MANCHESTER UNITED imebisha hodi Sevilla kutaka saini ya beki wao wa kati Clement Lenglet mwenye umri wa miaka 22.
Sentahafu huyo raia wa Ufaransa, anachukuliwa kama mmoja wa mabeki bora vijana barani Ulaya na sasa United inataka kumnyakua kiangazi hiki.
Licha ya kuruhusu goli moja tu zaidi kulinganisha na wapinzani wao Manchester City msimu uliopita, Mourinho bado anataka kuongeza sentahafu mwingini Old Trafford.
Kwenye upande wa beki ya kati, United inao Chris Smalling, Phil Jones, Eric Bailly, Victor Lindelof na Marcos Rojo, lakini kocha Jose Mourinho hajaridhika na umadhubuti wa safu yake ya ulinzi.
Comments