Nyota wa zamani wa Arsenal, Thierry Henry ambaye kwa sasa ni mchambuzi wa soka, amesema namna magoli ya Alexis Sanchez dhidi ya Crystal Palace yalivyokuwa na mapokeo baridi kutoka kwa wachezaji wenzake, inaonyesha kuna mgawanyiko ndani ya kikosi cha Arsene Wenger.
Sanchez anayehuhishwa na usajili wa kwenda Manchester City, alifunga mara mbili katika ushindi wa 3-2 kwenye dimba la Selhurst Park Alhamisi usiku.
Thierry Henry anasema hakufurahishwa na namna wachezaji wa Arsenal walivyoshangilia mabao ya Sanchez katika mchezo huo wa Ligi Kuu ya England.
"Kuna mgawanyiko wa wazi, Sanchez alionyesha ishara ya kuwaita wenzake, lakini hawakwenda, sielewi kwanini walifanya hivyo, walikuwa hawataki kushangilia?" alihoji Thierry.
"Hauko pale kwaajili ya Sanchez, uko pale kwaajili ya Arsenal, nenda kashangilie bila kujali nani amefunga, sherehekea na wachezaji wenzako.
"Pengine tunachunguza sana juu ya hili, lakini nilibaini mgawanyiko, Sanchez alinifanya nibaini hilo, ilikuwa ni kama vile alikuwa peke yake".
Hata hivyo tayari baadhi ya wachezaji wa Arsenal wamepinga vikali madai hayo ya Thierry.
Comments