Skip to main content

Posts

Showing posts from December, 2015

BAADA YA KUWATUMBUA WAKWEPA KODI,WAZIRI WA FEDHA ATANGAZA KIAMA KWA HAWA,ATOA KAULI NZITO

      BAADA ya kushughulikia wakwepa kodi ndani ya siku 27 alizokaa Mamlaka ya Mapato (TRA), Waziri mpya wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango amehamishia nguvu zake katika sekta ya fedha hasa benki, akizitaka zipunguze riba. Akizungumza na waandishi wa habari Ikulu Dar es Salaam jana, baada ya kuapishwa na Rais John Magufuli, Dk Mpango aliahidi kushughulikia tatizo la riba kubwa, inayotolewa kwenye benki za hapa nchini, jambo linalochangia kushusha idadi ya watu wanaokwenda benki kukopa. “Lazima sekta ya fedha isimamiwe vizuri ili kila mwananchi aweze kukopa, nitahakikisha riba za mikopo zinashuka ili wananchi wajipatie mikopo kwa riba nafuu,” alisema Dk Mpango. Born in Tanganyika to Nyerere Burito (1860–1942), Chief of the Zanaki,Nyerere was known by the Swahilihonorific Mwalimu or 'teacher', his profession prior to politics. He was also referred to as Baba wa Taifa (Father of the Nation).Nyerere received his higher education at Makerere Univer

Homecoming live ndani ya Sinema Zetu ya Azam

Na Mwandishi Wetu KAMPUNI ya Azam Media itaonesha live uzinduzi wa filamu ya Homecoming utakaofanyika keshokutwa katika Ukumbi wa Mlimani City. Azam kupitia king’amuzi chake itaonesha uzinduzi huo kupitia Chanel yake ya Sinema Zetu ambapo pia watangazaji wake watafanya mahojiano ya moja kwa moja na wageni watakaohudhuria hafla hiyo. Akizungumzia kuhusiana na hatua hiyo ya kuonesha tuko hilo Meneja Masoko wa Azam Mgope Kiwanga alisema kuwa king’amuzi hicho kinatambua nafasi ya filamu katika maendeleo ya sanaa na ndio maana imeamua kuunga mkono uzinduzi huo. Alisema kuwa Azam kupitia chanel yake hiyo wamekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha kuwa wapenzi wa filamu za hapa nyumbani wanaangalia kila kinachoendelea katika tasnia hiyo na ndio wameamua kuwaunganisha moja kwa moja kuona tukio hilo. “Sinema Zetu ni channel ambayo tuliiweka maalum kwa ajili ya filamu za kitanzania na hii filamu ya Homecoming ni zaidi ya filamu kwa kuwa kwanza ina viwango vya uhakika na wanan

Akudo yaanza kuonesha upya wake

 BENDI ya muziki wa dansi ya Akudo Impact 'Vijana wa Masauti' imeanza safari nyingine katika angaza utoaji wa burudani,ambapo meneja wa bendi hiyo Ramadhani Pesambili amesema huo ni moja ya mikakati  kamambe kuongeza vionjo, mvuto na ubora wa bendi hiyo. Akizungumza blog hii katika Bonanza la bendi hiyo la kila siku za Jumapili kwenye ukumbi wa Msasani Beach, Ramadhan alisema tayari katika mipango yakuja na utoaji mpya wa burudani ulionza kufanyika hivi karibuni tumebadilisha uongozi. Alisema Meneja wa bendi hiyo ulimvua madaraka yake aliyekuwa kiongozi wa bendi hiyo awali mwanamuziki Tarsis Masela ambapo mwanamuziki mwingine toka bendi hiyo Zagreb Butamu aliteuliwa na tayari ameonesha kumudu nafasi hiyo. "Zagreb Butamu ameonesha kupendwa zaidi na wanamuziki wenzake naamekuwa na maelewano mazuri na wenzake hivyo anaonekana kumudu kwani kiongozi ni muhimu kukubalika kwanza kwa anaowaongoza,"alisema . Ramadhani alisema kuwa mambo mengi yame

Akudo yaanza kuonesha upya wake

 BENDI ya muziki wa dansi ya Akudo Impact 'Vijana wa Masauti' imeanza safari nyingine katika angaza utoaji wa burudani,ambapo meneja wa bendi hiyo Ramadhani Pesambili amesema huo ni moja ya mikakati  kamambe kuongeza vionjo, mvuto na ubora wa bendi hiyo. Akizungumza blog hii katika Bonanza la bendi hiyo la kila siku za Jumapili kwenye ukumbi wa Msasani Beach, Ramadhan alisema tayari katika mipango yakuja na utoaji mpya wa burudani ulionza kufanyika hivi karibuni tumebadilisha uongozi. Alisema Meneja wa bendi hiyo ulimvua madaraka yake aliyekuwa kiongozi wa bendi hiyo awali mwanamuziki Tarsis Masela ambapo mwanamuziki mwingine toka bendi hiyo Zagreb Butamu aliteuliwa na tayari ameonesha kumudu nafasi hiyo. "Zagreb Butamu ameonesha kupendwa zaidi na wanamuziki wenzake naamekuwa na maelewano mazuri na wenzake hivyo anaonekana kumudu kwani kiongozi ni muhimu kukubalika kwanza kwa anaowaongoza,"alisema . Ramadhani alisema kuwa mambo mengi yame

