Skip to main content

Miaka 50 ya Uhuru wa Tanganyika, maswali 50 ya kujiuliza II


Ifuatayo ni sehemu ya pili ya maswali 50 ninayodhani tunatakiwa kujiuliza wakati tukiadhimisha miaka 50 ya Uhuru wa Tanganyika. Maswali 25 ya kwanza yalikuwa katika toleo la wiki jana:

  1. Je, hii ni nchi yetu na nchi ya wana wetu na vizazi vitakavyokuja (bila mwisho), na je, sisi tuliopo leo ni watu wenye dhamana ya kuitunza, kuilinda, kuitetea na kuiendeleza kwa niaba ya vizazi hivyo, au sisi dhima yetu ni kuitumia, kuitafuna, kuila, kuikamua hadi tone la mwisho ili tunapoondoka duniani kusiwe kumebakia kitu? Ni kwa nini tunawachukia wanetu na wana wao kiasi hicho?
  2. Ni kwa nini tumeachia masuala ya kuendesha nchi yetu yawe ni miradi ya wajanja wachache, walaghai na mabarakala, na watu waadilifu wamejiweka kando, wamekata tamaa, na hatima ya nchi hii wamewasabilia mabazazi?
  3. Leo tunawashangaa wabunge kutaka kujiongezea posho; ni lipi la kutushangaza? Mbona hivyo ndivyo watawala wetu wamekuwa wakifanya wakati wote? Mbona hatukushangaa wakati wanagawana nyumba za Serikali? Kwa nini hatukushangaa wakati mkuu wa nchi anajigawia mgodi wa Serikali na asishitakiwe na lolote lisiwe? Kwa nini hatushangai kwamba Serikali omba omba ndiyo inaanika hadharani matumizi ya kufuru katika magari ya fahari, safari za nje bila sababu, ‘uheshimiwa’ usiokuwa na heshima?
  4. Kwa nini tunaendelea kuwa na ‘wawakilishi’ wa wananchi wasiojua majukumu yao, mpaka wanatuambia kwamba kazi yao ni kugawa fedha majimboni? Nani kawapa jukumu hilo, na kama hilo ndilo jukumu lao kweli, ni lini tuliwawekea viwango vya pesa wanazotakiwa kuwapa wapiga kura wao?
  5. Ni kwa nini sisi ni wapenzi wakubwa wa upuuzi? Ni kwa nini hatuko makini katika mambo yanayohitaji umakini? Kwa nini inakuwa vigumu kusema ni katika kitu gani tumejipambanua kwa ufanisi mbele ya mataifa mengine? Elimu? Viwanda? Kilimo? Usafi wa miji? Uadilifu na mapambano dhidi ya ufisadi? Michezo? Hata lugha ya Kiswahili, ni kwa nini tumewaachia Wakenya?
  6. Ni kwa nini miji yetu imejaa vituo vya ulevi na uzinzi na hatuna vituo vya elimu au maktaba za wananchi wanaotafuta ujuzi? Ni kwa nini tumekubali kwamba sisi tutawekeza katika ujinga wakati wenzetu wa Kenya na Uganda wanawekeza katika elimu, halafu tunakuwa watu wa kulalamika kwamba hawa majirani watatunyang’anya ajira zetu? Kama tumekubali kuwekeza katika harusi na “kichen pati”, je, tumekubali pia kwamba tukiunganisha nchi zetu jukumu letu litakuwa ni kuandaa “kichen pati” wakati wenzetu wanatengeneza kompyuta?
  7. Ni kwa nini Watanzania walio ughaibuni wanafanya vizuri kutumikia nchi nyingine lakini wakiwa nyumbani wanakuwa hawafai?
  8. Mkuu mmoja wa nchi hii alizoea kuwaambia Watanzania kwamba ni wavivu wa kufikiri. Je, hii ni kweli, na kama ni kweli, je ni uvivu huo wa kufikiri unaotufanya tuwachague viongozi wa hovyo, pamoja na yeye mwenyewe?
  9. Tumethubutu, tumeweza, sasa tunasonga mbele? Kweli? Tumethubutu katika lipi zaidi ya ule uthubutu wa kuwaibia watu wetu na kuwadumaza kimaendeleo? Tumeweza nini zaidi ya kwamba tumeweza kuwadanganya watu wetu wakatuachia tuendelee kuwadanganya. Tunasonga mbele kwenda wapi? Kwa nini tunapenda maneno maneno yasiyosimama juu ya misingi ya mantiki?
