TAASISI ya kuzuia na kupambana na Rushwa Mkoa wa Kinondoni
(TAKUKURU) imesema kwa kipindi cha miezi(12) cha kuanzia
Julai hadi Juni 2018 imeweza kutekeleza malengo yake ya
utendaji kazi kama yalivyoainishwa kwenye Sheria ya Kuzuia
na Kupambana na Rushwa Na 11 ya mwaka 2007.
TAKUKURU Mkoa wa Kinondoni kuanzia mwezi Julai,2017 hadi Juni,
2018 iliweza kutekeleza majukumu yake kwa kupokea taarifa mpya
kufungua kesi mpya kuendesha kesi zilizokuwa zimeshafunguliwa,
kufungua majalada mapya ya uchunguzi na kuendelea na uchunguzi
wa majalada ya zamani.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam juu ya
taarifa hiyo Naibu Mkuu wa Takukuru(M)Eugenius Hazinamwisho
alisema kuwa mafanikio hayo ya utekelezaji wa jukumu la
kuchunguza taarifa za vitendo vya rushwa yametokana na
mwitikio mzuri wa jamii katika kutoa taarifa na utayari wa
kuipa TAKUKURU ushirikiano.
"Taarifa 376 zimepokelwa kutoka kwa wadau ambao ni vyombo
vya habari,vyombo vya ulinzi na usalama,Idara na Taasisi
mbalimbali pamoja na watu binafsi,uchunguziwa taarifa hizi uko
katika hatua mbalimbali,"alisema Eugenius.
Eugenius alisema kuwa taatifa hizo zimewezesha kukamatwa kwa
watuhumiwa tisa(9)mahakamani kwa kifungu namba 15 cha sheria
ya kuzuia na kupambana na rushwa namba (6)mahakamani kwa
kifungu namba 15 cha sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa
namba 11/2007.
TAKUKURU Mkoa wa Kinondoni imesema watumishi hao waliomba
rushwa ili kupindisha sheria kanuni na taratibu zinazotumika
katika utekelezaji wa majukumu yao.
Pia kesi nyingine tano(5)zilifunguliwa mahakamani ambapo
zilitolewa kibali na DPP.
Aidha katika taarifa hizo idara zilizoongoza kwa kulalamikiwa
dhidi ya vitendo vya rushwa vimetajwa kuwa ni TAMISEMI ambapo
taarifa 108(28.72%) zilipokelewa,idara ya Polisi taarifa 44 swasawa(11.70%)
zilipokelewa ambapo sekta binafsi taarifa 39
(1037%)zilipokelewa.
"Mahakamani taarifa 29 (7.71%) zilipokelewa ambapo ardhi
taarifa 22(5.85%)zilipokelwa na sekta ya elimu taarifa 14
(3.72%)zilipkelewa,"alisema Eugenius.
Eugenius alisema katika kipindi cha Julai 2017 hadi Juni 2018 taasisi imedhibiti na kuokoa jumla ya fedha za kitanzania milioni sabini na nane laki nne tisini na saba elfu mia tisa hamsini na sita na senti hamsini(78,497,956.50).
Kwa upande wa utoaji wa elimu kwa umma TAKUKURU imeendelea
kutekeleza majukumu yake ya kufanya utafiti na udhibiti na
uchambuzi mifumo,utendaji ,na miradi ya maendeleo ambapo
mifumo sita katika ofisi za TANESCO Kimara Wilaya ya Ubungo,TA
NESCO Tegeta Wilaya ya Kinondoni, pia DAWASCO Boko Wilaya ya
Kinondoni pamoja na Kimara Wilaya ya Ubungo zingine ni TASAF Manispaa
Ubungo na katika maeneo ya wazi kufanywa masoko na kusababisha serikali
kupoteza mapato.
TAKUKURU Kinondoni imeeleza kuwa katika kutekeleza majukumu ya
utafiti,udhibiti na uchambuzi wa mifumo jumla ya warsha 4 zili
fanyika katika idara zilizofanyiwa uchunguzi wa mifumo na kati
ya hizo idara tatu ziliweka makubaliano ya pamoja ya
jinsi ya kushughulikia mapungufu yaliyobainishwa.
Pia katika kuhakikisha kuwa fedha za serikali zinatumika
kulingana na lengo lililokusudiwa,thamani halisi ya fedha na
utekelezaji wa miradi kwa wakati TAKUKUTU Mkoa wa Kinondoni
imefuatilia miradi nane(8)ya maendeleo yenye jumla ya thamani
ya shilingi bilioni tatu nukta tisa (3.9 bilioni)nakufanyiwa
ukaguzi na udhibiti kwa lengo la kujua ubora wa miradi na
iwapo taratibu za matumizi ya fedha za umma umezingatiwa.
Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Kinondoni anatoa wito kwa Wananchi
wote kuendelea kushirikiana na taasisi katika mapambano dhidi
ya Rushwa kwa kutoa taarifa za vitendo vya rushwa,kwa kufika
ofisini au kwa kupiga namba 0652 409 165,wananchi pia wanaweza
kupiga simu ya bure namba 113 au kutuma ujumbe mfupi wa maneno
kwenda namba 113.
Taasisi inawaasa viongozi na watumishi wa umma na wa sekta
binafsi kuacha mara moja kujihusisha na vitendo vya rushwa
kwani watakapobainishka kufanya hivyo hatua za kisheria
zitachukuliwa dhidi yao.
Comments