Uganda kuitisha tena mazungumzo ya Burundi

Uganda imesema itaitisha tena mazungumzo ya upatanishi ya Burundi, kufuatia machafuko yaliyoipeleka nchi hiyo ndogo kwenye kingo za vita na kuulazimu Umoja wa Afrika kujitayarisha kutuma kikosi cha kuwalinda raia. Serikali ya Burundi na pia kundi kubwa zaidi la upinzani wamekaribisha hatua ya kuanzisha tena mazungumzo hayo. Siku ya Ijumaa, (18.12.2015) Umoja wa Afrika ulisema unajiandaa kutuma kikosi cha wanajeshi 5,000 nchini Burundi kuwalinda raia, ukitumia nguvu kwa mara ya kwanza kutuma wanajeshi katika nchi mwanachama dhidi ya matakwa ya nchi hiyo. Hali ya wasiwasi umekuwa ikiongezeka nchini Burundi hasa tangu watu wenye silaha walipovamia kambi za kijeshi katika mji mkuu Bujumbura wiki iliyopita, na kuzusha hofu katika kanda hiyo ambako kumbukumbu za mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 katika nchi jirani ya Rwanda zingalipo. Burundi ilitumbukia katika mgogoro mwezi Aprili baada ya Rais Pierre Nkurunziza kutangaza mipango ya kuwan

Rais Magufuli amtimua Dkt. Edward Hosea TAKUKURU

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ametengua uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Dkt. Edward Hoseah kutokana na kutorishwa na namna taasisi hiyo ilivyokua ikitekeleza wajibu wake katika kukabiliana na rushwa hususani kwenye upotevu wa mapato ya serikali katika bandari ya Dar es Salaam. Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue amesema kufuatia kutenguliwa kwa uteuzi huo, Rais Magufuli amemteua aliyekuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Bwana VALENTINO MLOWOLA kuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU. Balozi Sefue amebainisha kuwa, Rais Magufuli amechukua hatua hiyo baada ya kujiridhisha kuwa utendaji kazi wa TAKUKURU chini ya Dkt. Edward Hoseah hauwezi kuendana na kazi anayoitaka. “Eneo mojawapo la upotevu mkubwa wa mapato ya serikali ni Bandarini na Katika Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA, Hivyo Mheshimiwa Rais amesikitishwa na kitendo cha t

Serikali yatoa siku 14 kwa Wageni walioajiriwa nchini bila kuwa na vibali halali

'WANA LAMBALAMBA'AZAM FC YATEKELEZA AGIZO LA DR. MAGUFULI KWA VITENDO

Viongozi wa benchi la ufundi la Azam Academy wakishiriki shughuli za usafi kwenye Zahanati ya Chamazi Kikosi cha Azam FC leo kimetekeleza agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Mgufuli alilolitoa majuma machache kabla ya kuadhimisha siku ya Uhuru wa Tanganyika kwamba, siku ya kuadhimisha Uhuru wa Tanganyika December 9 wananchi wote wafanye usafi kwenye maeneo yanayowazguka ili kuzuia magonjwa mbalimbali yasababishwayo na uchafu. Katika kutekeleza agizo hilo la Rais Magufuli, kikosi cha Azam FC kwa kushirikiana na wananchi leo kimefanya usafi kwenye Zahanati ya Chamazi iliyopo eneo la Chamazi-Mbande, Manispaa ya Temeke kwa kusafisha mazingira yanayoizunguka zahanati hiyo. Wachezaji wakimwaga taka baada ya kusafisha mazingira yanayozunguka eneo la Zahanati ya Chamazi Asilimia kubwa ya wachezaji, makocha na viongozi wengine walikuwa wanatoka katika kikosi B kutokana na kikosi cha kwanza kuwa kwenye maandalizi ya mchezo wa ligi kuu dhid

