Skip to main content

Posts

Showing posts from 2011

Grooveback New Year's Eve Party!!

Waziri Dk Terezya Huvisa asaini kitabu cha maombolezo ubalozi wa korea kusini

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Dk Terezya Huvisa akiagana na Kaimu Balozi wa Korea ya Kusini Nchini Tanzania Bw Kim Yong Su Mara Baada ya Kuweka Saini Kitabu cha Maombolezo Kufuatia Kifo cha Kiongozi wa Nchi hio Kim Jong ll [Picha na Ali Meja}   Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Dk Terezya Huvisa akitia Saini Kitabu cha Maombolezo kwenye Ubalozi wa Korea ya Kusini Kufuatia kifo cha kiongozi wa Nchi Hiyo Kim Jong ll, Waziri aliweka saini kwa niaba ya Makamu wa Rais Dk Muhammed Gharib Bilali katika Ofisi za Ubalozini huo Mikocheni Mjini Dar es Salaam.[Picha na Ali Meja]

Killin’ for Candy and Concords: The Price of Black Life

by TRUTH Minista Paul Scott Hot Stories from All Hip Hop Young Buck Assets Face Liquidation The 2011 Playback: “AllHipHop: We’re Not Them” ATF and D.C. Police Impersonate Rap Label; Arrest 70 in Year Long Guns and Drug Sting R&B’s Anthony Hamilton Drops His “Top 5 Dead or Alive” On AllHipHop.com Daily Word: Happy Holidays!!! Breaking News: Police ID Rapper Young Vito As Suspect In Slim Dunkin Murder T.I. Ft. Rick Ross “I’m Flexin Remix” Slim Dunkin Funeral Set For Friday Young Buck Assets Face Liquidation The 2011 Playback: “AllHipHop: We’re Not Them” ATF and D.C. Police Impersonate Rap L

Maalim Seif: Zanzibar iwe na Benki Kuu; Mafuta na gesi si vya Muungano; Urais wa Muungano kwa Mzunguko

  Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad, amesema ni muhimu kwa sasa Zanzibar kuwa na benki kuu yake ikiwa inataka kutumia kikamilifu rasilimali zake kujenga uchumi wake.     Maalim Seif ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, akizungumza katika viwanja vya Kibandamaiti mjini hapa juzi alisema kuendelea kutegemea Benki Kuu ya Tanzania (BoT), kunainyima Zanzibar kutekeleza mipango yake ya maendeleo kwa ufanisi.   Aliuambia umati mkubwa uliojaa kwenye viwanja hivyo kuwa wananchi visiwani humo wanaweza kudai haki ya Zanzibar kuwa na benki kuu kwa njia ya kutoa maoni kupitia hatua mbalimbali za mchakato unaoendelea juu ya Katiba mpya ya Tanzania.   Akizungumzia huduma za BoT kwa Zanzibar, Maalim Seif alisema uwiano mbaya wa wafanyakazi kutoka pande mbili za Muungano unasababisha upungufu wa wataalam wa kuishauri benki hiyo juu ya mahitaji ya Zanzibar, “Ikiwa kwa mfano BoT ina wafanyakazi 80 na wanne tu wanatoka Zanzibar, bila shaka uwi

‘Umushyikirano’: Somo murua kwa JK kutoka kwa Kagame!

Johnson Mbwambo   KATIKA toleo Na. 215 la Raia Mwema, Jenerali Ulimwengu alitaja moja ya mapungufu ya watawala wetu Tanzania kwamba ni ile hulka yao ya kutotaka kujifunza na kuiga kutoka kwa wenzetu wa nje (Ughaibuni) wanaofanya vizuri. Aliandika hivi: “Watawala wetu ni watu wanaosafiri mno, hadi wamesababisha malalamiko kwamba hawatulii nyumbani jinsi walivyo ‘kiguru na njia’. Inashangaza kwamba wanakwenda Ughaibuni kila uchao lakini hawana wanachojifunza huko kuhusu jinsi wenzao walivyopiga hatua za haraka kujiletea maendeleo na kuzikwamua nchi zao kutoka kwenye mateso ya umasikini. “Wanakwenda Ughaibuni kushangaa maendeleo ya wenzetu na kufanya ‘shopping’ za upuuzi wakati nchi yao inadidimia. Hawana uwezo hata wa kutazama, kuona, kuelewa na kutaka kuiga kilicho kizuri.” Hivyo ndivyo alivyoandika Jenerali katika toleo hilo. Napenda kuuendeleza kidogo mjadala huo, na nianze kwa ku

