Rais wa Uganda Yoweri Museveni ametangaza siku tatu za maombolezi ya
kitaifa, kufuatia vifo vya watu 22 baada ya ajali ya barabarani katika
Wilaya ya Kiryandongo ijumaa ya wiki iliyopita.
Bendera zote nchini humo zinapepea nusu mlingoti kwa heshima ya watu
hao. Ajali hiyo ilihusisha basi la abiria na Lori la mizigo.
Aidha, serikali itatoa Shilingi za nchi hiyo Milioni 5 kwa kila Familia kuisadia katika shughuli za mazishi.
Takriban watu 22 wakiwemo watoto watatu waliuwa kwenye ajali ya basi
lililogonga tingatinga ambayo ilikuwa ikiendeshwa bila ya taa usiku kwa
mujibu wa msemaji wa polisi Emilian Kayima ambaye aliongea na shirika la
habari la AFP.
Awali shirika la msalaba mwekundu lilisema kuwa jumla ya vifo ni 48
wakiwemo watoto 16. Uganda ina kati ya rekodi mbaya zaidi za usalama wa
barabara ambapo kwa mujibu wa takwimu rasmi kati ya mwaka 2015 na 2017
Zaidi ya watu 9,500 waliuawa kwenye ajali za barabarani nchini humo.
Comments