Mbunge
wa Jimbo la Mtama Ndugu Nape Nnauye akimkabidhi Katibu wa Kata ya Mtua
Kilimahewa Ndugu Maliki funguo ya pikipiki kwa niaba ya makatibu kata 20
wa jimbo hilo ambao wote wamewezeshwa usafiri wa pikipiki ili
kurahisisha ufanisi wa kazi zao
Mbunge
wa Jimbo la Mtama (CCM) Nape Nnauye akijaribu moja ya pikipiki kati ya
20 alizowapa makatibu kata ili ziweze kuwasaidia kufanya kazi kwa
ufanisi kwenye shughuli zao za kujenga na kuimarisha Chama Cha Mapinduzi
Sehemu ya pikipiki zilizotolewa na Mbunge wa Jimbo la Mtama Ndugu Nape Nnauye kwa makatibu kata 20 wa jimbo hilo
Mbunge
wa Jimbo la Mtama Ndugu Nape Nnauye akizungumza mbele ya viongozi wa
CCM wilaya ya Lindi vijijini ambapo aliwaambia viongozi hao kuwa
amejipanga kufanya kazi katika jimbo hilo zenye kuleta tija na
kuhakikisha anatekeleza ahadi zote alizozitoa wakati wa kampeni na
kuwata makatibu kata waliokabidhiwa pikipiki 20 kuzitumia katika kazi za
kujenga na kuimarisha chama. Picha na Adam Mzee
Comments