Hatari

Tupia macho kusoma mambo ya Samuel L Jackson

Samuel L Jackson ni mmoja wa Wamarekani weusi waliofanikiwa sana Hollywood Nyota wa Hollywood Samuel L Jackson atahamia Afrika Kusini iwapo Donald Trump atashinda uchaguzi wa urais Marekani, tovuti ya News 24 imeripoti. Trump, mmoja wa wanaowania tiketi ya kugombea urais Marekani kupitia chama cha Republican, ameshutumiwa vikali baada ya kupendekeza Waislamu wazuiwe kuingia Marekani. Haijabainika iwapo matamshi ya mwigizaji huyo, yaliyopeperushwa kwenye sehemu ya kipindi cha Jimmy Kimmel Live iliyorekodiwa awali Jumatatu, yalitolewa kabla au baada ya matamshi hayo ya majuzi zaidi kutoka kwa Trump. Trump akemewa kwa kutaka Waislamu wasiingie Marekani Bw Trump, wakati mmoja amewahi kunukuliwa akikosoa kundi linalotetea haki za watu weusi Marekani la Black Lives Matter. BBC

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana azungumza na waandishi

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, akizungumza na waandishi wa habari jana Desemba 8, 2015, katika Ukumbi wa Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam. (Picha na Bashir Nkoromo) Juzi tarehe 07/12/2015 Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa ilifanya kikao chake cha kawaida mjini Dar es salaam kwa siku moja. Kikao hicho kiliongozwa na Mwenyekiti wa CCM, Rais mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete. Kamati Kuu pia ilipokea taarifa juu ya utendaji wa Serikali katika utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015-2020. Kwa ujumla na kwa kauli moja Kamati Kuu ya CCM Taifa iliipongeza Serikali ya Awamu ya Tano chini ya uongozi wa Rais Dkt. John Pombe Magufuli, Makamu wa Rais Mheshimiwa Samia Suluhu na Waziri Mkuu Mhe. Kassim M. Majaliwa kwa kasi nzuri waliyoanza nayo katika

Soma Stori ya Sanamu hii

DBanj alalama kuibiwa idea

Producer wa muziki wa msanii DBanj ‘Deevee’ ametoa malalamiko yake juu ya msanii ambaye ana imani kuwa anawaibia mawazo yao ya muziki. Deevee ametoa malalamiko kuwa rapa Mnigeria Olamide amekuwa akiiba idea za muziki wake na D’banj kila anapoenda kuwatembelea. Deevee aliandika habari hizi za kushtua kwenye kurasa yake ya twitter. Deevee pia amemuomba boss wake D’Banj msamaha kwa kuweka wazi habari hii. With due respect @olamide_YBNL, hav u ran out of ideas? Everytym u come 2 our zones u always gotta steal some idea..I won’t let this fly — #OminiProducer (@IamDeeveeLee) December 4, 2015. I’m vry sry boss @iamdbanj I mean no disrespect but i hv stayd silent 4 too long & I’m ready 2 face d consequences, for dropping the #OminiProducer (@IamDeeveeLee) December 4, 2015. Deevee, anasema Olamide ameiga wazo la wimbo “Shake It” wa DBanj.

NYOTA WA TANZANIA SAMATTA, ULIMWENGU WAMFUATA LIONEL MESSI.

Kikosi cha  TP Mazembe, leo kinakamata pipa kuanza safari ya kwenda nchini Japan. Watanzania wawili, Mbwana Samatta na mshkaji wake, Thomas Ulimwengu watakuwa sehemu ya msafara huo wa mabingwa hao wa Afrika kwenda kucheza michuano ya Kombe la Dunia kwa klabu. Ulimwengu amezungumza kutoka Lubumbashi na kusema: "Tunaondoka kesho (leo), mimi pia nipo vizuri. Kweli niliumia kidogo lakini nimepata matibabu na sasa niko vizuri." Wawili hao wanaendelea kuweka rekodi kwa mara nyingine ya kuwa Watanzania wa kwanza kucheza michuano ya Kombe la Dunia kwa klabu. Mazembe ya DR Congo, inacheza michuano hiyo baada ya kubeba ubingwa wa Afrika kwa kuifundisha kazi USM Alger ya Algeria kwa kuifunga mechi zote mbili za nyumbani na ugenini.

WACHEZAJI AZAM FC KUKATWA MISHAHARA.

Kocha Mkuu wa Azam FC, Stewart Hall, amewachimba mkwara wachezaji wa timu hiyo kuelekea mchezo dhidi ya Simba kwa kuwataka wasizungumze na na mtu yeyote wa nje ya Azam FC kuhusiana na mechi hiyo ambayo presha yake imeshaanza kupanda. Simba na Azam FC zinatarajia kukutana wikiendi hii katika Uwanja wa Taifa huku kukitarajiwa kuwa na upinzani mkali katika mechi hiyo ambayo kila upande utahitaji kushinda ili kujiweka katika nafasi nzuri zaidi ya msimamo wa ligi. Msemaji wa Azam FC, Jaffar Idd, ameeleza kuwa kocha amewataka wachezaji wote kutozungumza na mtu yeyote kuelekea mchezo huo na atakayebainika amezungumza atakatwa mshahara. “Kocha amewakataza wachezaji wote wa Azam kuzungumza kitu kuelekea mchezo wetu dhidi ya Simba na hata mchezo mwingine wowote, jambo hili limeandikwa hata kwenye mikataba yao, yeyote atakayekiuka agizo hili atakatwa mshahara. “Tumejiandaa vyema kuelekea mchezo huo na baada ya kurejea Tanga tutaweka kambi ya pamoja na wachezaji tulio

