza maendeleo ya sekta ya maji
kwakushirikisha halmashauri zote nchini, katika vipaumbele vya miaka mitano
ambapo sekta ya maji ni miongoni mwao na ni sekta ambayo hupata pesa
nyingi.
Alisema zipo jitihada nyingi zinazofanywa na serikali katika
kuhakikisha tatizo la maji linakwisha nakufikia malengo ya Dunia namba sita lakini pia serikali ina
malengo ya miaka mitano ambapo hadi sasa 58%-60 ya watu wa vijijini wanapata
maji safi na salama.
Aidha Prof Mkumbo alisema kuwa sekta ya maji inawekeza katika
matumizi yake katika maeneo makuu matatu yakiwemo umwagiliaji, majumbani, na
umeme.
“Tumekutana na wenzetu hawa wadau wa maji nakuwataka wawekeze
katika ushiriki wa viwanda kwakuwa maji
yapo yakutosha, kikubwa ni teknolojia na fedha kwa ajili ya kuvuna maji hayo na
serikali pekee haiwezi."Alisema.
Naye Ofisa Mkuu Mtendaji wa mfuko wa UTT alisema kuwa
serikali imewekeza vya kutosha katika sekta ya maji lakini mahitaji katika
sekta hiyo ni makubwa hivyo sekta binafsi haina budi kuunga mkono serikali
katika jitihada za kutatua tatizo la maji.
“Sekta binafsi inatakiwa nayo kufanya kwa nafasi yake kusaidia
nakuna haja ya kushirikiana na halimashauri na watekelezaji wa miradi ya maji
kwakuwapatia vitendea kazi mbalimbali.Alisema.
Hata hivyo Washima alisema kuwa wao kama UTT wamekuwa wakichangia
miradi mbalimbali ya maji nchini inayotekelezwa katika halmashauri mbalimbali.
Comments