Miaka 50 ya Uhuru wa Tanganyika, maswali 50 ya kujiuliza II

Jenerali Ulimwengu   Ifuatayo ni sehemu ya pili ya maswali 50 ninayodhani tunatakiwa kujiuliza wakati tukiadhimisha miaka 50 ya Uhuru wa Tanganyika. Maswali 25 ya kwanza yalikuwa katika toleo la wiki jana: Je, hii ni nchi yetu na nchi ya wana wetu na vizazi vitakavyokuja (bila mwisho), na je, sisi tuliopo leo ni watu wenye dhamana ya kuitunza, kuilinda, kuitetea na kuiendeleza kwa niaba ya vizazi hivyo, au sisi dhima yetu ni kuitumia, kuitafuna, kuila, kuikamua hadi tone la mwisho ili tunapoondoka duniani kusiwe kumebakia kitu? Ni kwa nini tunawachukia wanetu na wana wao kiasi hicho? Ni kwa nini tumeachia masuala ya kuendesha nchi yetu yawe ni miradi ya wajanja wachache, walaghai na mabarakala, na watu waadilifu wamejiweka kando, wamekata tamaa, na hatima ya nchi hii wamewasabilia mabazazi? Leo tunawashangaa wabunge kutaka kujiongezea posho; ni lipi la kutushangaza? Mbona hivyo ndivyo watawala wetu wamekuwa wakifanya wakati wote? Mbona hatukushangaa wakati wanagaw

Vita ya kumkomboa mwanamke inahitaji uelewa mpana wa mambo

Vita ya kumkomboa mwanamke inahitaji uelewa mpana wa mambo   MCHANGO wa wanawake katika maendeleo ya jamii tangu historia ya vizazi na vizazi vilivyopita hauwezi kupuuzwa.Wanawake wamekuwa mstari wa mbele katika kufanya shughuli za maendeleo, kuendesha familia na vikundi vya kijamii, kulea watoto na kushiriki moja kwa moja kwenye shughuli mbalimbali za kiuchumi na kiutawala. Lakini pamoja na mchango wao ulio wazi kwa jamii nyingi, bado nafasi yao katika jamii ni finyu. Tena kadri ziku zinavyozidi kusonga mbele, nafasi yao katika michango ya maendeleo inaachwa nyuma au kupotoshwa kutokana na maslahi ya jamii, kikundi fulani au kuingia kwa upofu mkubwa miongoni mwa jamii pana. Historia inatuambia tangu enzi za wanafalsafa na wanazuoni wa mwanzo huko Ugiriki,  wanawake hawakutambuliwa kama raia. Siku zote hawakuwa raia wa nchi hiyo na kwingineko. Hali ikaja kubadilika baadaye na sasa wanafurahia nafasi yao kama raia na kama ilivyo kwa binadamu wengine.Nchi ya

KHERI YA CHRISTMAS NA MWAKA MPYA !

POPE BENEDICT'S HOMILY AT THE MIDNIGHT MASS Submitted by Mjengwa on 25.12.11 Mimi  Francis Machibya ambaye ni mmiliki na muendeshaji wa blogi hii , ninawatakia kheri ya Christmas na mwaka mpya.

