Serikali kuhamasisha matumizi ya nishati mbadala
Date: June 1, 2018
|
wakati dunia ikiendelea kuazimisha wiki ya mazingira serikali ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania kushirikiana na taasisi na sekta mbalimbali itakihakikisha wananchi wanatumia nishati mbadala ili kuondokana na uharibu wa mazingira
akizungumza leo wakati wa ufunguzi wa kongamano lililowashirikisha mabarozi mbalimbali makamu wa raisi Bi Samia Suluhu amesema kuwa ukataji wa misitu sana unasababishwa na matumizi ya mkaa na kuni hivyo serikali itajitahidi kuhamasisha utumiaji wa nishati mbadala ili kutunza mazingira
aidha mama Samia ameongeza kuwa matumizi ya nishati mbadala yataenda sambamba na uzalishaji wa vyombo vya plastiki na mifuko ya plastiki katika kujadiliana namna ya matumizi ya vitu hivyo katika utunzaji wa mazingira
maadhimisho haya yanaenda sambamba na kauli mbiu isemayo”mkaa gharama tumia nishati mbadala”
Comments