Wasafiri wanne kutoka Kenya walishukiwa kuwa na maambukizi ya vimelea vya ugonjwa wa homa ya Chikungunya
WIZARA ya Afya Maendeleo ya Jamii jinsia wazee na watoto imesema
kuwa Jumla ya wagonjwa 226 wa homa ya Dengue pamoja na
wagonjwa nne wa homa ya Chikungunya wameripotiwa kuugua magonjwa
hayo kwenye mikoa ya Dar es Salaam na Tanga.
Hayo yamesemwa Dar es Salaam leo na Waziri mwenye dhamana hiyo Ummy
Mwalimu wakati akitolea taarifa kuhusiana na magonjwa hayo yanayoshabihia
na homa ya Chikungunya pamoja na Gengu.
Alisema mnamo Juni 26 mwaka huu wasafiri wanne kutokea Mombasa nchini
Kenya walishukiwa kuwa na maambukizi ya vimelea vya ugonjwa
wa homa ya Chikungunya Waziri Ummy ameongeza kuwa mpaka kufika july mosi
mwaka huu watakuwa na vituo maalum vya kufuatilia magonjwa hayo ikiwemo
kudhibiti mazalia ya mmbu.
"Niwajibu wa kila mtoa huduma za afya kutoa taarifa hasa hospitali
binafsi ambako changa kubwa imekuwa ni kushindwa kupata taarifakuhusu
ugonjwa huo,"amesema .
Amesema ugonjwa wa Ebora pia bado haujaingia rasmi katika nchini
hila tumejipanga kukabiliana nao hiwapo utaingia nchini .
Wakati huo huo Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Dk Mpoki Ulisubisya amesema
mbali na mikoa hiyo miliwi ambayo imebainika kuwa na wagonjwa wa magonjwa
hayo pia mikoa iliyopo kwenye hatari ya kupata ugonjwa huo ni pamoja na
Tanga, Kilimanjaro na Pwani.
Katika hatua nyingine Waziri ametoa taarifa kuhusu ugonjwa wa ebola kuwa
mpaka sasa jumla ya watu 61 nchini Congo wameugua ugonjwa wa Ebola, huku
akisisitiza kuwa ugonjwa huo bado haujaingia nchini ambapo pia naye
Mkurugenzi mkaazi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Dk Adiele Onyeze
ametolea ufafanuzi kuhusiana na ugonjwa huo.
Hata hivyo Waziri Ummy amesisitiza kuwa ni wajibu wa kila mtoa huduma
za afya kutoa kuhusiana na wagonjwa ambao wamekuwa wakifika kwenye vituo
vyao vya afya ili kuweza kukabiliana na magonjwa ya milipuko yanapojitokeza
Comments