UZINDUZI WA BIA MPYA 'SENETOR EXTRA LAGER'

   Mkurugenzi wa masoko wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) Ephraim Mafuru akizungumza katika uzinduzi wa bia mpya ya Senetor Extra Lager ambayo imeanza kuzaliashwa na kusambazwa na kampuni hiyo. Bia hiyo inawalenga wachapakazi wa hali ya chini kabisa, wakulima, wavuvi na wengineo wa kanda ya ziwa na majirani zake. Bia ya Senetor itauzwa kwa bei nzuri ya shilingi elfu moja na mia tatu tu (1,300/-)      Na Mashaka Baltazar,MWANZA   KAMPUNI ya Bia ya Serengeti (SBL) imezindua kinywaji kipya cha bia ya Senator, kinachozalishwa kwa kutokana na mazao ya mtama na shayiri na kuwataka wakulima wa mikoa ya Kanda ya Ziwa kulima mazao hayo kwa vile watakuwa na soko la uhakika. Hafla ya uzinduzi huo ilifanyika jana katika kiwanda cha SBL Mwanza,kuhudhuruiwa na baadhi ya wafanyakazi,mawakala na wauzaji wa bidhaa za kampuni ya SBL. Akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na uzinduzi wa kinywaji hicho kipya, Mkurugenzi wa

Dkt. Bilal atembelea kambi za waathirika wa mafuriko Dar

Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na mmoja kati ya wananchi waliohifadhiwa katika Kambi ya Shule ya Sekondari ya Azania, waliookolewa katika maeneo yaliyojaa maji  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Bi. Monica Luis, Mkazi wa Jangwani aliyeathirika na mafuriko  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na baadhi ya wananchi waliohifadhiwa katika Klabu ya timu ya Yanga ya Jijini Dar es Salaam, wakati alipowatembelea kuwapa pole leo. Makamu wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo ya jinsi maji yalivyokuwa yamejaa wakati wa mvua kubwa iliyosababisha mafuriko, kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Sadik Mecky Sadick Channzo ni Nyakasagani .Blogspot.

CHADEMA watinga na misaada kwa waathirika wa mafuriko Dar

 Mbunge wa Ubungo Bw. John Mnyika (aliyeinua mikono), akimuelekekeza Mwenyekiti wa CHADEMA Bw. Freeman Mbowe, na viongozi wa Chama hicho, eneo la Sinza lililoathiriwa vibaya na mafuriko, walipolitembelea leo  Mwenyekiti wa CHADEMA Bw. Freeman Mbowe akitoa msaada wa maji, mafuta na vyakula kwa waathirika wa mafuriko Dar leo  Mbowe akikabiidhi msaada wa mafuta ya kula kwa mmoja wa waathirika wa mafuriko leo.  Mbowe akizungumza na wananchi waliokumbwa na mafuriko leo.  Mbowe akiwasilikiliza waathirika wa mafuriko Kawe, alipowatembelea leo Posted by Maseypr at 7:28 AM 0 comments Email This BlogThis! Share to Twitter Share to Facebook Labels: Na Nyakasagani Masenza CHADEMA watembelea waathirika wa mafuriko Dar, watoa misaada  Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, akizungumza na waandishi wa habari, baada ya kutembelea eneo la mafuriko, Dar es Salaam leo  Mbowe akisaini kit

RASHIDI MATUMLA NA MANENO OSWARD WAPIMA UZITO LEO KWA AJILI YA MPAMBANO WAO KESHO

Mratibu wa pam\\\bano la Ngumi za kulipwa, Shabani Adios 'Mwayamwaya' akiwa katikati ya mabondia,Maneno Osward 'Mtambo wa Gongo' kushoto na Rashidi Matumla 'Snake Man', baada ya kupima uzito leo, kwa ajili ya pambano lao, litakalofanyika kwenye Ukumbi wa Helnken Mtoni Kijichi, Dar es Salaam siku ya Xmasi. (Picha na www.superdboxingcoach. blogspot.com ) Mabondia,Maneno Osward 'Mtambo wa Gongo' kushoto na Rashidi Matumla 'Snake Man', wakipima uzito leo, kwa ajili ya pambano lao, litakalofanyika kwenye Ukumbi wa Helnken Mtoni KIjichi, Dar es Salaam siku ya Xmas. (Picha na www.superdboxingcoach. blogspot.com

Ligi Kuu ya Uingereza (Premier League)

Kama Jack Wilshere, akiendelea kutumia muda mwingi akiwa majeruhi, Gonzalez anaweza kusajiliwa kwa muda kuziba pengo lake, lakini kikwazo kikubwa kitakachoweza kumkwamisha asijiunge na Arsenal ni umri na ada ya uhamisho, ambayo timu yake itahitaji .