Pichani kutoka kushotoni Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Taasisi hiyoAlhaj Suleiman Seif Nassor na kulia ni Katibu wa bodi hiyo Abduil RashldShenkh walipokuwa wakizungumza Dar es Salaam juu ya kujenga chuo Kikuu
kitakacho gharimu Shilingi bilion mbili za kitanzania nchini.
TAASISI ya Ridhwaa-Kinondoni ya Jijini Dar es Salaam Tanzania imewaombawadau mbali mbali waelimu na watanzania wenye uzalendo kujitokeza kuchangia mpango wa kujenga chuo Kikuu kitakacho gharimu Shilingi bilion
mbili za kitanzania ikiwa ni moja ya mikakati yao katika taasisisi hiyo kueneza
elimu nchini.
Akizungumza na mwandishi wa gazeti hili hivi karibuni Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi hiyo alhaji Suleiman Seif alisema watanzania wenye moyo wa uzalendo
amewaomba kujitokeza katika ujenzi wa chuo
Taasisi hiyo iliyosajiriwa miaka 25 iliopita kwa jina la The Registered Trustees of Masjid Ridhwaa(RTMR) yaani Bodi ya Wadhamini ya Ridhwaa Seminari ikiwa na lengo
la kujenga mskiti,kujenga vituo vya afya,vituo vya elimu na kuendesha miradi ya kiuchumi kwakuzingatiamisingi ya kiislaam.
Baada ya mafanikio makubwa Taasisi hiyo iliyo yapata kwakupitia shule ya Ridhwaa,Taasisi hiyoina wiwa kuanzisha Chuo kikuu ambacho kitatutumika kuelemisha umma
kwamapana zaidi nakuzalisha wataalamu katika nyanja mbali mbali nchini.
Hata hivyo Katibu wa Bodi hiyo Sheikh Abdul Rashid amesema kuwa ili kuunga mkono kauli ya Rais wa awamu ya tano Mh John Pombe Magufuli kuelekea uchumi
wakati na wa viwanda.
"Pamoja nakwamba Taasisi yetu toka kuanzishwa kwake ilikuwa na malengo ya kimkakati ya kuanzisha Chuo kikuu cha aina yake lakini tumeona tuendane na
kasi ya Mh Rais ili kabla hajaondoka madarakani Chuo hicho kitakachotambulika kwa jina la Musilim University of Tanzania (Chuo Kikuu Cha Kiislam Tanzania)
kiwe kimekwisha kamilika.
Hadi sasa Mradi wa ujenzi wa chuo hicho umefanikiwa kukamilisha ghorofa moja kati ya ghorofa tano zinazo hitajika Sanjari na hilo tayari zipo ekari 23 katika kijiji cha Kisemvule wilayani Mkuranga kwa ajiri ya maendeleo ya taasisi hiyo.
Katibu huyo amewataka wasamalia wema na wenye
mapenzi na Taasisi hiyo kuwaunga mkono katika michango ili kuweza kufanikisha jenzi wa Chuo hicho ambacho ujenzi wake unakadiriwa kuchukuwa miaka miwili hadi kukamilika kwake kulingana na upatikanaji wa fedha.
"Rai yangu kwa wapenda maendeleo,waislaam,Taasisi mbali mbali za fedha na zile zisizo za fedha,serikalini na hata kwa watu binafsi wanayo nafasi kubwa yakuchangia maendeleo ya chuo hicho kwani mwisho wa siku kitawafaa watanzania wote."
Mpango mkakati wa Chuo hicho nikutoa wahitimu watakao jiajiri wao wenyewe, nakutoa ajira kwa wengine.Huo ndiyo mpango mkakati wa kuanzishwa kwa chuo hicho kulingana na mabadiriko ya soko la ajira duniani.
Ulimwenguni kote watu wanatoa elimu itakayo mfanya mtu ajiajiri badala yakusubiri ajira toka serikalini au kwa mabepari ni wakati wa watanzania kuandaa mazingira ya
kujiajiri.
Kutokana na ukweli usiopingika Taasisi ya Ridhwaa imeona hii ni fursa itakayo saidia vijana wengi ambao wataondokana na kuzurura na bahasha katika ofisi za umma na binafsi
kwa kutafuta ajira.
Waweza kutoa ushirikiano wako kwa kutuma chochote kwenye namba
TIGO PESA 0656701100 ridhwaa trust fund
VODA M-PESA 0768 771340 ridhwaa trust fund
au
Amana bank hqts,A/C 0033140413700001.registered trustees of masjid ridhwaa
Comments