Skip to main content

Posts

Showing posts from December, 2017

George Weah, mshindi wa duru ya pili ya uchaguzi wa urais

Makamu wa rais Joseph Boakai akubali kushindwa Liberia J Makamu wa rais waLiberia Joseph Nyuma Boakai ampongeza George Weah kwa ushindi wake Desemba 29, 2017 katika hotuba alioitoa Monrovia, mji mkuu wa Liberia Siku moja baada ya tume ya uchaguzi nchini Liberia NEC kumtangaza nyota wa zamani wa Soka, George Weah, mshindi wa duru ya pili ya uchaguzi wa urais nchini humo, makamu wa rais Joseph Nyuma Boakai amekubali kushindwa na kumpongeza mpizani wake. George Weah alishinda kwa 61.5% ya kura , huku mpinzani wake, Makamu wa rais Joseph Boakai akipata 38.5% , Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) ilitangaza. Weah atachukua nafasi ya Ellen Johnson Sirleaf ambaye alikuwa rais wa kwanza mwanamke barani Afrika kuchaguliwa kidemokrasia na sasa anatarajiwa kukabidhi madaraka kwa amani. Rais Sirleaf alimshinda Weah katika uchaguzi wa duru ya pili uliofanyika mwaka 2005, baada ya kumalizika kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu kwa miongo kadhaa nchini humo. Punde baada ya

Sikia mapya ya Asia Utamu

MWANAMIPASHO Asia Utamu ameweka wazi kuwa hana posti kwenye mitandao ya kijamii kuhusiana na tukio la siku yake ya kuzaliwa kutokana na ukweli wa simanzi na majonzi uliojificha kwenye siku hiyo. Asia amesema kuwa kwa upande wake ni siku iliyotengeneza historia ambayo inabaki kuwa kumbukumbu katika muda wake wote atakaoishi ulimwenguni ambapo amesema kuwa amepanga kufunguka zaidi mwezi Januari, mwaka ujao. “Jina langu la pili naitwa FARAJA, ili mjue kwanini sisherehekei tukio la kuzaliwa kwa tarehe husika ntawajuza rasmi Januari tarehe za mwanzo ndo nimepanga kusherehekea, nasikitika sana ni siku ya kuzaliwa lakini ina siri nzito mpaka nimebakia mpweke,” amesema Asia. “Ewe Mola wangu mpe mama yangu kitabu chake kwa mkono wa kulia, jaman machungu yakipita tukiwa hai mtakula keki msiwazee,” ameongeza mwimbaji huyo aliyepata kutamba na kibao cha “Sioni Thamani ya Pendo”.

Thierry Henry sasa ni mchambuzi wa soka, ataja namna magoli ya Alexis Sanchez dhidi ya Crystal

Nyota wa zamani wa Arsenal,  Thierry Henry ambaye kwa sasa ni mchambuzi wa soka, amesema namna magoli ya  Alexis Sanchez dhidi ya  Crystal Palace   yalivyokuwa na mapokeo baridi kutoka kwa wachezaji wenzake, inaonyesha kuna mgawanyiko ndani ya kikosi cha Arsene Wenger. Sanchez anayehuhishwa na usajili wa kwenda Manchester City, alifunga mara mbili katika ushindi wa 3-2 kwenye dimba la  Selhurst Park Alhamisi usiku. Thierry Henry  anasema hakufurahishwa na namna wachezaji wa Arsenal walivyoshangilia mabao ya Sanchez katika mchezo huo wa Ligi Kuu ya England. "Kuna mgawanyiko wa wazi, Sanchez alionyesha ishara ya kuwaita wenzake, lakini hawakwenda, sielewi kwanini walifanya hivyo, walikuwa hawataki kushangilia?" alihoji Thierry. "Hauko pale kwaajili ya Sanchez, uko pale kwaajili ya Arsenal, nenda kashangilie bila kujali nani amefunga, sherehekea na wachezaji wenzako. "Pengine tunachunguza sana juu ya hili, lakini nilibaini mgawanyiko, San

Jeshi la polisi kanda maalum ya Dar es salaam leo limetoa takwimu ya matukio ya uhalifu ambayo yameripotiwa kwa mwaka 2017

Kamanda wa Jeshi la Polisi Kanda maalum ya Dar es salaam Lazaro Mambosasa akizungumza na wanahabari Jeshi la polisi kanda maalum ya Dar es salaam leo limetoa takwimu ya matukio ya uhalifu ambayo yameripotiwa kwa mwaka 2017 kuwa ni Laki moja na elfu 26 na miambili ukilinganisha na mwaka 2016 ambayo yalikuwa ni laki moja na 29 miasita na mbili. Kamanda wa Jeshi la Polisi Kanda maalum ya Dar es salaam Lazaro Mambosasa ametoa takwimu hiyo wakati akizungumza na wanahabari hii leo ambapo amesema kulinganisha data hizo kuna upungufu wa matukio elfu mianne na tano sawa na 2.6%.

