HIFADHI ya Ngorongoro pamoja na Hifadhi ya Taifa ya Serengeti ni moja ya
maajabu mapya nane ya Dinia,Mwaka 2010,kamati ya masuala ya Urithi wa Dunia
ilitaja kuwa Hifadhi ya Norongoro kuwa Eneo la Utamaduni la urithi wa Dunia.
Afisa Uhusiano wa Hifadhi ya Ngorongoro Nickson Nyange wakati akizungumza na kuhusiana na maonyesho ya wiki ya mazingira
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi Dar es Salaam katika viwanja vya mnazi mmoja
katika muendelezo wa maonyesho ya wiki ya mazingira Afisa Uhusiano idara ya
ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro Nickson Nyange aliwataka Watanzania kujiwekea
mazoea ya kutembelea hifadhi mbalimbali za Taifa zilizopo hapa nchini
ikiwemo Hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro.
Alisema Tanzania imebarikiwa na Mungu kwa kuwa na vivutio vingi
ambavyo vimesheheni maajabu lakini pia wanyama pori wa aina tofauti
tofauti hivyo ni vyema wananchi wanaonyesha muamko wakwenda kutalii.
“Tumekuja kwenye viwanja nvya mnazi mmoja kwa lengo la kuwapatia elimu watanzania
namna ambavyo wanapaswa kutembelea mbuga zetu za wanyama ili kushuhudia uumbaji
wa Mungu”alisema Nyange
Katika suala la utunzaji wa mazingira alisema wanashiriki kwenye kampeni ya
kuhakikisha wanayatunza na kuyahifadhi mazingiza ya hifadhi ikiwa ni pamoja
na upandaji wa miti ili kuacha mazingira mazuri kwa vizazi vijanvyo.
Inaelezwa kuwa Hifazi ya Ngorongoro inasimamiwa na Mamlaka ya Hifadhi ya
Ngorongoro ambayo kisheria inatekeleza majukumu yake makuu kama kuifadhi
maliasili zilizo ndani ya Eneona pili inasimamia kukuza na kuendeleza
utalii katika eneo la Hifadhi ya Ngorongoro.
“Miti mikubwa ambayo munaiona sasa hivi haikuoteshwa jana wala juzi wala mwaka
jana bali ilioteshwa miaka mingi iliyopita hivyo tunapaswa kuyatunza na kuyahifadhi
mazingira.”alimaliziea kusema Nyange.
Ngorongoro ni eneo la kasoko kubwa nchini Tanzania, lenye umbali wa takriban
kilomita180 kutoka Arusha; pia ni hifadhi ya taifa inayojulikana kote duniani
ambapo inasemekana Kuna jumla ya wanyamapori wakubwa takriban 25,000, wakiwa
pamoja na vifaru, viboko, nyumbu, pundamilia, nyati, simba, fisi na chui.
Comments