Mshambuliaji wa klabu ya Barcelona, Neymar Jr 23, ameshinda tuzo ya
mchezaji bora wa La Liga wa mwezi Novemba na kuweka rekodi ya kuwa
mchezaji wa kwanza wa Barca kuchukua tuzo hiyo tangu kuanzishwa kwake
Septemba 2013.
Neymar Jr ambaye ni kinara wa magoli La Liga mpaka sasa, amechukua
tuzo hiyo baada ya kufunga magoli matano katika mechi 3 alizocheza
katika mwezi huo.
Wakati huohuo kocha wa klabu ya Atletico Madrid, Diego Simeone,
amechukua tuzo ya Kocha bora wa mwezi Novemba katika La Liga baada ya
kushinda mechi zote 3 za Ligi hiyo katika huo, hii ni mara ya pili
Muargentina huyo anashinda tuzo hiyo.
Comments