  10. Tumethubutu kuua viwanda vyetu karibu vyote tulivyokuwa navyo, hata viwanda vya kuongeza thamani kwa mazao yetu na viwanda vya kuzalisha mazao hayo; huko ndiko kuthubutu tunakojivunia? Tunaagiza kutoka nje (hususan China) kila kitu, hadi sindano na uzi; je tunajua kwamba tunaongeza ajira za vijana wa China huku tukiwanyima ajira vijana wetu?
  11. Tumeweza kupuuza kilimo kwa muda mrefu, pamoja na kuhakikisha kwamba hata vile viwanda vichanga vya kuunda nyenzo za kilimo tumeviua, kisha tunadiriki kusema kwamba kilimo ndio uti wa mgongo wa uchumi wetu? Mkuu wa nchi aliyeulizwa iwapo kuna jambo anadhani amelisahau katika kipindi cha miaka kumi ya utawala wake, naye akajibu “labda kilimo” alitaka kutuambia kwamba muda wote aliokuwa madarakani alikuwa anashugulikia nini kama alisahau maisha ya  asilimia 80 ya Watanzania?
  12. Tunasonga mbele kuelekea wapi? Huko huko ambako tumekuwa tukielekea kwa takriban miaka ishirini na tano, ambako hatukujui? Hivi hatujkaelewa msemo kwamba kama hujui unakokwenda, njia yo yote itakufikisha huko?
  13. Tunasonga mbele kwa elimu ipi inayotoa wahitimu wa darasa la saba wasio na ujuzi wa darasa la pili? Majengo yanayoitwa shule huku yakiwa hayana walimu? Mitihani inayouzwa kijiweni? Huku ni kusonga mbele au ni kusonga nyuma?
  14. Miaka hamsini ya Uhuru wa Tanganyika tumetoa wataalamu gani wa kujivunia? Ni kwa nini tunao madaktari wengi wa fizikia lakini hatuna wanafizikia, maprofesa wa historia lakini hatuna wanahistoria, na kadhalika katika medani takriban zote? Miaka hamsini tumetoa mteule (nominee) mmoja tu wa Nobel (Kamuzora), tena wa mwaka 1980; hatuoni haya?
  15. Je, hatuoni kwamba elimu duni isiyofikirisha ndiyo chanzo cha ushirikina wa kila aina, toka imani za tiba za ‘kikombe’ hadi viungo vya albino kupitia wachuna ngozi? Iwapo hata watu waliodhaniwa kuwa wasomi na watu wakubwa miongoni mwa watawala wetu katika ngazi za juu bado wanaamini uchawi, je tumewahi kuvuka karne ya XV? Imani za watu kuweza kupaa kwa ungo zinaendana vipi na teknolojia na kompyuta mawingu (cloud computing)?
  16. Je, tunaamini kwamba nchi inaweza kuendela bila mipango ya maendeleo, kwamba alimradi tupo na tumetimiza miaka hamsini, basi tutaendelea tu, tupende tusipende? Hatuelewi kwamba maendeleo hayana budi kupangiliwa na kusukumwa na uwekezaji usiositasita kwa muda wote. Hatuoni kwamba tunaweza kudumaa na hiyo ikawa ndiyo hatima yetu kwa siku zijazo? Hatujaona nchi kama Haiti, ambayo miaka 200 baada ya Uhuru uliopiganiwa kishujaa, bado ni nchi ya dunia ya nne? Wakati huo huo hatuoni wenzetu wa Kenya, Msumbiji, Rwanda, Botswana na Ethiopia (nitaje nchi za karibu) wakionyesha maendeleo katika kipindi kifupi kwa sababu ya fikra chanya na matendo madhubuti, na kukataa upuuzi? Miaka 50 ni robo ya umri wa Haiti; hatuoni kwamba kwa mtaji huu, tutakapotimiza miaka 200 tutakuwa kama Haiti ilivyo leo? Hatuogopi vizazi vijavyo na laana zake kwetu?
  17. Imekuwaje tumekubali kwamba rushwa, ufisadi na upuuzi ndizo alama za utambulisho wa Mtanzania? Hivi hatujaona macho yanayotutazama ‘tenge’ tukiwa ughaibuni anapoingia albino katika chumba cha mkutano? Hili halitutii unyonge moyoni?
