WANAFUNZI wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha nchini kilichopo jijini Dar es Salaam (IFM)
kimefanya maandamano ya hamasa juu ya kada mbalimbali kuelewa zaidi umuhimu wa
wananchi kuwa na bima.
Maandamano hayo yenyelengo la kuongeza uelewa wa wananchi juu ya utumiaji
wa huduma za bima yaliyopewa kaulimbiu ya "BILA BIMA HAUNA SALAMA YA KUTOSHA"
yalianzia katikati ya mitaa ya Jiji na kuhitimishwa katika ukumbi wa Karimjee
jijini hapa.
Katika maandamano hayo hamasa kwa wananchi ilitolewa na chama cha madalali wa BIMA tanzania TIBA juu ya huduma za bima nchini imeelezwa kuwa mwitikio bado ni mdogo .
Hali hiyo imethibitishwa na wadau wa bima katika maandamano yaliyoratibiwa na
chuo hicho cha IFM kwa hisana ya TIBA yaliyojumuisha wadau wa bima na wanafunzi
wote wa masomo ya bima kutoka chuoni hapo na wakuu wao wa idara ya
Wadau mbali mbali walioshiriki katika maandamano hayo kwa lengo
la kuongeza mwamko wa kutumia bima za aina mbali mbali katika kukabilia
na na changamoto mbali mbali za maisha na hasa kuelekea katika uchumi
wa viwanda.
Kamishina Mkuu Wakala wa za Bima kwa upande wa serikali (TRA),Baghayo
Saqware amewatoa hofu wananchi kuhusu bidhaa za bima kwamba hakuna kampuni ya bima ambayo ni feki,kwa kuwa zote zimesajiliwa na kupewa leseni na TRA
"Katika maisha ya mtanzania kumekuwa na vitu ambavyo haviepukiki kama magonjwa ya
kushitukizwa ajali za bara barani,moto,vifo na mengine mengi ambayo yanaweza kumpata
mtu na wakati huo akiwa hana pesa mfukoni lakini akiwa na bima aina haja ya kupaniki
anaamini bima zita mwezesha katika kumaliza matatizo hayo,"anasema Saqware.
Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais JPM imekuwa ikishauri watu kuzidi kuzishambulia
huduma za bima ambapo ni moja ya ajenda zake wakati akiingia madarakani ambazo
zina tija ya kuhakikisha maskini anapata unafuu katika maisha yake.
Mhadhiri na Mkuu wa Idara ya Bima wa Chuo hicho Dkt.Mussa Juma amesema wamekuwa na desturi ya kufanya maandamano ya aina hiyo kila mwaka hili kuongeza uelewa wa bima kwa Umma wa Tanzania baada ya kufanya utafiti na kugundua kuwa asilimia 65 ya watanzania wote hawana uelewa juu ya huduma za bima na wengine hawajui bima ni nini.
"Mara ya tatu tunafanya maandamano haya ambapo tunaona tunafanikiwa kuongeza
mwitikio kwa watanzania kutumia bima,kadri watu wanavyosikia kupitia
vyombo vya habari kwa kiasi kikubwa kuna mwitikio mzuri juu ya ununuzi wa
bidhaa za bima,"anasema Dkt.Juma.
Mwanafunzi wa shahada katika sayansi ya bima(Bachelor of Science and Risk
Management)Mkagambage Fulgence Kyaruzi amesema amejikuta akivutiwa kusoma
mazomo hayo baada ya kugundua hayana changamoto kubwa katika ulimwengu wa ajira.
"Uchumi unakuwa na tunaelekea katika uchumi wa viwanda ambapo viwanda vyenyewe,
kampuni binafsi,taasisi na ata mtu mmoja mmoja ataitaji bima hili kurahisisha
shughuli zake. Hivyo nikiwa na elimu ya masuala ya bima ata nisipo ajiliwa
ninajua namna gani ya kujiongeza kutoa elimu kwa wananchi na kisha kufanikiwa
kuwauzia bidhaa zangu za bima.Katika kampuni mbali mbali za bima kuna programu
za kuwawezesha watoa huduma za bima chipukizi kuwafikia wananchi vijijini,"anasema
Kyaruzi.
Makamu Mkuu wa Chuo anaye simamia Taaluma,Utafiti na Ushauri Dkt.Imanuel Mnzava
amesema kutokana na kwamba Chuo cha Usimamizi wa Fedha nchini (IFM)ni chuo pekee
nchini kinachotoa taaluma ya bima jambo ambalo linawafanya kutoa motisha kwa
wanafunzi wanaofanya vizuri katika masomo ya bima hili kushawishi wahitimu
wenye sifa stahiki kujiunga na kitivo hicho hili kuisaidia seriklai kupata wataalamu
wengi wa huduma za bima ambao ndio wenye uwezo mkubwa wa kumshawishi mtu na kisha kumuuzia bima.
"Watanzania ni wengi zaidi ya milioni 50 lakini ni asilimia 20 tu wenye uelewa
kuhusu bima hivyo toka 2016 tulipoanzisha programu ya kufanya maandamano na kushiri
kisha wanahabari tulianza watu mia na leo washiriki ni zaidi ya 400.Kadhalika ripoti
ya bima 2016 kutoka TRA inaonesha asilimia 7 ya watumiaji imeongezeka ambapo inakadiriwa siku za usoni ongezeko la asilimia 1 kila mwaka litawezekana,"anasema Mnzava.
Mchango wa sekta ya bima katika pato la taifa ni chini ya asilimia moja ya pato
la taifa ukilinganisha na nchini jirani ya Kenya pamoja na nchini nyingine kama
Zimbabwe na nchi nyingine zenye uchumi mkubwa.Jambo ambalo linahitaji nguvu ya
pamoja ya wadau wote na wananchi kwa pamoja katika kubadili mtazamo uliopo.
Kwa upande wake Rais wa Chama cha Madalali wa huduma za bima nchini (TIBA)Mohamed
Jaffer amesema tayari TIBA imeandaa kamati ya watu saba itakayoandaa mpango kazi
wa utoaji huduma za bima kwa miaka minne ijayo ambapo baada ya yeye kustaafu Rais
ajae itampasa kufuata mpango kazi alioukuta katika chama na kuusimamia hili mtazamo
wao wa kuhakikisha kila mwananchini anatumia huduma za bima walau zile za lazima
ifikapo miaka 2025 uweze kufanikiwa.
"Pamoja na majukumu mengine ya chama Rais mpya anapaswa kufuata mpango kazi
alioukuta kwenye chama akisaidiana na wanakamati 7 kuutekeleza hili kutimiza
malengo ya chama kama ilivyo kusudiwa,"anasema Jaffer.
Comments