watu waliojaribu kulifukua kaburi la marehemu Ivan Ssemwanga lililoko katika kijiji cha Nakaliro usiku wa Jumanne iliyopita ili kuutoa mwili wake. Ssemwanga alizikwa kijijini kwao huko Mei mwaka huu katika mazishi yaliyokuwa na shamrashamra kibao.
Habari zilizopatikana kutoka kwa mmoja wa ndugu zake zimesema waliofanya hivyo walikuwa wamelenga kulichukua fuvu lake. Kaburi lake lilikuwa likilindwa na polisi kuzuia watu wasilifukue na kuchukua fedha ambazo zilitupwa ndani ya kaburi hilo na marafiki zake waliokuwa wanajiita “kundi la matajiri”.
“Nilikuwa nikipita karibu na kaburi majira ya saa saba mchana na niliona shimo kwenye kaburi la Ssemwanga. Nilisogea karibu kuona nini kilikuwa kimetokea,”alisema Ali Wamala, mmoja wa ndugu wanaoishi nyumbani hapo. Hata hivyo, alidai kwamba huenda waganga wa kienyeji walikuwa nyuma ya njama za kuufukua mwili wa Ssemwanga.
Polisi walililinda kaburi hilo kwa zaidi ya mwezi mzima. Naye Naibu Mkuu wa wilaya hiyo, Yahaya Were, amesema upelelezi umeanza na watuhumiwa watakaokamatwa watafikishwa mahakamani. “Hili ni suala la usalama na polisi wameanza uchunguzi dhidi ya watu wanaotaka kuharibu amani ya wafu,” aliongeza Were.
Tangu kuzikwa kwa Ssemwanga, ndugu zake walikodi walinzi kulinda kaburi hilo lakini habari za kuaminika zimesema walishindwa kuwalipa mishahara yao kwa mujibu wa makubaliano yaliyofikiwa. Inasemekana walinzi hao mwezi wa kwanza walilipwa Sh. 600,000 mbali na kwamba walikuwa wamekubaliana kuwalipa Sh. milioni moja.
Comments