Florian Mkeya:Ni vyema watu wakaiheshimu misitu kwani inasaidia vizazi vya leo na baadae

Watanzania wametakiwa kuitunza na kuithamini misitu ikiwemo kuepuka kuikata hovyo  ili kuondokana na changamoto ya ukosefu wa mahitaji muhimu yanayotokana na misitu. Afisa Misitu wa wakala wa Huduma za Misitu Tanzania Florian Mkeya ameyaeleza hayo leo wakati akizungumza na chanzo kimoja cha habari  jijini Dar es salaam ambapo amesema ni vyema watu wakaiheshimu misitu kwani inasaidia vizazi vya leo na baadae. Mkeya amesema hakuna mahali ambapo watu hawategemei misitu hivyo watu wanapaswa kuepukana na uharibifu wa ukataji wa misitu na kuchoma mikaa pasipo kufata taratibu za upandaji wa miti. Amesema misitu inasaidia nyanja mbalimbali hapa nchini ikiwa ni pamoja na kuendeleza shughuli za utalii unaotokana na mazingira halisia ya misitu. Afisa Misitu Mkeya amesema kuanzia mwaka 2015 walipata ufadhili kutoka shirika la maendeleo la Dunia la UNDP kwa lengo la kuboresha miundombinu ya usimamizi wa bayanuai katika mtandao wa misitu 12 ya asilia ili kutangaza vivutio mbalim

winga wa kimataifa wa Tanzania, Simonafunga bao pekee

BAO pekee la winga wa kimataifa wa Tanzania, Simon Happugod Msuva leo limeipa ushindi wa 1-0 Difaa Hassan El-Jadidi dhidi ya Hassania Agadir katika mchezo wa Ligi Kuu ya Morocco, maarufu kama Botola. Msuva, mchezaji wa zamani wa Yanga alifunga bao hilo dakika ya 52 katika mchezo uliofanyika Uwanja wa Ben Ahmed El Abdi mjini El Jadida, Mazghan nchini Morocco.   Huo ni mwendelezo mzuri kwa Msuva tangu ahamie  \ Morocco kufuatia kuwika katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kwa kuwa Mfungaji Bora na Mchezaji Bora. Kikosi Difaa Hassan El Jadida kilikuwa; Yahia El Filali, M. Hahdhoudhi, Y. Aguerdoum, Bacary N’diaye, Anouar Jayid, Adil El Hasnaoui, Tarik Astati, Fabrice Ngah, Simon Msuva/Ayoub Nanah dk75, Bila El Magri/Mario Mandrault dk75 na Adnane El Quardy. 

YANGA MWANZA WAJITOLEA KUSAJILI WACHEZAJI 10

WANACHAMA wa matawi ya Yanga mkoani Mwanza wamekutana katika mkutano wao wa mwisho wa mwaka wenye lengo la kujadili mustakabali na mwenendo klabu yao katika msimu huu. Katika mkutano huo uliohudhuriwa na Kaimu Mwenyekiti wa Yanga,  Clement Sanga wanachama hao kupitia kwa Mwenyekiti wa Matawi hayo, Salehe Akida wamedhamiria kufanya harambee katika matawi yote ya Mkoa wa mwanza ili kuhakikisha wanapata fedha za kuwawezesha kusajili wachezaji 10 katika msimu ujao kama nia na lengo la kuweza kua karibu na timu yao. "Hakika tumedhamiria kufanya makubwa katika msimu ujao kwa kuweza kuyafanya matawi yetu ya wanachama wa Mwanza kuwa yakuigwa na kuwa mfano katika matawi yote Tanzania". katika hatua nyingine wanachama hao wanechangishana fedha tasilimu shilingi laki tisa na elfu thelathini kwa lengo la kuwapa motisha wachezaji kuweza kujituma katika mchezo wao wa ligi kuu Tanzania bara dhidi ya Mbao FC utaokaochezwa siku ya jumapili kwenye uwanja wa ccm kirumba mwanza