  18. Hivi ni kweli tumeshindwa kupambana na ufisadi, na angalau kuupunguza, kama wenzetu walivyoweza nchini Botswana, Rwanda na Ethiopia? Tunaona uzito gani kufanya jitihada za kuiga kutoka kwa wenzetu iwapo kila mtu anayekwenda huko anarudi na sifa za mambo mema? Au tumekwisha kuamini kwamba hao wenzetu ni wao na sisi ni sisi, na ndani yetu hatuna uwezo wa kujifunza kutoka kwao kwani tumeamua kuwa watu wa upuuzi? Tunashindwa nini kuwa ‘high-minded’ na kwa nini ni lazima tuwe watu wa ‘nonsense’ ?
  19. Tunashindwa nini kujifunza kutoka kwa wenzetu, ambao nao wanayo matatizo ya rushwa na ufisadi lakini hawana  “Mswalie Mtume” wanapomkamata kiongozi aliyewaibia. Hatujaona marais wakifungwa kwa sababu walipokuwa madarakani walitumia nafasi zao kujitajirisha? Hatuoni kwamba kuwaachia wakubwa wakaiba na kisha wakaachiwa bila adhabu ndiyo sababu ya watu kutoogopa kutenda jinai wanapokuwa madarakani?
  20. Ni kwa nini tunadangayika, kwa vishawishi vya kipuuzi na shibe ya siku moja, kuwachagua watu ambao hatujui wana fikra gani za kimaendeleo, watu ambao hawajawahi kuandika sentenso moja ya kueleza wanafikiri nini na wana dhamira gani kwa nchi yetu? Sasa tunashangaa nini wanapokuja kuonekana hawafai?
  21. Juzi watu kadhaa wamepewa nishani kama njia ya kutambua mchango wao katika miaka 50 ya Uhuru wa Tanganyika; nani hasa anajua ni vigezo gani vimetumika kuwapa baadhi na kuwanyima baadhi? Wapo waliohoji vigezo hivyo; mbona hatusikii majibu? Ni kwa nini suala la nishani za utumishi kwa umma linafanywa kama fadhila badala ya kuwekewa vigezo madhubuti, jambo litakalofanya watu waanze kuzibeza hata hizo nishani zenyewe kama zilizogubikwa na ufisadi?
  22. Kama nchi, Tanzania ilijijengea sifa kama taifa la watu wenye misimamo ya kujali utu, kuwajali wanyonge, kupigania haki kote duniani, kupinga ubeberu na kila aina ya uonevu. Sifa hizi zimekwenda wapi? Ni kitu gani kimetugeuza kuwa watu wa dhuluma na ulaghai, uroho, ulafi na ubabaishaji? Ni kwa nini tunakubali kupoteza tunu hii iliyotujengea sifa mbele ya mataifa mengine?
  23. Ni kwa nini tunakubali kuwa jalala kunakotupwa kila takataka, nyingine zikiwa ni zenye sumu za maangamizi tunazouziwa kama dawa, vipodozi, huku tukishuhudia jinsi watu wanavyozidi kufa kwa saratani za kila aina ambazo hatukuziona siku za nyuma? Je, hatuoni uhusiano wa moja kwa moja kati ya saratani hizi na uroho wa baadhi yetu wanaotamani utajiri haramu?
  24. Ni kwa nini tumekubali ubinafsishaji ufikie kiwango cha kubinafsisha hata dola na Serikali, kiasi kwamba karibu kila mtumishi wa Serikali amejibinafsishia idara yake na anaitumia kama kitegauchumi chake?  Maofisa wa Serikali wakiisha kuwa ni wafanyabiashara na wakatumia ofisi zao kwa shughuli binafsi, ni nani atawahudumia wananchi wanaohitaji huduma za idara za Serikali?
  25. Tumepotea njia au hatujapotea njia? Kama hatujapotea, ni kwa nini hakuna dalili kwamba tunakaribia hatima ya safari yetu? Mbona tunazungukazunguka, mara tukirudia alama tulizokwisha kuzipita huku viwango vya uwezo wetu wa kuendelea na safari vikionekana kupungua?
Kama tumepotea, mbona hatuketi chini tukatafakari upya safari hii tunataka itupeleke wapi na tuamue njia mwafaka ya kutupeleka huko? Au tunasubiri litote tugawane mbao? Chanzo ni Gazeti la Raia Mwema.