Kanye West na Kim watangaza jina la mtoto wao wa kiume

Kim na Kanye West wametangaza jina la mtoto wao wa kiume Kim Kardashian ametangaza kwamba yeye na Kanye West wamempa mtoto wao wa kiume jina Saint. Kim alitakiwa kujifungua Saint siku ya Krismasi lakini mtoto huyo amewasili wiki tatu kabla. Kanye hupenda kujiita Yeezus wakati akiimba, na aliachiwa wimbo “I Am God” mwaka 2013.

Wasome nyota wa soka waliobeba tuzo La Liga

Neymar Jr akiwa ameshika tuzo ya mchezaji bora wa La Liga katika mwezi Novemba. Mshambuliaji wa klabu ya Barcelona, Neymar Jr 23, ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa La Liga wa mwezi Novemba na kuweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza wa Barca kuchukua tuzo hiyo tangu kuanzishwa kwake Septemba 2013. Neymar Jr ambaye ni kinara wa magoli La Liga mpaka sasa, amechukua tuzo hiyo baada ya kufunga magoli matano katika mechi 3 alizocheza katika mwezi huo. Diego Simeone Wakati huohuo kocha wa klabu ya Atletico Madrid, Diego Simeone, amechukua tuzo ya Kocha bora wa mwezi Novemba katika La Liga baada ya kushinda mechi zote 3 za Ligi hiyo katika huo, hii ni mara ya pili Muargentina huyo anashinda tuzo hiyo.

Nape amwaga pikipiki Mtama

Mbunge wa Jimbo la Mtama Ndugu Nape Nnauye akimkabidhi Katibu wa Kata ya Mtua Kilimahewa Ndugu Maliki funguo ya pikipiki kwa niaba ya makatibu kata 20 wa jimbo hilo ambao wote wamewezeshwa usafiri wa pikipiki ili kurahisisha ufanisi wa kazi zao Mbunge wa Jimbo la Mtama (CCM) Nape Nnauye akijaribu moja ya pikipiki kati ya 20 alizowapa makatibu kata ili ziweze kuwasaidia kufanya kazi kwa ufanisi kwenye shughuli zao za kujenga na kuimarisha Chama Cha Mapinduzi Sehemu ya pikipiki zilizotolewa na Mbunge wa Jimbo la Mtama Ndugu Nape Nnauye kwa makatibu kata 20 wa jimbo hilo Mbunge wa Jimbo la Mtama Ndugu Nape Nnauye akizungumza mbele ya viongozi wa CCM wilaya ya Lindi vijijini ambapo aliwaambia viongozi hao kuwa amejipanga kufanya kazi katika jimbo hilo zenye kuleta tija na kuhakikisha anatekeleza ahadi zote alizozitoa wakati wa kampeni na kuwata makatibu kata waliokabidhiwa pikipiki 20 kuzitumia katika kazi za kujenga na kuimarisha chama. Pic

Manji amwandikia barua Magufuli

Mwenyekiti wa Kampuni ya Quality Group Yusuf Manji Mwenyekiti wa kampuni ya Quality Group, Yusuf Manji amemwandikia barua Rais John Magufuli kumuelezea mchakato wa zabuni aliyoshinda kuendeleza ufukwe wa Coco maarufu kama Coco Beach uliopo Kinondoni. Taarifa iliyotolewa na kampuni hiyo kwa vyombo vya habari jana ilisema Manji aliandika barua hiyo Desemba 5 mwaka huu akimuelezea kiongozi huyo wa nchi usahihi wa mchakato wa zabuni ya kuendeleza eneo hilo akiwa ameambatisha majibu ya pendekezo la mradi huo kuwa lilitakiwa kutekelezwa na kampuni tanzu ya QGL, Q Consult Ltd. Alisema kampuni hiyo ilishinda zabuni kwa kufuata masharti na vigezo vilivyokuwa vimependekezwa na Manispaa ya Kinondoni. Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Manji katika barua hiyo alionekana “kuisemelea” Manispaa hiyo kuwa Januari 20 mwaka huu QCL aliiandika barua yenye kumbukumbu namba QCL/KMC/01/15 ili kusuluhisha kesi hiyo iliyokuwa mahakamani kwa muda mrefu, la