JESHI LA POLISI LASEMA LITAMUHIJI ASKOFU KAKOBE

Askofu Zakaria Kakobe Licha  ya kutokiri moja kwa moja juu ya taarifa zinazosambaa mitandaoni kuhusu kumkamata Askofu Zakaria Kakobe wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship (FGFC) lililoko Mwenge jijini Dar es Salaam, Jeshi la Polisi limesema ni lazima litamhoji kiongozi huyo wa kiroho. Kuhojiwa huko kumetokana na kauli yake dhidi ya serikali aliyoitoa wakati wa ibada ya Krismasi. Jana, kulienea taarifa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii kueleza kwamba askofu huyo alitiwa mbaroni jana asubuhi na askari wa Jeshi la Polisi huku sababu za kukamatwa zikielezwa kuwa ni ujumbe alioutoa wakati wa mahubiri yake ya ibada ya Krismasi. Akizungumza na Nipashe jana kuhusiana na ukweli wa taarifa za kutiwa mbaroni kwa Askofu Kakobe, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa, alisema kuwa ni kweli walishakuwa katika harakati za kumkamata. "Ametoa maneno ya kashfa katika mahubiri yake, lakini sina taarifa kama amekamatwa,"   Kamanda Mam

JESHI LA POLISI USALAMA BARABARANI LATOA TAKWIMU ZA SIKUKUU

Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Kamanda Fortunatus Musilimu(picha na mtandao) Katika Kuelekea mwisho wa mwaka 2017 Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani limetoa twakimu za sikukuu ya krismas ya mwaka huu zikionyesha kumetokea jumla ya ajali 10 zilizosababisha vifo 5 na majeruhi 11 zikilinganishwa na takwimu za mwaka jana za krismas. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salama Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Kamanda Fortunatus Musilimu amesema kutokana na takwimu hizo amewatoa hofu watanzania wanaotumia barabara na kuwahakikishia kuwa kupitia operesheni ya KA-MA-TA itasaidia kupunguza ajali barabarani. Musilimu amesema kuwa wamejipanga kweli kweli  kuwadhibiti madereva wazembe na wamejitahidi kupunguza ajali huku akitolea mfano siku ya leo kuwa zimetokea ajali 3 tu. Pia amewahakikishia watu wote wanaosafiri katika kipindi hiki cha sikukuu kuwa watasafiri salama bila tatizo lolote huku akiwataka madereva wanaoendesha vyombo vya mot

TFF yalamba mkataba wa mamilioni

Rais wa TFF, Wallace Karia, kulia kwenye picha akikabidhiana mkataba na Viongozi wa Kampuni ya Macron. Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), limetangaza kuingia mkataba mkataba wa miaka miwili na kampuni ya vifaa vya michezo ya Macron. Kwenye mkataba huo Macron itakuwa ikitengeneza jezi kwa ajili ya timu ya wakubwa, Taifa Stars na zile za wanawake pamoja na vijana. Akitaja kiasi cha fedha walichopata kwenye mkataba huo, Rais wa TFF, Wallace Karia amesema mkataba huo utagharimu kitita cha Tsh milioni 800 kwa miaka hiyo miwili. Karia amesema kampuni hiyo itakuwa ikiwatengenezea vifaa mbalimbali vya michezo ikiwemo jezi za timu za mpira wa miguu za taifa.  

Baraka The Prince amefunguka amechoshwa na mtu ambaye anamfanyia hujuma katika mtandao wake wa 'Youtube'

Baraka The Prince amefunguka na kusema kuwa amechoshwa na mtu ambaye anamfanyia hujuma katika mtandao wake wa 'Youtube' na kuamua kutangaza dau la milioni tatu kwa mtu ambaye anaweza kumgundua mtu ambaye anapunguza watazamaji wake kwenye mtandao huo. Baraka awali alikuwa akilalamika akionyesha kuwa mtu ambaye anamfanyia hujuma hizi anamtambua kuwa ni moja kati ya viongozi wake ambao walikuwa wakimsimamia katika kazi zake za muziki.  "Kwanza nishukuru sana mashabiki zangu mnaojitahidi kunipigania na kupoteza muda wenu kwa ajili ya kazi lakini kuna mtu mmoja tu ambae aliumbwa kurudisha nyuma hatua za watu. Kila siku 'viwes' wanazidi kupungua sasa basi natangaza kumpa zawadi ya Tsh Milioni 3 kwa yeyote atakayetuthibitishia na kutuletea uyu mtu" aliandika Baraka The Prince  Aidha Baraka aliendelea kulalamika "Maana huku ni kudharau kazi yangu na kudharau muda wa mashabiki zangu, Radio na Tv na vyombo vyote vya habari ambavyo vimenipigania

takriban watoto 100 wamekamatwa kufuatia uvamizi wa shule moja inayofunza dini ya Kiislamu nchini Kenya