Comments

Popular posts from this blog

Thousands of protesters clash with police in Chicago: Chaos in the Windy City as 45 activists arrested and one cop stabbed after demonstrators target NATO

By DAILY MAIL REPORTER Thousands of demonstrators upset with the war in Afghanistan, climate change and the erosion of union rights have raised the intensity of a march in downtown Chicago on Sunday as world leaders assembled for a NATO summit. The protest, one of the city's largest in years, turned violent at the end of an anti-NATO march, where demonstrators confronted Chicago police, pushing against a line of officers several blocks from the lakefront convention center where President Obama hosted a gathering of world leaders. Authorities were seen making arrests one by one and leading individual demonstrators away in handcuffs. After a clash near McCormick Place, Chicago Police Superintendent Garry McCarthy said at a news conference that the protests resulted in 45 people being arrested and four officers suffering injuries - one from a stab wound in the leg. Scroll down for video Clash: Demonstrators try to flee the police as they are move in on them

MBINU ZA KUMFIKISHA MWANAMKE MWENYE MAKALIO MAKUBWA KILELENI KWA HARAKA

Kwa kawaida wanawake wanafikia kilele (mwisho wa utamu wa ngono) kati ya dakika ishirini na saa moja, yaani kwa kifupi inawachukua muda mrefu sana hali inayopelekea mpenzi mvivu kuchoka na ufanyaji wake utakuwa wa “ovyo” hali itakayo kufanya wewe kuishiwa na hamu ya kuendelea. Pamoja na kuchelewa huko ambako kunatokana na utofauti wetu kati ya mwanaume na mwanamke lakini nakumbuka hapo nyuma nilikutana na wanawake 2 waliokuwa ndani ya ndoa na wamezaa lakini hawajawahi kabisa kujua utamu wa tendo hilo alimaharufu kama “kufanya mapenzi”. Natambua kuwa ni ngumu au niseme si wanawake wote ambao wamejaaliwa kimaumbile kwamba wanafanikiwa kufika kileleni zaidi ya mara mbili kila wanapofanya mapenzi/ngono (kumbuka ni kati ya dakika 15 na saa moja hivyo Jibaba hapa awe na uwezo wa kujizuia kwa zaidi ya dk 45) na ikiwa jamaa ni “mzamiaji” basi unaweza ukaondoka na goli 3 ktk mzunguuko mmoja. Lakini kwa nini basi baadhi yao tu ndio wafike kileleni na wengine was

HAYA NI MAKAO MAKUU YA MTANDAO WA Tigo TANZANIA DAR ES SALAAM

MAHALA yalipo ni Lugoda Street Gerezani Industrial Area , kwa sasa mdandao huu umefanya makubwa , kuna Tigo Bwerere Uilisha cheki hiyoooooo watu full kujiachia wana chonga tuu kwenye vyao vilonga.