mmea wa Tumbaku
Dar es salaam ,Chama cha kudhibiti Tumbaku Tanzania (TTCF) na washirika wake wameiomba Serikali kusitisha kilimo cha Tumbaku nchini ili kupunguza vifo vinavotokea kila mwaka.
Pia ametumia fursa hiyo kumuuomba Waziri wa Kilimo, Dk Charles Tizeba kushirikiana na wizara ya afya maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto ili kuelimisha umma juu ya madhara ya matumizi ya tumbaku,kuwaokoa vijana dhidi ya matumizi ya tumbaku,kusaidia wakulima kupata masoko bora na endelevu kwa ajili ya mazao yao mbadala na kuwapatia msaada wakulima wanaoendelea na kilimo cha tumbaku ili waweze kuachana na kilimo hiko na kujikita kwenye kilimo mbadala.
Katika hatua nyingine mkurugezi wa (TTCF) Kagaaruki amezungumzia Mkataba wa kimataifa wa kudhibiti Tumbaku wa Shirika la Afya Ulimwenguni (WFCTC) ambao Tanzania iliridhia Mkataba huu Aprili 2007 miaka 10 iliyopita,ina wajibu wa kuutekeleza,ili kulinda watu wake.
Comments