Baadhi ya wahubiri na takriban watoto 100 wamekamatwa kufuatia uvamizi wa shule moja inayofunza dini ya Kiislamu nchini Kenya kulingana na vyombo vya habari nchini humo. Haijulikani ni kwa nini uvamizi huo katika mji wa likoni pwani mwa Kenya ulifanyika . Hatahivyo ripoti kadhaa zinasema kuwa vikosi vya usalama vya kimataifa vilihusika huku Marekani na Uingereza zikidaiwa kuhusika. Vyombo vya habari vinahusisha uvamizi huo na eneo moja la kukuza ugaidi mbali na biashara haramu ya kusafirisha watoto inayohusisha mataifa kadhaa na mabara. Gazeti la The Star liliripoti kwamba watoto hao ni wa hadi umri wa miaka mitano na wanatoka umbali wa Marekani, Uingereza na Canada pamoja na mataifa mengine ya bara Afrika. Duru moja ya polisi ambayo imekataa kutajwa iliambia chombo cha habari cha Reuters kwamba shule hiyo ya madrassa ilikuwa kituo cha kuwapatia wanafunzi mafundisho ya kuwa na itikadi za wapiganaji na kimekuwa kikichunguzwa kwa mara kadhaa. Sheikh Hassan Omar, ambaye ni af

DRC: Mkutano kati ya rais Kabila na magavana wamalizika Goma

Rais wa DRC Joseph Kabila Rais JOSEPH KABILA pamoja na viongozi wa ngazi za juu nchini DRC, waliokutana jijini GOMA tangu jumatatu wamehitimisha mkutano wao usiku wa kuamkia leo huku wakiwataka raia wa nchi hiyo kutojihusisha wala kujiunga na makundi ya waasi yanayotatiza usalama kwenye eneo la mashariki mwa nchi hiyo. "Tumewaalika raia wa Congo kuilinda nchi yao piya twa shukuru wana jeshi ambao hivi sasa wajitahidi katika ulinzi wa raïa wilayani KASAI." Huko magaavana walio shiriki mkutano huo walijulisha umuhimu wa mazungumzo yao dhidi ya raïa wa Congo DRC, kama alivyo julisha LOLA KISANGA liwali wa Jimbo la UELE. "Twatazama yote tukiona jinsi gani usalama wa kweli waweza rejea na kusaidia kwa ujenzi bora wa nchi yetu" Raia wamepokeaje yaliyo zungumziwa jijini Goma na viongozi serikali ya Congo DRC ! "Ikiwa hakuna upendo haya yote ni kupoteza mda.cha maana magavana hao watimize waliyo zungumza." Licha ya kutozungumza na wanahabari k

Je, rais Zuma atang'atuliwa madarakani kufuatia mabadiliko ya uongozi wa ANC?

Image caption Jacob Zuma amekuwa Rais wa ANC kwa miaka kumi sasa Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma inawezekana asimalize muhula wake wa mwisho madarakani baada ya chama cha ANC kumchagua Cyril Ramaphosa kama kiongozi wake mkuu. Kwa kipindi cha miaka kadhaa iliyopita, Ramaphosa alikua rafiki wa karibu wa Zuma na hata msaidizi wake, lakini uhusiano wao umekua wa mashaka siku za karibuni. Ramaphosa anasema atapambana na rushwa jambo ambalo kwa Zuma limekua kama mzigo. Hivi ni vitu vichache ambavyo vinaweza kujitokeza kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2019:

Idd Pialali atwanga Shiva kutoka India

Bondia Mtanzania, Idd Pialali amsema amefurahia  wake kufuatia  kushinda mkanda wa ubingwa wa kimataifa wa ujulikanao kwa jina la ( UBO) baada ya  kumchapa mpinzani wake Shiva ambaye ni raia wa India  pointi kwenye Ukumbi wa Travel Lodge ambao pia wanatajwa kuwa wadhamini katika pambano hilo lililofanyika wilayani Bagamoyo mwisho wa wiki iliyopita. Pialali amliambia gazeti hili jana kuwa  pambano hilo lilikuwa kubwa  na kuwa ni mara ya kwanza kufanyika  Bagamoyo ingawa awali alisha pamana  wilayani humo,  lilianza kwa mabondia kucheza kwa tahadhari kutokana na kusomana. Alisemma licha ya kibuka na ushindi huo  amedodosa kuwa  ameshinda pambano hilo ila lilikwenda nje na mipango yake kwani alikuwa akiitaji ushndi wa mapema zaidi hila mpinzani wake kutoka India alikuwa makini hali iliyomfanya kusogeza zaidi raundi katika mpambano. "Nilikuwa nimeisha jiandaa miezi michache baada ya kuibuka na ubingwa wa Global Tv, Afrika Mashariki nakati siku chache tu hivyo ilikuwa ni mpa